KINACHOJENGWA KINAWEZA KUBOMOLEWA

 


Adeladius Makwega-MWANZA

Kwa muda wa mwezi mmoja  Mwanakwetu amekuwa akifuatilia tukio la mama mmoja ambaye alikwenda kutibiwa Hospitali ya Mlonganzila, na alipewa huduma  nzuri za matibabu kutoka hospitali hiyo ya umma.

Mwanakwetu kwa heshima zote anatoa pongezi wa Hospitali hii ya Mlonganzila kwanza kwa watumishi wote  na pili kwa viongozi wote kwa nzuri.

 Mwanakwetu anasema,

‘ Kuanzishwa kwa Hospitali hii kumesaidia  kabisa kuziloga huduma mbovu za afya na sasa huduma zake ni nzuri, hongereni sana kwa kufanya kazi kwa ufanisi. Mhe Rais Samia Suluhu Hassan popote ulipo mama yetu kama unachagua Mganga Mkuu wa Taifa, kama unachagua  katibu Mkuu wa Afya, vyeo vyetu  vya Afya  kuna wadada na vijana wanachapa kazi mno Hospitali ya MLONGAZILA , mama  watazame kwa jicho lako makini , hawa vijana, watazameni sana, wanakupa heahima kubwa mhe Rais samia na wanakupa jina zuri kwa raia wako.’

HEKO MLOGANZILA

Mama mgonjwa  alipofika mapokezi Mlonganzila alitoa kadi yake ya NHIF na kuwapa wahusika ambao sehemu yao ni  watumishi wa Mlonganzila na sehemu ni watummishi  NHIF, ambapo sasa hivi wanashinda mahospitalini.Taratibu za matibabu zilifanyika vizuri na kulazwa ili siku iliyofuata mgonjwa huyu afanyiwe  upasuaji .Alipokuwa anapewa kitanda Ili kulazwa aliuliza, jamani nina kadi yangu ya NHIF ninahitaji maana isije kupotea, wahudumu walishuka kuifuta mapokezi na hawakuiona kadi hiyo ya NHIF, walijibu kuwa ilikuwapo labda hawa jamaa wa NHIF wameondoka nayo  tungoje kesho.

Kwa kuwa mama huyu alishalazwa na kadi yake ilishatambuliwa katika mfumo, hilo halikuwa neno, kesho yake akafanyiwa upasuaji vizuri , Mungu bahati akatoka salama , alipopata nafuu aiiulizia tena kadi yake lakini haikupatikana.

‘Mama siku hizi  NHIF wanashinda hapa,  wakiona kadi wanachukua,  kwa hiyo tunaifuatilia  lakini nenda  Kinondonii pale itakuwepo.’

Mama huyu aliporuhisiwa aifika Kinondoni  NHIF na siku hiyo alielezwa mhusika hayupo aende siku inayofuata, kweli siku  hiyo ya pili alifika  na kadi hiyo kutafutwa lakini haikupatikana.

‘Kadi yako haipo,tunakuomba nenda polisi , alafu ujaze  fomu , uje nayo na ulipe 20,000/  tutakupatia kadi nyingine,  wala usiwe na neno , hiyo ni kazi ndogo sana.’

Mama huyu akampigia simu Mwanakwetu akamwambia  hayo maelezo kama yalivyo.

 Mwanakwetu akamwambia,

‘Jamani kuna wakati mwingine, baadhi ya taasisi zinafanya utani na Jeshi la Polisi, Kadi imepotea mikononi  mwa taasisi,Inakuwaje tena wewe ubebe mzigo wa kutoa taarifa  polisi na kulipa shilingi 20,000/ kwa makosa ya mtu mwingine? Mimi sijasoma sheria lakini ninaona mwenye kupoteza ndiyo anayepaswa kuitoa taarifa polisi. Oongea nao vizuri wakueleze kadi yako anayo nani? Wanapobanwa siku nyingine watakuwa makini.’

Huyu mama alifanya hivyo na  aliporudi Mlongazila watumishi wa taasisi hii ya tiba wanajitambua mno , ndiyo maana Mwanakwetu katoa heko.

Madaktari bingwa na wauguzi walikuwa wakali mno juu ya tukio hilo, wahusika wa mapokezi wakisema jina la mgonjwa na nambari ya kadi yake ipo  na inaonekana ilipokelewa  vizuri , lakini aliyechukua  kadi hajulikani, wakihisi imekwenda Kibaha-NHIF, Huko walifunga safari na haikuonekana. Huyu mama mgonjwa nguvu  hana , akarudi kupumzika Tanga kwa majuma kadhaa, alafu akarudi Dar es Salaam na nyaraka kwenda kuomba kadi mpya ya NHIF maana alikuwa pia na miadi na daktari wake, alipokwenda NHIF kinondoni siku hiyo kulikuwa na watu wengi tangu saa tatu foleni ndefu, wengine wakisema shida ni mfumo na hadi saa 9. 20 ndiyo anafika mlangoni kwa mhusika. Akiwa hapo alitoa fomu yake iliyojazwa na mjadala ulikuwa huu,

Mama tunaomba cheti cha ndoa

Mama akatoa nakala ya cheti cha ndoa.

