Adeladius Makwega-MWANZA
Padri Samwel Masanja Paroko wa Parokia ya Malya, alisimama na
kusoma injili katika misa hiyo ya mazishi ndani ya Kanisa la Bikira Maria
Malkia wa Wamisionari, Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Alasiri ya Julai 3, 2023
huku kanisa hilo likijaa waombolezaji tele.
Bwana awe
Nanyi!
Awe Rohoni
Mwako
Somo katika
Injili ilivyoandikwa na Yohaneee…
Utukufu
Kwako Eee Bwanaaa…
Yesu alipofika Bethania, alimkuta Lazaro ameshakuwapo kaburini,
yapata siku nne , na Bethania ilikuwa karibu na Yelusalemu, kadili ya maili
mbili hivi, na watu wengi katika Uyahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na
Mariamu, ili kuwafariji kwa habari ya ndugu yao. Basi Martha aliposikia Yesu
anakuja alikwenda kumlaki, na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani.
Basi Martha akamwambia Yesu,
“Bwana! Kama ungalikuwapo hapa ndugu yangu hangali kufa,
lakini hata sasa najua ya kwamba yoyote utayaomuomba Mungu, Mungu atakupa.”
Yesu akamwambia,
“Ndugu yako atafufuka.”
Martha akamwambia ,
“Najua atafufuka siku ya mwisho.”
Yesu akamwambia,
”Mimi ndimi huo ufufufo na uzima, yeye aniaminiye mimi ajapokufa
hatakufa, ataishi, naye kila aishiye na kuniamini hatokufa kabisa ataishi
milele, Je unayasadikia hayo ?.”
Akamwambia,
”Naam Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiyo Bwana, Yesu
Kristo, Mwana wa Mungu yule ajaye ulimwenguni.”
Neno la Bwana!
Sifa Kwako Eeee Kristo.
Waamini wanaketi katika viyi huku
sauti zinasikika namna wanavyoketi.
“Mimi ndimi huo ufufuo na uzima, yeye
aniaminiye mimi ajapokufa atakuwa anaishi, naye kila aishiye na aniaminiye
hatokufa bali ataishi milele.”
Padri Masanja anayarudi maneno hayo
ya Injili ya Yohane ambapo Yesu anamwambia Martha, huo ni katika utangulizi wa
mahubiri ya Misa ya Mazishi huku jeneza likiwa kando kanisani.
Padri Masanja anaendelea kuhubiri, ndugu
zangu wapendwa, hayo ni maneno ya Yesu Kristo mwenyewe, ni maneno ya uhakika,
ni maneno ambayo yanamfanya Martha aungame Imani.(huku ndani ya kanisa sauti ya mtoto mdogo akiwa miongoni mwa waombolezaji akilia
ikisikika).Akubali uwezo wa Mungu, akubali utekaji wa Kristo , anapomwambia
nimesadiki ya kwamba wewe ndiye Kristo Mwana wa Mungu.
Ndugu zangu wapendwa, ni jioni ya leo
iliyotukusanya hapa ni kwa ajili ya huyu mwezetu, ambaye amehama kutoka katika
dunia hii, anaingia katika maisha mengine mapya, maisha ya umilele. Ambayo hayo
maisha mapya anayoingia ndugu huyu, sisi tumekusanyika hapa kuyaombea yake ya
maisha ya milele yawe ya furaha, yawe maisha ya amani milele.
Ndugu zangu wapendwa, sisi ambao
tumepata bahati ya kumjua Mungu, ya kumuungana Mwenyezi Mungu, lakini zaidi
tukapiga hatua si kwa maneno tu, bali kwa vitendo, leo tunaadhimisha maisha ya
huyu ambaye ni mwenzetu, ambaye naye katika maisha yake ya hapa dunia bila ya shaka
atakuwa alikuwa amepiga hatua hiyo ya kukubali kumtumikia Mungu , na hilo
alilitangaza pale alipokubali kubatizwa na kupokea imani, kutoka katika hali ya
upagani na kumtumikia Mungu ili siku moja aweze kuungana naye, siku moja aweze
kukutana naye .
Ndugu zangu wapendwa, huo ni ushujaa
wa pekee, ambao mimi na wewe yamkini tumeufikia, tunaendelea kupambana katika
kuupalilia , ili nasi litakapotokea jambo kama hilikwa ndugu zetu wengine,
tusali, tukiamini kuwa tupo katika makao salama.
Ndugu zangu wapendwa, tumesikia
katika somo la kwanza kuwa mwenye haki anapokufa, tunaamini anakuwa katika
mikono salama, maana Mungu anamchukua katika waovu ili apumzishe , amuweke
mahala pa ustawi, amuweke pahala ambapo ni salama. Hilo siyo jambo la
kushangaa, mwenye haki ataishi milele, mwenye haki yumo mikononi mwa Mungu , ni
jambo ambalo mimi na wewe tunaalikwa kulipokea na kulitafsiri katika maisha
yetu, tunaweza kujiuliza
“Je mimi ni mwenye haki ? Je wewe ni
mwenye haki?”
Ndugu zangu wapendwa, kifo ni tukio
linalotufika bila matarajio, bila hata taarifa, kifo kinafika bila kupiga hodi,
kwa sababu hiyo tunaalikwa kuwa macho, tunaalikwa kukesha kwa sababu hatujui
siku wala sala. Katika Injili ya leo ni Injili ya masikitiko ambapo familia ya
Martha .Maria na Lazaro, hapo mmoja wao ameanga dunia ambaye ni Lazaro. Familia
hii walitegemea Yesu awatembelee mapema lakini haikuwa hivyo anafika siku ya
nne baada ya kifo. Yesu alikwenda baadaye, anapofika apashwa habari ya kifo cha
Lazaro.Yesu anamwambia Martha,
“Usiogope, usijali kwa kuwa kaka yako , ndugu yako atafufuka.”
Martha anajibu naam najua atafufuka
siku ya mwisho, Yesu anamfungua macho kuwa yeye ndiyo huyo ufufuo na uzima yeye
amuaminiye ataishi.
Padri Masanja alaiendelea kuhubiri, ndugu
znagu katika maneno hayo sisi tuliokutana leo hii tuliofika kumsali ndugu huyu
tunamini haya kwa ndugu yetu,
“N mzima, natunamini anaishi, tunaamini yu hai kwa sababu
yeye angali hai alisadiki na aliungama na kupokea juu ya fundisho la Kristo mwenyewe
na kwa kusadiki hivyo tunaaamini kwamba japokuwa amekufa yu hai yu mzima ,akiishi
katika Kristo. Sasa hatupaswi kuwa na huzuni,hatupaswi kuwa na simanzi ,
ikitokea hivyo huzuni zetu iwe kusali na kumuombea mpendwa wetu ambalo ndilo
hilo linaloafanyika hapa.”
Yalipokamilika mahubiri hayo, misa iliendelea
hadi mazishi ya kijana Bendikti aliyezaliwa 2002 kifo chake kilitokana na ajali
ya bodaboda na kuzikwa.
Mwanakwetu kwa heshima zote na kwa
hisani yako wewe msomaji wako ameamua kuyaweka mahubiri hayo ya Padri Samwel
Masanja katika maandishi ili yaweze kupitiwa na kila mmoja wetu atayejaliwa
kuyasoma maana kila uchao sote tunafariki au tunapoteza wapendwa wetu.
Swali kwangu na kwako ni hili,
“Je mimi ni mwenye haki ? Je wewe ni
mwenye haki?”
Nakutakia siku njema.
0717649257
Post a Comment