Adeladius Makwega-MWANZA
Wagombea walioshiriki katika kinyanganyiro hicho ni pamoja na
Wiliam Shelukindo, Abubakari Mshihiri, Leonard Kaoneka, Joseph Kijangwa, Lea Shemndolwa,
Raphael Shemtambo na Abdulkadir Kaniki.
Katika Jimbo hilo mwaka 2010, Januari Makamba
alipata kura 14,612, akifuatiwa na mbunge anayemaliza muda wake William Shelukindo
kura 1,700 na Abdi Mshihiri kura 609. Januari Makamba alishinda bila ya kupigwa
katika katika uchaguzi mkuu jimboni hapo.
Miaka mitano baadae yaani 2015 CCM
iliagiza wapiga kura za maoni kuwa wanachama wake wote katika kila jimbo, kwa
jimbo la Bumbuli kulikuwa na wana wa CCM wapiga kura wanaokaribia 21, 000 na
ushehe.
Wagombea walioshiriki walikuwa ni wanne Yusufu Juma Shemkavi
ambaye alipa kura 69, Abubakari Juma Mshihiri alipata kura 205, Abdukadri Abdi
Mgheni 2403 na Januari Makamba aliyepata kura 17,805 ambaye ndiye alikuwa
mshindi, Huku akipita bila kupigwa katika uchaguzi mkuu wa jimbo hilo.
Miaka mitano ilikwisha uchaguzi wa kura za maoni CCM 2020
ulitumia wajumbe jimboni kupiga kura za maoni, maamuzi hayo ya CCM ambapo baada
ya sarakasi nyingi ambazo Mwanakwetu alizifuatilia hatua kwa hatua Mshihiri Madiwa
alipata kura 12, Abdulkadiri Kaniki alipata kura 21 na mshindi akiwa Januari
Makamba aliyepata kura 680, huku wagombea wengine kadhaa wakipata kura 2, 1 na
sufuri akiwamo Kapteni Nyarali ambaye alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Bumbuli tangu mwaka 2016.
Ukiyatazama matokeo hayo ya kura za maoni CCM kwa miaka 10
ndani ya chaguzi tatu utabaini kuwa Januari Makamba alimvuka mwenzake
anayemfuta kwa kura 12,000 (2010), kura 14,000(2015) na kura 650 (2020).
Kwa ukweli wa wazi Januari Makamba alishinda kura hizo za
maoni.
Swali ambalo linakuja je ushindi huo aliupataje?
Jimbo la Bumbuli ni jimbo la watu masikini kabisa kama ilivyo
majimbo mengi ya Tanzania yetu, Pale Bumbuli kuna kata inaitwa Soni ambapo kuna
akina mama wanaofanya biashara ya kuuza nyanya, vitunguu, matunda , karoti ,
kabichi na bidhaa kadhaa ndogo ndogo kutoka mashambani.
Mandhari ya Stendi ya Soni punde basi au gari likifika hapo
mara akina mama hao wengi wanasogelea madirisha wakiiva hizo bidhaa , wakiwa na
maneno mazuri , lugha tamu , lugha ya biashara yenye maelewano mazuri sana na
wateja wao, msomaji wangu kama haujawahi kusikia lugha tamu masikioni mwako
nenda Soni.
“Baba nitakuongezea, Baba lipa shilingi
2000 nitakupa mapeasi yote, Baba makabichi matano shilingi 2000. Baba nunua mapeasi
haya ya leo matamu kweli kweli, Baba mkwe! Wewe ni mteja wangu kila mara leo
nunua matunda damu.”
Mwanakwetu hayo ni maneno ya kawaida
kutoka kwa akina mama hao wa Stendi ya Soni
ambao ni wakwe na shemeji wa Mwanakwetu, hilo msomaji wangu naendelea
kulirudia kila mara.
Pata picha ya mtoto wa mama anayeuza mapeasi hayo au matunda
hayo hapa Stendi ya Soni anaweza kuelezwa namna ya kushiriki siasa za Jimbo la
Bumbuli na aweze kupata kura 14,000?
Mwanakwetu anafikiri hayo akilini mwake na anabaini kuwa mjuzi
wa somo la kura 14,000 za maoni kila baada ya miaka au kura 600 za wajumbe linalo
mwalimu wa vitendo ambaye ni Januari Makamba, ndugu yao na Msambaa mwenzao.
Je kama tukimpa kazi hiyo mhe. Januari Makamba amuelekeza
mtoto huyo wa muuza mapeasi, je anaweza kueleza kura zile 14,612 (2010), kura
17,805 (2015) na kura 680(2020) zilivyopatikana?
Kwa hakika Mwanakwetu anatambua kuwa Bumbuli ni jimbo la watu
masikini huku maneno haya anayarudia kila mara, Ukifika Bumbuli ukifuatilia
utabaini kuwa familia nyingi ni za wakulima wadogo wadogo wa bustani katika vitivo,
wakulima chai na wakulima wachache wa kahawa. Wakulima wengi wanafugaji kuku,
bata , mbuzi na wachache mno wanafuga ng’ombe kati ya 1-5 kwa kuokoteza.Wengi
wa wakulima hao koo zao zilihamia hapo kufanya kazi katika mashamba ya mkonge
wakiwa MANAMBA wakioleana na Wasambaa wa asili. Hawa akina Makamba ni zile koo
masikini kama walivyo akina Mwanakwetu kule kwao Mrundu Mahenge-Ulanga ,
Morogoro, kumbuka TANU kiliwaunganisha hao masikini na kudai uhuru na
kuunyakua.
TANU ilikuwa na matajiri lakini waliwahakiki mno na kutambua
nia zao kama hazina hila, ndipo walishirikiana nao kwa uhakiki wa kina. Kwa
hiyo mtoto wa muuza mapeasi wa Stendi Soni lazima umpe majibu ya namna
unavyoshiriki siasa ili nayeye aweze kushiriki maana CCM ni zao la masikini wa
TANU na ASP, utaki usitake.
Mwanakwetunakumbusha hili,
“John Rupia, tajiri na Bilioniea wa TANU aligombea uchaguzi Usukumani
/Unyamwezini kura za maoni alishindwa na mtu masikini kabisa.”
Kwa nini Mwanakwetu anaona umuhimu wa hilo?
Hao masikini wakielezwa na kupata majibu na kuweza kupenya
watatambua kuwa ahaaa kumbe bado chama hiki ni chao.
Pili CCM lazima ishituke na ikumbuke kuwa walichokifanya
masikini wa TANU na ASP kuungana, wasipopewa majibu watayafirikiri yale yale ya
wakati wa TANU na ASP utake usitake.
Kama mtu anashinda kwa kura nyingi kwa kutumia mbinu anazofahamu
yeye au rafiki zake hilo linaweza kusababisha mtu akawa anashinda kwa nguvu za watu
wengine na akafanya kazi kwa maslahi ya watu hao wengine siyo maslahi ya wengi
ambao ni wanyonge.
Mtu anaweza akatambua kuwa Mwanakwetu ni maskini wa kutupwa, kwao
ni manamba wa mkonge , hawana ng’ombe 100,000 wao wamezoea kulima miraba,
tukimpatia shilingi bilioni 1 akashinda ubunge atatusaidia katika mambo yetu,
Mwanakwetu atakuwa amenunuliwa, , Mwanakwetu atakuwa kiganjani kwa mtu kwa
maana anayemlipa mpiga filimbi ndiye mchagua wimbo.
0717649257
Post a Comment