MASHA
“Husna hana shida, kwa hakika ameayagusa mno maisha
yangu na bila ya yeye hata hii biashara ninayoifanya hii nisengekuwapo hapa,
sasa hibi nimeacha kufanya vibarua bali nina biasahra yangu mwenyewe, maana amenishika
mkono na siyo mimi peke yangu bali ni wengi.”
Hayo ni maelezo ya Jamila Ngogo mkazi wa
Vuri Lushoto,Mkoani Tanga akizungumza wakatia makala haya yakitayarishwa.
Maelezo ya Bi Jamila yananukuliwa
mwanzoni kwa sababu nyingi maana hivi karibuni mbunge huyu wa viti maalumu
mkoani Tanga, ametembelea vikundi vya akina mama vilivyokopeshwa fedha kupitia
asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Tanga. Mbunge huyo
amekuwa karibu na Wanawake wengi mkoa wa Tanga kutokana na kufanya kazi kwa
pamoja na kidugu, alitembelea vikundi vya ufugaji kuku, usagaji nafaka pamoja
na uuzaji wa unga wa chakula , hiyo ikiwa ratiba yake kila akitoka Bungeni.
Akizungumza na akina mama hao katika kikao kilichofanyika Kata
ya Mnyanjani na kisha mkutano kule Mabokweni ambako alizungumza na wananchi wa
Kata za Nguvumali na Chumbageni alisema,
”Mikopo waliyopewa vikundi hivyo vya ujasirimali watumie pesa
hizo kujenga uchumi wao na kupiga hatua kimaisha.”
Aliongeza kuwa fedha walizopewa zinatakiwa zirejeshwe ili
ziweze kukopesha wajasirimali wengine kwa kuwa dhamira ya serikali ni kuwasaidia
ili waweze kuinuka kiuchumi. Hata hivyo, alisema mikopo hiyo inayotolewa na
serikali asilimia nne vijana na wanawake na asilimia mbili makundi ya watu
Wenye ulemavu, kwasasa imesitishwa ili kuboresha kwa makundi hayo tofauti na
awali. Mbunge huyo aliipongeza Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa kuweza kutoa
fedha nyingi za mikopo tofauti na maeneo mengine aliyopita baada ya kukuta
kikundi kimoja kimepewa mkopo wa zaidi ya shilingi milioni 40.
"Kiukweli nimetembea wilaya nyingine na hata kule kwetu
Lushoto hakuna mjasiriliamali ambaye Halmashauri imeweza kumkopesha fedha kama
hizi sana sana huko wanawakopeshwa shilingi milioni mbili au tatu,"
Kinagaubaga aliwaambia akina mama hao kuwa fedha hizo wasione
zinatolewa tu kwa bahati mbaya bali ni usimamizi mzuri wa mbunge wa jimbo la
Tanga Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya.
"Muungeni mkono mbunge wenu (Ummy) ni kiongozi makini na
ndiyo maana ameaminiwa na kupewa uongozi, mnaweza msione umuhimu wake lakini
nawaambia mshikeni sana mbunge wenu."
Mhe Husna katika ziara yake katika jimbo la Tanga shabaha
yake ilikuwa ni kukutana na wananchi na kujua changamoto zao lakini pia
kuwaomba wananchi wamuunge mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi
nzuri anayoifanya nchini ikiwemo mkoa wa Tanga. Kwani kina mama wanao wajibu
mkubwa wa kumuunga mkono Rais licha ya kuwa mwanamke mwenzao lakini ametekeleza
miradi mingi ya maendeleo nchini katika sekta za afya, elimu, maji na miundo
mbinu.
Wakizungumza kwa nyakati tafauti akinanana kadhaa wa mkoa wa
Tanga ambayo mawazo yao yanafanana na ya Jamila Ngogo wa Lushoto ambayo
yanaonekana mwanzoni mwa makala haya wanasema,
“Dada Husna anachapa kazi sana, ameendelea kutuunganisha wanawake
wote wa mkoa wa Tanga na kila mara tunapomuhitaji afike katika kufungua vikoba
vyetu na hata katika magawiwo ya fedha za vikundi vyetu amekuwa hodari sana wa
kufika na kutuongezea nguvu na kutushika mkono.”
Hayo ni ya Bi Aisha Mlelwa wa Mkinga.
“Tulikuwa hatuna kikundi, mh Husna alifika hapa,
akatuhamasisha vizuri na kuweza kuanzisha kikundi chetu, mwongozo wake
umetujenga vizuri, sasa tunasifa zote, tumeambiwa na Halmashauri yetu ya Korogwe
Mji chini ya mkurugenzi wake Tito Mganwa kuwa tutapata fedha katika mgao wa robo
ya pili ya mwaka wa fedha 2023/ 2024, hakika.Mhe .Husna Sekiboko ni hodari na kuchanja
mbuga za Maendeleo ya Tangamano.”
Alisema Rehema Madenge mkazi wa Mji
wa Korogwe.
Mhe. Sekiboko aliingia Bungeni kwa
mara ya kwanza mwaka 2020, kitaaluma ni mwalimu mwenye Shahada ya Kwanza ya Elimu
ya Sayansi ya Siasa na Historia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mzaliwa wa
Lukozi Lushoto mkoani Tanga. Kabla ya kuwa mbunge aliwahi kufanya kazi kadhaa
ikiwamo Ualimu katika shule za kutwa mbili za Masasi na Shekilango na baadaye akateuliwa
kuwa Katibu Tawala wilaya mojawapo ya mkoa wa Lindi.
Post a Comment