Adeladius Makwega-Pugu&Malya.
Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania mhe. Mizengo Pinda amesema kuwa zamani kwake ilikuwa ngumu
kukumbuka kuwa imefika siku yake ya kuzaliwa lakini muda ulivyokuwa unasonga
akawa anapata ujumbe kuwa leo ni siku yako ya kuzaliwa kutoka kwa watu
mbalimbali, jambo hilo linampa faraja sana.
Hayo yamesemwa na mhe Pinda Agosti 27, 2023 nyumbani Kwake
Pugu Jijini Dar es Salaam alipotembelewa na kundi na vijana kadhaa waliowahi
kuguswa kwa namna mbalimbali katika maisha yao na kiongozi huyu mstaafu.
“Ninawashukuru mno kwa niaba yangu na mama Tunu kwa kufika
hapa kwangu na kutukumbuka,, kwa mawazo nilitamani tukutane hapa, ni jambo zuri,
kwani Mungu ametujalia uhai, najua mpo katika shughuli mbalimbali za kutafuta
riziki, siku ya kuzaliwa siyo lazima ifanyike siku ile ile, kuisogeza mbele
siyo shida , nawashukuru kwa zawadi zenu mlizonipatia. Natambua na kuheshimu
sana zawadi hizi, Unapopewa zawadi usiitazame tu ile zawadi, bali natazama ule
upendo wenu kwangu na kwa mama Tunu, kwa kutukumbuka, mkaanza kuhangaika na
kuzitafuta hizi zawadi, Mungu awabariki sana.”
Akiendelea kuzungumza mbele ya
wawakilishi wa kundi la vijana hao karibu 200 Mhe Pinda ambaye alitimiza miaka
75 Agosti 12, 2023.aliongeza kuwa,
“Moyo wenu huu napenda uwasaidie wengine ,msaada kwa mwingine
si utajiri, ni ile hali ya kujipima wewe na yule unayemsaidia, hicho ni kitu kikubwa
sana, unaweza kuwa na mashati 18 mengine umeyaacha tu wala hayavaliwi, lakini
yupo mtu anahitaji shati moja tu. Jamani yakusanyeni yapelekeni kwa wazee hao, yapelekeni
kwa wahitaji. Huo ni moyo wa upendo hiyo ni karama, Mungu kakupa unatakiwa uitumie
kusaidia wenzako. Fanyeni hivyo hata katika mazingira mnayoishi, kuna bibi na
babu wengi wanaishi katika mazingira magumu. Usingoje bibi/ babu huyo aseme anaomba
hiki na kile, kusanya shati na doti ya khanga mpeleleke mara moja na atakushukuru
kweli kweli.
Akizugumza kwa unyenyekuvu mkubwa
kama mtu ambaye hakuwa na mamlaka yoyote, akitamka neno kwa neno mbele ya
vijana hao mhe Pinda alisisitiza kuwa,
“Ninawaombeni sana kila mmoja, kwa nafasi yake, kila wakati
na kila mwaka muwawatembelee na kuwasaidia wahitaji sambamba na siku yangu ya
kuzaliwa.”
Mara baada ya mhe Pinda kusema hayo Mwenyekiti wa vijana hao ndugu
Edward Clement Kyungu alisimama na kusema haya,
“Tunakushukuru sana kwa
kutupokea, tunakushukuru sana kwa kutukumbuka, tunakutakia maisha mema,
tumeyapokea yote uliyoyasema na tutayatekeleza kwa vitendo na uhodari mkubwa,
Mungu akubariki kwa kutimiza miaka 75 ya kuzaliwa.”
Vijana hao kwa pamoja waliimba wimbo
wa kuzaliwa, wakakata keki na kupiga picha ya pamoja.
Mwenyekiti Kyungu aliambatana na
viongozi wenzake akiwamo Make Apolinari Nyema (Mhazini), Vivian Nyanjala Mtebe
(Katibu) na Lilian Phidelis Mwidunda( Makamu Mwenyekiti) .
Mwadishi wa ripoti hii alivutiwa sana
na sebule ya kijamaa ya mhe Pinda huku ikipambwa na picha moja kubwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mhe.Samia Suluhu
Hassan iliyoonekana amevalia mavazi yake rasmi ya CCM.
(Makamu Mwenyekiti Liilian Mwidunda)(Picha ya ilivyomvutia mwandishi)
Post a Comment