Adeladius Makwega-LUSHOTO
Siku ya Aprili 29, 2022 Mwanakwetu alikuwa katika Mji wa Lushoto, mkoani Tanga. Mandhari ya mji huu ilikuwa ya baridi kali, manyunyu na mvua kubwa. Kwa kuwa alifika katika ofisi mojawapo iliyokuwa katika majengo ya Halmashauri hii ambayo sasa imepangishwa ili wajiongezee kipato. Wakati narudi kutoka huko alipita kandokando ya Kanisa Katoliki la Ekaristi Takatifu Lushoto Mjini Jimbo Katoliki la Tanga, kwa pembeni kuna nyumba ya makazi ya mapadri alishuhudia vibanda kadhaa vizuri kuzunguka nyumba hii.
Vibanda hivyo vilimvutia mno kwani
vimebadilisha mandhari ya eneo hilo kutoka kichaka na kuupamba vizuri mji huu
mkongwe ambao una Ikulu ya kwanza iliyojengwa na Mjerumani.
Alipokuwa anatazama vibanda ambavyo
ujenzi wake ulipitia hatua kadhaa za changamoto mara bomoa mara wekwa alama X
lakini sasa vimekamilika kwa ushirikiano wa waamini wa kanisa hilo na viongozi
wao.
Mwanakwetu akiyaona manufaa mengi ya
vibanda hivyo,
“Vinameondoa kichaka cha wigo mjini
na kuwa urembo unaopendezesha sehemu ya mji huu. pia kuliongezea kipato kanisa
hilo na tatu, kuongeza idadi wa wafanyabishara katika mji huu. Nne, hata
kuongeza bidhaa zinazouzwa Mjini Lushoto. Tano kusogeza huduma jirani na jamii
na kupunguza safari za wateja kwenda mbali kufuata bidhaa hizo na Sita kuongeza
mzunguko wa pesa katika eneo hilo.”
Mandhari ya vibanda hivyo ilimkumbusha
Mwanakwetu namna Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga linavofanya miradi kadhaa ya
maendeleo ikiwamo ya elimu, afya, ufugaji na kilimo inayosimamiwa na mapadri na
watawa kwa miaka mingi katika eneo hili lililopo Kaskazini Mashariki mwa
Tanzania.
Mwanakwetu akiwa anazunguka mji huo huu aliikumbuka barua moja ambayo aliwai kuandikiwa na Baba Askofu Antony Banzi wakati wa uhai wake mwaka 2017/2018 ambayo ni yake ya kwanza kuandikiwa na Baba Askofu katika maisha yangu.
“Mtu mdogo kama mimi kiimani na kwa
kila kitu inawezaji kupokea barua kama hii yenye tafakari nzito kutoka kwa Baba
Askofu Banzi na kusainiwa na yeye mwenyewe?”
Barua hiyo haikuwa na maelekezo ya
kiroho wala barua ya maombi ya kitu chochote kwa Mwanakwetu bali kwa nafasi yake
ilikuwa barua ya tafakari kutoka kwa Baba Askofu kwenda kwa mtu mdogo sana
Mwanakwetu.
“INAWEZEKANA,TIMIZA WAJIBU.”
Hayo yalikuwa maneno yaliyonukuliwa
na Askofu Banzi si kutoka kwa kauli mbiu ya TANU ya Julius Nyerere na Oscar
Kambona la hasha bali alibainisha kuwa amekuwa akifuatilia kauli mbiu hii
ambayo imekuwa ikibaki katika kila Kitabu cha Wageni kinachosaini iwe mjini au
kijijini na Mwanakwetu.
“Katika maisha ya binadamu na hasa
kwa kijana, jukumu lako ni kufanya kazi kwa bidii sana na usikatishwe tamaa na
mtu yoyote yule kwa kuwa inawezekana kukamilika kwa kutimiza wajibu tu kama
kauli yako mbiu.”
Alisema Baba Askofu Banzi katika
barua hiyo yenye kurasa mbili za maandsihi.
Baba Askofu Antony Banzi ambaye
alikuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga kwa miaka 26 tangu alipoteuliwa Juni
24, 1994 na kutawazwa rasmi septemba 15, 1994 aliufanya utume huo hadi
alipofariki dunia Disemba 20, 2020.
“Mwanakwetu alitafakari mno barua
hiyo lakini akibaki na maswali mengi juu ya Askofu Banzi. Je aliwezaje kuyaona
maandishi yangu kadhaa ya vitabu vya wageni vilivyokuwa vinaandikwa kauli hii
ya TANU na kusaini saini ya Mwanakwetu katika maeneo mbalimbali ya ofisi za
vijijini, mitaa na kata alizozitembelea kati ya mwaka 2016-2018 katika
Halmashauri ya Lushoto?”
Swali hilo Mwanakwetu anatambua fika
haliwezi kujibiwa na Askofu Banzi ambaye sasa amelala usingizi mzito kaburini.
“Mwanakwetu akiwa njiani kueleka
alipofikia alibaini kuwa kanisa si majengo yanayoonekana kwa ajili ya kusali tu
kanisa ni jamii husika ambayo inakaa pamoja ikifanya kazi mbalimbali za
maendeleo ili kuistawisha jamii hiyo.”
Mnapofanya kazi hizo za ustawi wa
jamii mnakutana na mnafahamiana vizuri, siyo lazima ukutane na Baba Askofu bali
unaweza kukutana na mwingine ambaye mtafahamiana huyo akakuelezea kwa mwingine
namna ulivyo iwe kwa mema au kwa mabaya.
“Raha ya milele uumpe ee Bwana na
mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani, amina.”
Mwanakwetu anatambua fika kuwa kwa
sasa bado JImbo Katoliki la Tanga
ahalipata aAskofu wake , kitendo cha kuyakumbuka meme ya kiongozi huyu wa
kiroho Mwanakwetu anaendelea kusali sala
zake ili jimbo Katoliki la Tanga kupta
Askofu wake , huku akimwomba balozi wa baba Mtakatifu nchini kumkumbusha hilo, hili Baba Mtakatifu
Fransisko amchague Askofo wa Jimbo hilo.
makwadeladius@gmail.com
0717649257
Post a Comment