Mwaka 1972 ndugu S Kazi ambaye anajitambulisha kama alikuwa
mwalimu na mzaliwa wa Usukumani alizunguka maeneo kadhaa ya Usukumani kama vile
Maswa, Shinyanga na Mwanza kufanya tafiti nying juu ya kabila lake hilo.
Ndugu S Kazi anaeleza wazi wazi kuwa katika safari hizo hali
ya usafiri ilikuwa ngumu sana ambapo maeneo mengi alisafiri kwa kutumia punda,
baiskeli na mara chache kupanda malori na mabasi kutoka eneo moja kwenda lingine.
Msomaji wa Mwanakwetu nakuomba utambue kuwa ndugu Kazi amefanya
tafiti nzuri zenye simulizi nyingi za Wasukuma ambazo mara nyingi ndugu yetu
Mwanakwetu anazinukuu kama zilivyo.
Ndugu Kazi katika ukurasa wake 187 katika kitabu kimoja kikubwa
kilichokusanya tafti kadhaa za makabila ya Tanzania kikiwa na jina Utani Relationships in Tanzania Volume Five Edited by Stephen A Lucas kilichotoka mwaka
1975.
Humo ndugu kazi anazungumzia visa vingi baina ya makabila
ya Pwani na Wasukuma.
“Wasukuma na Wanyamwezi walifika Pwani kwa sababu ya Biashara
ya Utumwa iliyofanywa na Waarabu na wakifanya biashara zingine.”
Katika zoezi hilo wapo waliochukuliwa utumwa wakatokomea
utumwani na wapo waliokimbia njiani na kurudi Usukumani, wapo waliokufa njiani
na wapo waliobaki maeneo hayo hayo ya Pwani.
“Wasukuma waliweza kwenda sana Pwani na makabila ya Pwani
yaliyoweza kufika bara lakini kwa uchache mno, kwa hiyo Wasukuma waliwafahamu
mno watu wa Pwani kuliko watu wa Pwani walivyowafahamu Wasukuma na Wanyamwezi,
ndiyo maana hadi kesho makabila ya Pwani yanashindwa kuwatafautisha Wasukuma na
Wanyawezi.”
Makabila ya Pwani hadi
kesho yanaendelea kutowafahamu makabila haya mawili huku nao Wasukuma na
Wanyamwezi wanashindwa kwa kiasi kuwatafautisha Waluguru, Wapogoro Wazaramo ,
Wakwere, Wadoezi na makabila mengine ya Pwani labda wale Wasukuma na Wanyawezi
walioishi huku kwa muda mrefu..
Wasukuma waliokwenda
Pwani wengine walioa/kuolewa huko na kuzaa na makabila haya huko huko na
kufahamu tamaduni nyingi za watu wa Pwani, lakini Watu Wapwani walibaki kuwa
maamuma wa Wasukuma na Wanyamwezi waliobaki huku bara.
Ndugu S Kazi anadai kuwa,
“Watu wa Pwani walipata kazi nyingi baada
ya ujenzi wa Reli ya Kati hivyo wengi walipa ajira katika vituo vya Gari Moshi
na wengine kuhamia kuhamia moja kwa moja katika maeneo haya ya bara yenye Wasukuma
na Wanyamwezi wengi.”
Jambo hilo kidogo lilisaidia sasa Wazaramo
, Wakwere na watu wa Pwani kuingia katika kuwafahamu Wanyamwezi na Wasukuma moja
kwa moja.
Walipofika Mwanza walikaribishwa
majumbani mwa Wasukuma na hapo walikuta wanyama wanaishi pamoja na binadamu ,
katika makundi makubwa makubwa.
“Nyie jamaa vipi! Mbona mnaishi na Nyati, hawana madhara ? Je
hawawezi kuwachoma na pembe zao ?”
Wasukuma hata walipowakaribisha Wazaramo
hapa majumbani mwao walikuwa waoga na ng’ombe walipokuwa jirani hapo hapo walikimbilia
ndani ya nyumba za Wasukuma na kujificha, huku wakigoma kutoka nje.
S. Kazi anasema,
“Uwoga huo wa Wazaramo kwa mifugo ya bara ulisababisha hata wakati
mwingine Gari Moshi liliwapita na kuwaacha na hivyo kugonga Gari Moshi lingine na
wakati mwingine walipoteza kazi kisa uwoga wa nyati( ng’ombe)”
Mwanakweu siku ya leo anasema nini?
Ndugu zake Mwanakwetu mara zote wanaogopa
nyati anayeishi nyumbani kama anavyosimulia
ndugu S Kazi hivyo ili wawe salama na wasichelewe kupanda Gari Moshi ni
lazima wawe na Msukuma kando maana anakulinda na nyati hao, hofu ni zile pembe za
nyati hao wanaofugwa majumbani.
Mwanakwetu ndugu zake hawako tayari
kupanda Gari Moshi lingine na hawataki kulipa nauli mara mbili, wanataki kuwahi
Gari Moshi kwa wakati ule na tiketi ile ile.
Mwanakwetu Upo?
Msukuma Hodari Kukaa na Nyati.
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
Post a Comment