Adeladius Makwega-MWANZA
Safari njiani kutoka Bumbuli Lushoto mkoani Tanga kuelekea Dodoma kushiriki kikao cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi, baada kwa zile kata na majimbo ambayo yalikuwa yanakaribia kufanya uchaguzi wa kuziba mapengo kilichoitishwa kutokana na vifo na wengine kuunga mkono juhudi na kuhamia chama tawala kutoka vyama vya upinzani.
Bumbuli ilikuwa nimiongoni mwa Halmashauri iliyokuwa na uchaguzi huo, kufuatia kifo cha Diwani wake wa viti maalumu Mama Titu ambaye pia alikuwa ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Lushoto ambayo ilikuwa na majimbo matatu Mlao, Lushoto na Bumbuli.
Katika uchaguzi huo jimbo la Mlalo kata yake ya Lunguza kulitokea kifo cha diwani wake, hivyo nayenyewe ilikuwa katika mchakato huo. Hivyo jimbo la Bumbuli , Jimbo la Mlalo na majimbo mengine yenye kata kadhaa Tanzania Bara safari ya kuelekea Dodoma iliwahusu.
Waliotoka Bumbuli walifika Dodoma kikaoni, hawakuwa wengi sana, maana ni kata moja tu, waliokuwa wanatarajiwa kuwa wengi ni wale waliokuwa wakifanya uchaguzi wa mbunge, jimbo zima. Japokuwa chaguzi hizo maeneo mengi hazikufanyika maana kulikuwa na hoja ya kupita bila kupigwa.
Kikao hicho kinafanyaki ukumbi wa Kambarage HAZINA Jijini Dodoma. Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa sasa ambaye alikuwa hajaondolewa nafasi hiyo wakati huo. Viongozi wengine kadhaa wakiwamo wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi akiwamo Jaji Mstaafu ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Tume hii wakati huo, walikuwapo.
Ukumbi huu ulikuwa mkubwa, viyoyozi kila kona, kuta za ukumbi huu za mbao ziking’ara mno, viti vimepangwa ngazi kwa ngazi katika mtindo wa duara. Nazo mikrofoni kila kona, ukiponyeza tu unaongea na kusikika ukumbi mzima kama upo Bungeni-Dodoma.
Mafunzo yalifanyika vizuri hasa namna hati na fomu kadhaa za uchaguzi zinavyojazwa, hatua kwa hatua na kila mmoja kupewa kibegi chenye nyaraka za mfano za fomu hizo za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Siku mojawapo ya mafunzo hayo ambayo ndiyo Jaji Mstaafu ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Tume hii aliongea kukawa na kipindi cha maswali na baada ya maswali hayo, mada kutolewa. Mwendo ukiwa mada na maswali. Mada mojawapo iliyokuwa na utata ni juu ya Msimamizi wa Uchaguzi Kula Kiapo cha Kuukana Uanachama wa Chama chake cha Siasa, ili aweze kutenda haki katika uchaguzi wakati wa kusimamia.
“Inawezeja mtu akaukana uanachama
wake? wakati ana kadi na anaamini moyoni juu ya hicho chama? Je imani inaweza
kuondolea kwa kutamkwa maneno mbele tu ya mtu?”
Watu wakijiuliza.
Mtoa mada alieleza kuwa kiapo hicho kitafanyika hapo hapo baada ya mada zitakapokamilika na sasa kukaribisha maswali .
Maswali mengi yaliulizwa lakini swali nzuri, swali makini na swali kukumbwa la kikao hicho litabaki la mjumbe kutoka Bumbuli, ambaye alifahamika kama Peter Nyalali. Ndugu mmoja mpole ambaye aliongea kama hataki lakini maelezo yake yalinyooka na hayakuyumba.
“Kweli mnadhani hilo
linawezekana? Mimi binafsi ni mwanachama wa CCM siwezi kuukana uanachama wangu
hata kwa saa moja. Mathalani mimi ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Ninapokula kiapo hicho ninapoteza hiyo nafasi. Mjanja akijua nimekula kiapo
anaweza kunipinga mahakamani. Asanteni.”
Baada maneno hayo watu wanashangaa na hivyo ndiyo ilivyokuwa, ndugu huyu akatoka kuelekea Uwanja wa Ndege wa Dodoma na kupanda ndege kuelekea Dar es Salaam.
Nafasi yake ikajazwa na mtu mwingine kutoka Bumbuli, Mtu huyu mwingine kutoka Bumbuli ambaye aliziba nafasi ya Peter Nyalali alikuwa ni Afisa Mipango wa Bumbuli wakati huo sasa Oktoba 2023 ndiye Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmsahauri ya Bumbuli.