Mama tunaomba original

Mama akatoa cheti cha ndoa Original

Mhusika akakaa kimya kwa muda , huku akikagua fomu hiyo  ya maombi ya mrejesho ya kadi ya NHIF.

Mama mbona majina ya mumeo ya cheti cha ndoa, majina yamegeuka ? La kwanza limekuwa la mwisho na la mwisho ndiyo  limekuwa la kwanza?

Mama huyu akajibu akisema ndiyo maana nimeambatanisha na kiapo vinginevyo nisingeweka kiapo hicho.

Naomba kiapo Original

Mama akafungua pochi lake na kutoa kiapo Original cha Mahakama.

Msomaji wangu huyu muuliza maswali mtumishi wa NHIF hakumtambua mtu anayeongea naye na maswali ya kisheria aliyokuwa akimuuliza, hahaha Mwanakwetu.Watu wanaheshimu mamlaka wanayokutana nayo kwa asilimia 100, wewe ndugu yangu mtumishi wa NHIF ofisi ya Kinondoni kuwa makini na tenda haki.

 Kumbuka sana haya maneno kwa ajili yako-Yohane Paulo II(Mtakatifu) anasema,

‘ Ujinga nayo ni zawadi ya mwanadamu kutoka kwa Mungu lakini usitumie vibaya.’

 Kumbuka msomaji wangu mama huyu akatoa kiapo  cha mumewe.

 Mhudumu  wa NHIF akasema  mbona jina la mumeo la kazini mama na la NIDA halifanani ?

Mama huyu akisema ndugu si ndiyo maana nimekupa kiapo  cha mahakama cha jina hilo!

Naomba Salary Slip ya mumeo .

Mama akafungua pochi na kutoa Salary  Slip ya mumewe ya  Aprili 2023 na kuwapa NHIF..NHIF wanekuwa benki inayotoa mikopo?

Jamaa wa NHIF akasema mama subiri hapo nje kidogo.

Mama huyu akampigia Mwanakwetu na kumueleza juu maombi ya Salary Slip.

Jamaa akamuita mama huyu akamuomba salary slip ya hivi karibuni.

 Mama  akapiga simu kwa  mumewe  wakaanza kuhangaikia   Salary Slip ya karibuni,

Mumewe akamjibu kuwa nikiwa naingia kwenye huu mfumo wa Wizara ya Fedha inanigomea  hivyo huwa nazipata  kuomba kwa  wahasibu kazini,  kwa hiyo ngoja niombe lakini sasa hivi ni saa  9.30 watakuwa wametoka ofisini. Mama wa watu kwa  kuwa msomi akaomba  taarifa za mumewe akaingia katika mfumo huo  wa  Wizara ya Fedha hakupata salary slip maana password ilikosewa



Mama akarudi kumueleza mhusika juu ya hilo.

 'Jamani nisadieni nipate kadi nikatibiwe matibabu ni gharama , vitu vyote vipo  hvyo vingine vinatoka hapa hapa NHIF?’

Jamaa akagoma kabisa, mama huyu akampigia Mwanakwetu kuomba aongee nao hawa ndugu, kwa kuwa simu  tayari imepokelewa na mama huyu,  jamaa  akasema hapana sina muda huo nina kazi nyingi.

 Mwanakwetu akamuomba mama huyu awe mpole sana na Tanzania ni nchi yetu jambo hilo litakwisha tu

Mwanakwetu akaingia katika mtandao na kuitafuta namba ya simu ya  NHIF KINONDONI, alipouliza GOOGLE majibu yalitoa namba hiii  0756456895.




Namba hiyo ilipigwa dakika kama tatu, haikupokelewa lakini baadaye alipokea mama mmoja  na alipoulizwa hapo ni NHIF KINONDONI mama huyu alijibu hapana.

Kazi iliongezeka   Mwanakwetu alitembelea  tovuti ya NHIF Makao Makuu Dodoma nayo  ilionesha na namba hizi kama zinayooneka chini baada ya aya hizo mbili 

Namba hizo zilipigwa,, zipo zilizoita  lakini hazikupokelewa, zipo ambazo hazikuita kabisa. Mwanakwetu anawapa hongera sana NHIF makao makuu kwa kuwa ni simu zinazopigwa harafu hazipokelewi.

