USIKUBALI KUKATISHWA TAMAA


 Adeladius Makwega-MWANZA

Mwaka 2013 juma la mwisho kabla ya Sikukuu ya Noeli, shajara ya Mwanakwetu inaelezea tukio moja ambalo ndilo linabeba makala haya siku ya leo.

Mwanakwetu alitoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam, Mahakama ya Kazi kuelekea Sinza Kumekucha ambapo alikwenda kuonana na ndugu Zabroni Bugingo ambaye wakati huo alikuwa ni Mtayarishaji Vipindi Mwandamizi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) pale Mikocheni TBC ambapo wakati huo Bugingo alipangiwa kitengo cha Mitandao ya Kijamii.Mwanakwetu alikubaliana na ndugu Bugingo kwa simu wakutane eneo linaloitwa Vatikani jirani na Sinza Kijiweni. Mwanakwetu alifika eneo hilo mapema sana na kukaa kumgonja ndugu Bugingo.

Msomaji wangu ni vizuri ukamfahamu zaidi ndugu Bugingo ambaye baadaye alifanya kazi TASAF Tanzania pia akafanya kazi na Halmashauri ya Kibiti kama Mkurugenzi Mtendaji huko mkoani Pwani na sasa yaani 2024 ni Afisa habari Mkuu ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Kumbuka msomaji wangu kuwa Mwanakwetu yu Sinza hapo alitumia muda mrefu sana kumngoja rafiki yake huyu, hivyo alisimama muda mrefu hapo Vatikani, ndugu Bugingo hatokei. Alipowasiliana naye alibaini kuwa ndugu Bugingo alikuwa na kazi ya dharula aliyopewa na mwajiri wake hivyo kuiacha kazi hiyo ilikuwa vigumu sana na hakuwa na budi kuifanya.

Mwanakwetu alichoka kusimama ilibidi sasa atafute eneo ambalo linauzwa chakula ambapo baa moja kando ilikuwepo, alivuka barabara hiyo na kwenda, alipofika, aliketi kwa amani akaagiza chakula akala na kunywa soda huku akimsubiri nduguye Bugingo.

Msomaji wangu kwa hakika kila mmoja wetu hapa duniani anaye mtu anayemuheshimu sana, kwa hiyo Mwanakwetu anamuheshimu sana kaka yake Bugingo wa Zabroni.

Kufahamiana baina ya Mwanakwetu na Bugingo kunatokana na sababu hii, wakati Mwanakwetu anaajiriwa na TBC mwaka 2009, siku ya mahojiano alifika pale TBC makao makuu, siku hii ilikuwa ni mfugo wa Ramadhani, ikakubaliwa Waisilamu wafanye mahojiani kwanza alafu Wakristo wafanye baadaye ili waliofunga wawahi kufuturu.

Msimamizi wa mahojinao hayo alikuwa Dastani Mhando, akamuagiza Taji Liundi aseme hilo, kweli akina Mwanakwetu walipoulizwa hawakupinga, walikubaliana nalo kwa sauti moja.

Anayekwambia Tanzania kuna udini, mtazame mara mbili mbili-yeye huyo huyo ndiye mdini.”

Kumbuka msomaji wangu Mwanakwetu na Watanzania wenzake kama 200 wapo katika mahojiano ya kutafuta kazi ya utangazaji hapo TBC, hiyo ni mwaka 2009. Taji Lindi akasema,

“Mkurugenzi Mkuu, Tido Mhando amesema siku ya leo futari kwa waliofunga na chakula cha mchana kwenu nyote kipo.”

Watu walishangilia sana sana, hasa hasa ndugu Chunga Ruza ambaye kwa mwaka wa 2024 ni mtangazaji aliyepaa tatizo lakukosea juu ya ile meli, huyu ni mtangazaji mahiri sana aliyetokea Tanga wakati huo na siku hiyo alikuwa amefunga Ramadhani, Mwanakwetu anamtambua vizuri sana Chunga Ruza na hata siku hii aliyokosea juu ya meli alikuwa amefunga Ramadhani, watu wengi hilo hawalifahamu, hilo nakuuma sikio msomaji wangu.


 

Mwanakwetu akiwa hapo wakati Waisilamu wanafanya usaili akachukua karatasi ya walioitwa kwa usaili na kupitia akabaini jina la Zabroni Bugingo ambalo alikuwa analiskia Redio Free Africa, akauliza jamani Bugingo ni nani? Alipouliza hakupatikana. Dada mmoja akasema huyu nimesoma naye Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Mwanza mwaka 2005-2008 lakini sina namba yake.

Mwanakwetu aliposikia juu chuo cha SAUT Mwanza alikuwa na namba ya Christopher Ndyana ambaye wakati huo Mwanakwetu na Ndyana wanasoma pamoja shahadaya Uzamili ya Uongozi wa Biashara MBA Tumaini iringa , akampigia simu akimuuliza kaka unafahamu Bungingo? Ndyana akajibu ndiyo.

