NIA YA MCHUNGAJI SI KUMPOTEZA KONDOO

 


Adeladius Makwega–MWANZA

Wanachuo wa Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya Juni 30, 2023 wameshukuru wanachuo waliohitimu chuoni hapo mwaka 2022 kwa kuwapa zawadi ya seti ya runinga wakisema kuwa huo ni utaratibu wao waliojiwekea kila mwaka na hata wahitimu wa 2021 walikabidhiwa zawadi kadhaa na wale wa 2022 kulingana na uwezo waliokuwa nao.



Akizungumza katika mapokezi ya zawadi hiyo Baptist Kapinga ambaye alikuwa Rais wa Serikali ya wanachuo Chuoni hapo 2021-2023 alisema kuwa anashukuru kwa moyo huo wa kiungwana pia aliongeza kuwa,

“Hata sisi, tunaomba Mungu tukihitumu salama tutafanya hivyo, tunatoa ahadi mbele ya wanachuo wote kuwa tunajipanga kuchangishana na tutakuja na zawadi kwa ajili ya wenzetu mnaobaki hapa chuoni.”

Mara baada ya mapokezi ya zawadi hiyo kulifuatiwa zoezi la Baptist Kapinga na makamu wake kukabadhi uongozi wa serikali ya wanachuo baada ya uongozi mpya kula kiapo na kuanza kazi.

Akizungumzia changamoto kadhaa ambazo uongozi wake ulizipitia Mwalimu Kapinga alisema,

“Ninakumbuka kuwa mwaka 2022 wakati wa kampeni nilitoa ahadi kuhakikisha wanachuo wote nilioanza nao, ningehakikisha wanahitimu salama, wapo wanachuo wachache ambao walipata changamoto zao binafsi, hivyo yale ambayo yalikuwa juu ya uwezo wangu yalitokea lakini kwa nafasi yangu, nimetimiza wajibu wangu , kwa akili na nguvu zangu zote, nawaombeni na kubwa kweni kila mmoja afuate tu lile ambalo limemleta hapa Malya, maana nia ya mchungaji si kumpoteza kondoo wake yoyote yule, bali wote wafike salama.”



Akizungumza huku wanachuo hao wakishangilia, mwandishi wa ripoti hii ameshuhudia shughuli hizo zote zikiwashirikisha viongozi kadhaa wa chuo hiki na zikiambatana na burudani za kila aina na michezo kadhaa.

 










0/Post a Comment/Comments