Namba ambayo ilitoa matumaini ni HOTLINE 199 yenyewe ilieleza habari za magonjwa lakini hadi mwisho haikupokelewa .HONGERENI SANA NHIF.




Mama huyu akiwa hapo  alipita ndugu mmoja  ambaye alisoma naye chuo kikuu na alisoma na Mwanakwetu akamuuliza shida yako nini huku akimtaja na jina lake alieleza kilichotokea, akamchukua na kupelekwa ofisi nyingine na kukutana na mtu muungwana na mama akaandika maelezo yake na kuacha fomu zote wakisema jumatatu watampigia simu. Mama wa watu katoka kachoka, yupo NHIF Kinondoni tangu asubuhi ya Ijumaa ya Septemba 29, 2023 na hiyo sasa ikiwa saa 10 , 05 ya jioni ya siku hiyo.




Mwanakwetu siku ya leo anasema nini?

Mosi Mfuko wa NHIF umeanzishwa kwa mujibu wa sheria nia ikiwa  nzuri sana, lakini sasa kuna mambo mengi hayaendi sawa . NHIF tangu viongozi wao na watumishi wote wafahamu kuwa wao hawana hospitali hata moja, wao siyo MSD hawana hata  kidonge cha PANADO, bali wao ni watu wa kati wanaokusanya fedha za wanachama na kuzipelekwa kwa taasisi zinazotoa huduma za tiba.

NHIF ni watu wa kati, kushoto kuna Hospitali/Vituo vya Afya& Zahanati, kati ni NHIF ma mwanzo ni Mteja na wengi ni watumishi.Hawa wateja likitokea la kutokea  wakawaeleza wabunge wao inaweza kuamuliwa vinginevyo na hiyo NHIF ikabaki simulizi kama zilivyokuwa kwa taasisi zingine za umma. NHIF wasipokuwa makini hilo linaweza kutokea maana kama iliweza kujengwa kwanini isibomoke?

Wateja wanaokwennda kupata huduma hapo hawaji kupata hisani bali wanakuja NHIF kudai haki yao maana wanailipia kila mwezi. NHIF watambue kuwa wao siyo TRA, wao siyo Benki Kuu wanatakiwa kufanya kazi kwa mujibu washeria iliyooundwa  na madhumuni ya awali yalisomwa mbele ya Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na kusainiwa na Rais  Benjamni Mkapa.

Mwanakwetu anasema kuwa kazi inayofanywa na NHIF inaweza kufanywa na hata na Hazina na kuzikusanya fedha na hesabu  zake na kupelekwa kwa watoe huduma iwe  Hospitali/ vituo vya Afya na hata zahanati.Mbona pesa ya lipa kulinga na unachopokea zinakusanya vizuri na zinafika sehemu husika?  

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF ajitahidi akae na wanafanyakazi wake awaeleza nia ya kuundwa kwa mfuko huu, mkurugenzi Mkuu wa NHIF atambue kuwa  Tanzania inaweza kusonga mbele  bila ya NHIF, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF atambue kuwa pesa zinazokusanywa zitumike kuwatibu wagonjwa wenye shida zaidi na siyo kuwawekea  masharti. Mkurugenzi wa NHIF na Bodi yake itambue kuwa masharti yoyote yanayowekwa kwa wanachama wa NHIF wanajiwekewe wao wenyewe na familia zao. Kama siyo Leo basi kesho, hapo  mbele ya safari labda wasiwe Watanzania.

Mfuko huo ni wa huduma na siyo mfuko wa faida.

Mkurugenzi wa NHIF awaambie watumishi wake waache kuzunguka mahospitalini, wao hayapigwa chanjo za mgonjwa mbalimbali, twendeni hosptalini tukiwa wagonjwa. NHIF itumie mifumo ya kukwepa udanganyifu na siyo kukusanya hovyo hovyo kadi za wagonjwa mahospitalini.NHIF simu zenu za mezani za mawasiliano zipatikane na zikiita zipokelewe, pia muweke simu zenu za mikononi.

Mwisho kabisa Mwanakwetu anaomba NHIF KINONDONI huyu mama aliyesimuliwa apewe kadi mara moja.

Mwanakwetu anaweka chini kalamu yake akisema udalali wa NHIF uwe na manufaa kwa wanachama , inachongwa kinaweza kubomolewa na maana sasa hatutaki tena kurudi kutibiwa kwa waganga wa kienyeji.

 Mwanakwetu upo?

Nakutakia siku Njema.

 makwadeladius @gmail.com

0717649257 


0/Post a Comment/Comments