Adeladius Makwega-MWANZA
Wakristo wameambiwa kuwa japokuwa mwezi wa Mama Bikira Maria OKTOBA
umemalizika bado wanatakiwa kuendelea
kusali Rozali maana hiyo ni sala muhimu kwao nyakati zote za maisha yao hapa
duniani.
Hayo yamesemwa na Padri Samson Masanja, Paroko wa Parokia ya
Malya Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Oktoba 31, 2023 katika azimisho la Ekaristi
Takatifu, misa maalumu ya kuhitimisha safari ya mwezi mzima wa Mama Bikira Maria
iliyofanyika katika kanisa la Bikira Maria Malkia wa Wamisionari hapa Malya
“Sasa siyo wakati wa kuiweka Rozali shingoni, kuiweka Rozali mifukoni tu
na kama tutafanya hivyoi hapo itakuwa ni kitu cha hivi hivi tu . Rozali ni kitu
thamani kubwa kwetu na sasa tunatakiwa kusali zaidi. Wote tunatakiwa kuisali
Rozali maana katikia kusali huko tunaombea amani katika ulimwengu na pia tunaombea
kuondoa machafuko katika ulimwengu huu, tunaombea watu waache dhambi na sote tumcheMungu.”
Padri Masanja aliongeza kuwa Rozali imetoa matokeo chanya mengi mno, wapo walipokea uponyaji kutoka na shida mbalimbali. Tunaosali Rozali tunaonja upendo wa Mungu na hapo pia tunapokea neema za Mwenyezi Mungu.
Akiendelea kuhubiri katika azimisho
la misa takatifu iliyohudhuriwa na waamini karibu 100, watawa watatu na makatekista wawili Padri Masanja alisema,
“Bikira Maria amemzaa Yesu Kristo, kwake Ulimwengu umepokea
uponyaji.Huyu ni mama wa thamani kubwa kwetu”
Wakati wa maombi ya misa hiyo Padri Masanja
aliruhusu waamini kila mmoja kuombea nia yake binafsi.
Hadi misa hiyi iliyoanza saa 10 ya jioni ya Oktoba 31, 2023 inamalizika majira ya saa 11 ya jioni , hali ya hewa ya Malya na viunga vyake ni ya jua na mvua , huko mashambani kilimo na ufugaji vinandelea vizuri
Post a Comment