Mwanakwetu anatambua kuwa wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wanabadilika, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa hivyo na hata Mwenyekiti wa Tume Hii pia.
Kwa sasa Mungu Bahati aliyeshuhudia tukio hilo, aliyelisimamiia kwa karibu hadi Peter Nyalali anatoka nje ya ukumbi wa Kambarage Dodoma ndiye Mkurugenzi wa Tume Taifa ya Uchaguzi kwa sasa.
Ikukumbukwe kuwa Peter Nyalali hadi kesho bado ni Mwana CCM, tena mtiifu.
Mwanakweu Upo?
“Ili uwe mwanaccm utaratibu ulikuwa
kwanza unaonesha nia ya kuwa mwanachama, pili unawajulisha viongozi wako wawe wa
shina , tawi au ngazi yoyote ile. Hapo unaandaliwa mafunzo ya miezi kadhaa na
siku ya siku anakuja kiongozi aliyepangwa kuwahitimishia mafunzo hayo .
Hapo wote kwa pamoja mkiongozwa
na katibu wenu wa Itikadi na Uenezi wa tawi au wa kata na hata Wilaya
anawaongoza mnazisoma ahadi za Mwana CCM Kwa sauti ,mkono wa kushoto kifuani na
mkono wa kulia juu,-mnakula kiapo. Mkishakula kiapo hicho mnapewa kadi, hadi
hapo hapo mmeshakuwa wanachamawa chama hiki.”
Ndugu Nyalali aliulinda uanachama wake wa CCM, ambapo tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikuwa inaupoka kwa muda wa uchaguzi. Alifanya hivyo mbele ya Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa Tanzania na mbele Jaji ambaye alikuwa pia Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania..
Kwa hakika inawezekana leo CCM haina hiyo kumbukumbu, hakuna anayeweza kukumbuka kabisa hilo na pengine hata hapa leo Mwanakwetu anapokumbusha Peter Nyalali anaweza kuonekana ni kituko. CCM inatakiwa kwanza kuwakumbuka wanachma wake pale wanapoonesha kulinda itikadi yao, kulinda kile wanachoamini. CCM isione ina wanachama wengi hao pia walikuja mmoja mmoja.
Mwanakwetu anawaambia CCM wakumbuke kuwa Peter Nyalali siyo kituko, ni mtu makini ambaye aliheshimu tu kile alichokiamini na watu wa namna hiyo ni adimu mno. Mtu hawezi kukupokonya kile unachokiamini hata kwa sekunde moja, hiyo ni haki yako
Ndani ya hilo kukiwa maswali kadhaa mathalani lile la Wabunge 19 wa CHADEMA, kukiwa na Spika mwanye PHD ya sheria kwa sasa, wakati Sofia Simba amepata shida jambo lake lilikimbizwa haraka haraka akapoteza ubunge . Hawa 19 bado wapo tu, wamepita wapi? Mbona bado wapo salama?Je akitokea Sofia Simba mwingine apite wapi awe salama kama hawa? Au ndiyo wana CCM hawana thamani kwa viongozi wao wakigombana nao?Thamani ya Bi Sophia Simba aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa UWT ni ndogo kwa thamani ya Bi Halima Mdee wa CHADEMA ndani ya CCM? Tuwaheshimu wanachama wetu hata kama tunapishana kimawazo katika baadhi ya mambo.Tuheshimu zile kazi walizofanya nasi awali.
Walio wengi wapo ladhi kulinda nafasi yake na maslahi yake tu ili mkono uende kinywani. Msomaji wangu tambua kuwa hata mwovu anaweza kukupa cheo, pesa na hata dhahabu kwa maslahi yake. Kikubwa ni kuheshimu kile unachokiamini . Kwa hakika Peter Nyalali mwisho wa siku alipoteza hivyo vyote, kwa heshima ya imani yake.
(Ndugu Peter Nyalali.)Msomaji wangu nikuulize wewe hapo ulipo unaweza kukilinda kile unachokiamini.? Wapo ambao wanaitika wanaitika ndiyo kwa kila kilichopo mbele yao, kwa sababu ya maslahi binafsi. Kumbuka kama hoja ni maslahi binafsi anaweza kutokea mtu akapanda dau kubwa na ukanunulika na hata kuleta madhara kwa wenzako, hoja si pesa si dhahabu wala siyo cheo.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikumbuke kuwa tukio hilo halifahamiki na wengi, Mwanakwetu analipandisha jalife lakejuu kuwakumbusha tume hii kuwa kama kuna marekebisho yawe sheria ya Uchaguzi au Kanuni , hoja za Peter Nyalali zikumbukwe sana sana.
Mwanakwetu Upo ?
Kumbuka Kukilinda Kile unachokiamini.
Nakutakia siku njema.
Post a Comment