Adeladius Makwega-MWANZA
Mwanakwetu alikuwapo nyumbani
kwake, hiyo ikiwa jioni ya Agosti 18, 2023, hapo katulia tuli keshamaliza kuusoma
waraka wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, wakati akisoma waraka huo wenye
kurasa 8 mwanzoni moyoni alijiuliza kwanini waraka huu umetolewa kwa kuchelewa ?
Baadaye
swali hilo lilijibiwa na maelezo ya kina ya waraka huo ambapo ulionesha kulikuwa
na majadiliano baina ya TEC na upande uliombwa kufanya maamuzi.
Huku Mwanakwetu akisema
moyoni,
“Waraka
huu unapousoma unaweza kujiuliza maswali na kujijibu wewe mwenyewe kadili
unavyousoma, maana unajieleza wazi wazi.”
Mwanakwetu
wakati anausoma alikumbuka aina nne za usomaji,
“Skimming, Scanning, Extensive
na Intensive Reading.”
Kumbuka msomaji wangu Mwanakwetu
yu nyumbani kwake na alipousoma waraka huo alitumia Intensive Reading, akawa
anautafakari moyoni.
Mara akaingia katika kundi
mojawapo la mitando ya kijamii na kukutana na mijadala juu ya waraka huo kutoka
kwa wadau mbalimbali wakitoa maoni yao, Mwanakwetu akayasoma vizuri wengine
wakimshambulia Padri Kitima, Mwanakwetu akasema hayo siyo mawazo binafsi wa
Padri Kitima bali ni msimamo wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzamia na ukurasa
wa saba na wanane unajibu hilo kwa orodha ndefu wa MABABA WALIOKETI katika jambo hilo kutoka 1-37-Kutoka Askofu Mkuu
Gervas Nyaisonga hadi Askofu Mteule Thomas Kiangio.
Pia Katika kundi hilo
Mwanakwetu akakutana na maneno haya,
“Shemasi hata upadri hajakaribia !”
Wadau wa kundi hilo wakawa wanatiririka
kwa sentensi tele, mwingine akasema,
“Basi wamfukuze.”
Mwanakwetu
anaendelea kusoma ujumbe unaofuata ambapo mdau mwingine akasema,
“Ni daraja dogo sana, unajiondoa
mwenyewe tu, haufukuzwi.”
Maoni
yanaendelea kuporomoshwa na huku mdau mmojawapo miongoni wa mwenye maoni hayo
juu akaugeuza usikani gafla , akasema maneno haya ,
“Ana haki ya kutoa maoni yake,
pia he is a free man, hafungwi na Kanisa.”
Msomaji
wangu Mwanakwetu anaendelea kusoma kila ujumbe unaofuata, sasa akaibuka mdau
mwingine,
“Shemasi vs Maaskofu? Hamna
shemasi humo.”
Msomaji
wangu Mwanakwetu anaendelea kusoma ujumbe huo huku akicheka kwa sauti maana awali
alikuwa anachekea moyoni na sasa akaibuka mkubwa mwingine akaja na hili,
“Hakuna shemasi humo, hapa
Shemasi magirini, from the factory.”
Msomaji
wangu kicheko cha Mwanakwetu kikaongezeka, kumbuka wadau wa kundi hilo ambalo
ni la wasomi wenye shahada za elimu mbalimbali wanafunguka, wengine wanatuma
michoro na picha za ishara ya kucheka na kukubaliana na hoja zinazotolewa kwa wajumbe
wote wanaotoa mawazo yao.
Hiyo
sasa ni saa mbili usiku, mara Mwanakwetu akabanwa na njaa na kiu ya maji, kwa bahati
mbaya na nyumbani kwake hakukuwa na kitu, alitoka nyumbani kwake na kwenda
kununua chakula na maji ya kunywa.
Msomaji
wangu hapo pahala anapoishi muungwana Mwanakwetu kila akielekea dukani na
mikahawani lazima apite Kanisa Katoliliki jirani ambalo lina ukumbi mkubwa unakodishwa
kwa watu wenye harusi na sherehe mbalimbali.
Akiwa
anapita kando na Kanisa hilo akausikia wimbo huu ukumbini,
“Ingekuwa hivyo wezi wangeenda,
Ingekuwa hivyo wachawi wangeenda,
Ingekuwa hivyo waongo wangeenda,
Bwana…
Bwana wa Bwana hapokei rushwa,
Bwana wa Bwana hapokei rushwa…”
Wimbo huo unaimbwa ukumbini
naye Mwanakwetu akawa anapita njiani kuelekea mkahawani mkononi akiwa na tochi
nyeusi huku sasa na yeye akivutiwa kuimba kiitikio cha wimbo huo,
“Bwana wa Bwana hapokei rushwa.”
Mwanakwetu akiimba kiitikio
hicho huku boda boda na baiskeli zikimpita kwa kasi mawazo yake ni kuwahi kula
mkahawani.
Mwanakwetu upo?
Mwanakwetu alifika mkahawani kula na baadaye dukani na
kuyanunua maji kisha kuianza safari ya kurudi nyumbani kwake, huku akilini
mwake akiukumbuka mno ule mjadala wa shemasi yule aliyepachika jina la Shemasi
Magirini.
Nakutakia siku njema.
0717649257
Post a Comment