Serikali imesema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndicho chenye
miradi yote ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa hivyo kisisite na kinapaswa kushirikishwa
katika hatua zote ili kiwezo kutoa maoni na ushauri wake wakati wa utekelezaji.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza ndugu Balandya
Elikana akiwa Malya Wilayani Kwimba wakati akitembelea miradi kadhaa ya
maendeleo katika mkoa huo ambayo inatekelezwa kwa nguvu za wananchi, Serikali
za Mitaa na Serikali Kuu, Juni 30, 2023.
“Diwani wa CCM upo? Unaufahamu huu mradi? Je unafuatilia
utekelezaji wake? Unautambua kuwa huu ni mradi wako? Pale pesa zinapochelewa
usisitwe kufika katika ofisi yangu ili tuweze kutambua shida ni nini? Na nani
anakwamisha hilo. Jambo hili ninalisema si Malya tu bali mkoa mzima wa Mwanza
katika miradi yote, iwe ya Serikali Kuu au Serikali za Mitaa.”
Katibu Tawala Elikana alionekana akiambatana na viongozi
kadhaa wa mkoa huo kutoka kamati mbali ikiwamo Kamati ya ulinzi na Usalama waliovalia
sare za majeshi yetu mbalimbali ; JWTZ, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji , Jeshi la Magereza na Askari Kanzu kadhaa.
Msafara huu uliombatana na kiongozi huyo ulionekana wakikagua
miradi kadhaa katika Wilaya ya Kwimba ambapo walipofika Chuo cha Maendeleo ya
Michezo Malya walikagua Jengo la Hosteli la wanachuo ambao ni mradi wa bilioni
kadhaa unaogharamiwa na Serikali Kuu ambapo kwa sasa jengo hilo lipo katika
hatua nzuri.
Akizungunza katika lugha ya kushauri, wakatii mwingine akitoa
maagizo ya serikali kwa kutumia lugha ya staha na heshima mara kadhaa kiongozi huyo
Mkoa wa Mwanza alionekana kushirikiana kwa karibu na aliongozana nao.
“Hapo mmeona pana marekebisho, itabidi mfanye marekebisho
hayo mapema eeeh…! Tunaziomba hizo taarifa mapema, mna imani kuwa huu mradi
utakamilika mwaka wa fedha wa 2023/ 2024?. Natambua hapa sisi serikali tumeweka
pesa nyingi.”
Katika ziara hiyo, wakiwa katika mradi wa Hosteli ya Chuo cha
Maendeleo ya Michezo Malya walitumia zaidi dakika 79 huku Mkuu wa Chuo cha Maendeleo
ya Michezo Malya Richard Mganga akijibu maswali kadhaa na ufasaha mkubwa pia
akipokea maelekezo kadhaa ya serikali yaliyotolewa ziarani hapo.
Mara baada ya dakika 80 kutimu, ugeni huo uliingia katika motokali
zao zilizoongozwa na vIjana wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza,walionekana wakipanda
Toyota Land Cruizer-I hz kwa ukakamavu mkubwa na kuongoza msafara huo.
Mwandishi wa taarifa hii akiwa kandoni ya ugeni huo alitumia
fursa hii na alizungumza na viongozi kadhaa wa CCM kutoka Kata ya Malya
waliovalia sare za CCM akiwamo Bi Hawa Salehe ambaye alijitambulisha kama
Katibu Kata CCM Malya huku akisema,
“Nashukuru kwa maelezo hayo ya Serikali na namshukuru mno Katibu
Tawala wa Mkoa wa Mwanza kwa kututambua , kwa kufika Malya na maaagizi yake yote,
kata ya Malya itatekeleza kama yalivyoelekezwa. Tutajipanga na Diwani wetu
kuhakikisha tunapokagua miradi ya Kata yetu na miradi yote ya Serikali Kuu katani
itaingizwa katika orodha na kukaguliwa ipasavyo.”
Mwandishi wa ripoti hii pia alibaini kuwa Bi Hawa Binti Salehe
aliambatana na Diwani wa Malya mhe. Atanas Niga, Katibu Mwenezi wa Kata ndugu
Mohamed Mangwela na Mwenyekiti wa Vijana Kata ndugu Manyunga Kidoyayi.
Post a Comment