“Si unajua nipo Dar,Tunafanya usaili hapa RTD TAZARA jina lake lipo.”

Ndugu huyu alimpigia simu na kubaini yu Mwanza, Bugingo akapewa taarifa na Christpher Ndyana ambaye sasa ndiye Msemaji wa Wizara ya Uchukuzi ya Tanzania na hapo hapo namba ya simu ya Bugingo akapewa Mwanakwetu, hiyo ni saa tatu ya asubuhi, Bugingo akaongea na Mwanakwetu akasema

“Kaka nakuja napanda ndege sasa hivi mchana nitakuwepo TAZARA.”

Bugingo alifika Dar es Salaamna na kufanya usaili yeye na Mwanakwetu muda mmoja kumbuka mahojiano walianza Waisilamu akiwamo Chunga Ruza na Jamali Hashimu mwishoni Bugingo , Mwanakwetu Chunga Ruza, jamali Hashimu baadaye akina Neema Mbuja, Charles Mwebeya, Musa Twangilo, Gervas Hubile na wengine wengi walipata kazi hiyo hapo TBC.

Msomaji wangu kumbuka sana ,

Wema unajenga udugu nao ubaya unajenga uadui.”

Haya yanayoyaeleza leo hii ni namna tu Mwanakwetu alivyomfahamu Zabroni Bugingi, kumbuka Mwanakwetu yu Sinza anamgonja Bugingo ambaye ni rafiki na ndugu yake.

Kwa-pembeni ya baa hiyo kulikuwa na kituo cha daladala ambacho kilimshangaza mno Mwanakwetu maana watu wengi waliovalia nadhifu walishuka na kuingia ndani kwenye mtaa huo mkono wa kushoto.


 

Mwanakwetu alipoouliza pale kuna shughuli gani ? Alijibiwa na dada mhudumu kuwa hapo kando kuna ukumbi ambapo kuna mhubiri anafanya maombi, anazunguka mikoa mingi Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam anaitwa Mchungaji Mwamposa. Kweli baada ya dakika kama ktatu hivi ulisikika wimbo ulioanzisha na mtummoja na wengine wanaitikia.

“Damu ya Yesu Inanema mema, Inanena mema

Damu ya Ukombozi, Inanena mema

Inanena mema., Ohh inanena mema

Inanena mema , Inanema mema.”

Bwana Asifiweeeee… na umati ukajibu Ameniiiii...

Sauti hiyo ikasikika ikasika tena ikisema kila mmoja afungue  Biblia yake Injili ya Luka Sura ya 24 mstari wa ule 8 hadi 34 (Huku haya maneno yakirudia rudia)

 

Hapo Mwanakwetu katulia, anasikiliza kwa umakini mkubwa kupitia zile spika za mchungaji huyo, ambapo zilimuhamisha Mwanakwetu kutoka katika ukumbi uliojaa walevii na kelele  tele za nymbo za kidunia na kumpeleka kimawazo katika mkutano

Bwana Yesu asifiweeeeeee…. Aminiiiiiii...

“’Hapo wanawake wakayakumbuka maneno yake,wakarudi kutoka kaburini, wakawapa mitume wale kumi na mmoja na wengine habari za mambo hayo yote.Hao waliotoa habari hizo kwa mitume ni: Maria Magdalene, Maria mama wa Yakobo, pamoja na wanawake wengine walioandamana nao.Mitume waliyachukua maneno hayo kama yasiyo na msingi, hivyo hawakuamini. Lakini Petro alitoka, akaenda mbio hadi kaburini.

Alipoinama kuchungulia ndani, akaiona tu ile sanda. Akarudi nyumbani huku akiwa anashangaa juu ya hayo yaliyotokea. 

Siku hiyo hiyo, wawili kati ya wafuasi wake Yesu wakawa wanakwenda katika kijiji kimoja kiitwacho Emau, umbali wa kilomita kumi na moja kutoka Yerusalemu.Wakawa wanazungumza juu ya hayo yote yaliyotukia. Walipokuwa wakizungumza na kujadiliana, Yesu mwenyewe akatokea, akatembea pamoja nao.Walimwona kwa macho, lakini hawakumtambua.Akawauliza, ‘Mnazungumza nini huku mnatembea?’ Nao wakasimama kimya, nyuso zao wamezikunja kwa huzuni. Mmoja, aitwaye Kleopa, akamjibu, ‘Je, wewe ni mgeni peke yako Yerusalemu ambaye hujui yaliyotukia huko siku hizi?’  Naye akawajibu, ‘Mambo gani?’ Wao wakamjibu, ‘Mambo yaliyompata Yesu wa Nazareti. Yeye alikuwa nabii mwenye uwezo wa kutenda na kufundisha mbele ya Mungu na mbele ya watu wote.

