Adeladius Makwega-MWANZA
Wakristo wameambiwa kuwa maisha ya leo yanachangamoto nyingi,
hivyo vipaji vya Roho Mtakatifu viwasaidie kuweza kuishi katika maisha mema,
kutenda mema na kuongozana kuyakata mabaya.
Kauli hiyo imetolewa na Mlei Mkatoliki ambaye alialikwa na Padri Samwel Masanja kutoa neno katika la misa ya Dominika ya Pentekoste, Mei 28, 2023, misa ya pili ndani ya Kanisa Bikira Maria Malikia wa Wamisionari Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza.
“Mimi na wewe tulibatiza na na tukapata Kipaimara, Je
tunayatumia vizuri Matakatifu ya Roho Mtakatifu? Tunayaheshimu hayo yote
tuliyopewa kutoka nyumba ya Bwana? Je watu wanayaonja matakatifu ya maisha
yetu? Je tunatangaza neno la Bwana kutoka kwetu sisi nakwenda kwa wengine? Sote
tunaalikwa kuwa mabalozi wa kuitangaza Injili maana Injili ya Yesu Kristo na
Kanisa lake lilianza siku ya Pentekoste.”
Ulipowadia wakati wa maombi ndani ya misa hiyo ya sherehe ya Pentekoste walialikwa walei kutoa maombi katika lugha tatu za makabila, Kiswahili na Kiingereza ambayo maombi hayo yalikuwa na ujumbe huu.
“Tunakushukuru ee Mungu kwa wema na baraka zako, tunasema
asante kwa siku hii muhimu ya kuadhimisha sikukuu hii ya Penntkoste,
unapotualika kila mmoja wetu kumpokea Roho Mtakatifu utujalie tuishi kwa
mapenzi yako.”
Wakati misa hiyo inamalizika Padri Samweli Masanja ambaye
ndiye Paroko wa Parokia ya Malya aliuchukua Mshumaa wa Pasaka uliokuwa kando ya
altare na kwenda nao Sakaristia.
Huku hali ya hewa ya eneo la Malya na viunga vyake ilikuwa na
jua kali wakati wa mchana na nyakati za usiku kukiwa na joto kali.
Post a Comment