Makuhani na watawala wetu walimtoa ahukumiwe kufa, wakamsulubisha. Lakini sisi tulitumaini kwamba yeye ndiye angeikomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu mambo hayo yalipotendeka. Tena, wanawake wengine wa kwetu wametushtua. Walikwenda kaburini mapema asubuhi, wasiukute mwili wake. Wakarudi wakasema kwamba walitokewa na malaika waliowaambia kwamba alikuwa hai.Wengine wetu walikwenda kaburini wakashuhudia yale waliyosema hao wanawake; ila yeye hawakumwona.’ Kisha Yesu akawaambia, ‘Mbona mu wapumbavu kiasi hicho na mioyo yenu ni mizito hivyo kusadiki yote yaliyonenwa na manabii? Je, haikumpasa Kristo kuteswa, na hivyo aingie katika utukufu wake?’

 Akawafafanulia mambo yote yaliyomhusu yeye katika Maandiko Matakatifu kuanzia Mose hadi manabii wote.Walipokikaribia kile kijiji walikokuwa wanakwenda, Yesu akafanya kana kwamba anaendelea na safari; lakini wao wakamsihi wakisema,’Kaa pamoja nasi, maana kunakuchwa, na usiku unakaribia.’ Basi, akaingia kijijini, akakaa pamoja nao. Alipoketi kula chakula pamoja nao, akachukua mkate, akaubariki, akaumega, akawapa. Mara macho yao yakafumbuliwa, wakamtambua; lakini yeye akatoweka kati yao. Basi, wakaambiana, ‘Je, mioyo yetu haikuwa inawaka ndani yetu wakati alipokuwa anatufafanulia Maandiko Matakatifu kule njiani?’

Wakaondoka saa ileile, wakarudi Yerusalemu: wakawakuta wale mitume kumi na mmoja na wale wengine waliokuwa pamoja nao, wamekusanyika wakisema, ‘Hakika Bwana amefufuka, amemtokea Simoni.”

Kumbuka msomaji wangu mchungaji Mwamposa anasoma hayo, naye Mwanakwetu anasikiliza huku akinukuu katika shajara yake vizuri ya Disemba 2013.Baada ya Injili hiyo ya luka Sura ya 24 mstari wa ule 8 hadi 34 kusomwa mchungjai akauliza 


 

Je unakubali kurudi kijijini?

Waamini wakajibu hapana, tunabaki Yerusalem

Mchungaji akasema,

“Katika maisha usikubali kurudi kijijini, nina maana hao mitume wa Yesu walikata tamaa baada ya kuuwawa mwalimu wao, kila mmoja alikuwa anarudi alikotoka na anarudi kufanya kazi yake ya awali, je kama asingalifufuka na kuwatokea je Injili hii tungeihubiri leo hii hapa sinza? Waamini wakasema hapana. Mchungaji akaendelea kusema  amefufuka kama alivyosema na amewatokea mitume wake na akapaaa Mbinguni.’

“Haya sasa Sema nabaki-Nabaki Mjini

Sema Nabaki -Nabaki Mjini

Sema Nabaki Yerusaleem,Nabaki Yerusaleem.”

Mchungaji anasema waamini wanaitikia.

“Nabaki Yerusaleem, Nabaki Yerusaleem”

Wakati maneno haya yanaendelea mara Zabroni Bugingo alishuka katika gari yake na kumsalimu Mwanakwetu na kunmpa pole ya kumgonja kwa muda mrefu hapo Vatikani Sinza Dar es salaam Disemba 2013 walifanya mazungumzo haya kwa dakika chache naye Mwanakwetu kurudi zake Mbagala.


 

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Kwanza kwa hakika Mwanakwetu siku hiyo hakuipoteza bure bali alijifunza hayo aliyoyasimulia kutoka katika mahubiri ya huyu mchungaji rejea injili ya Luka sura ya 24mstari 8-34

Pili taasisi zote za dini zikumbuke kuwa mahubri wanayoyafanya sio kwa ajili ya waliyo kanisa tu baliihata walio mbali nao wanahitaji kufahamu yaliyomo katika Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo, huko Injili inaweza kuwafikia kwa kutumia tekinolojia ya sasa kama vile magazeti, redio , simu, runinga na mitandoa ya jamii kwa kadili ya uwezo wa makanisa yao.

Spika zile zilimsaidia Mwanakwetu aliyekuwa baa akimgonja rafiki yake kuandika makala haya yenye sehemu ya Injili ya Luka miaka 11 baadaye, huo ndiyo umuhimu wa tekinoljia

Mwisho Mwanakwetu anakuomba msomaji wake ukumbuke kuwa usikubali kurudishwa nyuma na mtu yoyote yule katika maisha yako na usikubali kukata tamaa, kikubwa kusimama pahala sahihi.

Mwanakwetu Upo?

“Usikubali Kurudi Kijijini.”

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257



 

 


0/Post a Comment/Comments