SAMBAZA UPENDO KWA WENGINE-PADRI MASANJA

 



Adeladius Makwega-MWANZA

Wakristo wameambiwa kuwa Jumapili ya Oktoba 29, 2023. Kristo anafundisha kuwa kila Mwanadamu anapaswa kumpenda kwanza Mungu alafu kumpenda jirani yake kama anavyojipenda yeye mwenyewe na funzo hilo linafupishwa na mafundisho ya Kristo kutoka amri na sheria 613 na kuwa na Amri Kuu Mbili ambapo hizo ndiyo ukamilifu wote wa Torati na Manabii.

Hayo yamesemwa na Katika Kanisa la Bikira Maria -Malkia wa Wamisionari na Padri Samson Masanja Paroko wa Parokia ya Malya-Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza katika misa ya kwanza ya dominika ya 30 ya Mwaka A wa Liturjia ya Kanisa.

“Kristo anapofundisha jambo hilo katika dominika ya leo huo ni muendelezo kutoka kitabu cha Kutoka 22:21-27 ambapo ni sheria nyingi walizoelekezwa wana wa Israel namna ya kumpenda Mungu na kupendana wao kwa wao.”

Wana wa Israel waliambiwa wasimuonee mtu yoyote, awe ni mjane , awe  ni mgeni na hata  awe ni yatima bali wawatendeane kwa haki na mapendo.


Padri Masanja aliendelea kuhubiri akisema kuwa hiyo ndiyo maana halisi ambayo Kristo anayosisitiza katika somo laInjili ya dominika hii Mt 12:34-46.

“Kumpenda jirani haina maana ya kusema kwa maneno tu , mimi ninampenda mimi ni nampenda kwa namna hii hii na ile, kusema unampenda ili hali unamuumiza hiyo haina maana kabisa.”

Padri Masanja alisisitiza kuwa masomo ya dominika hii yanatupa tafakari tujiulize je tinaishi vipi na wenzetu,? Je wewe unatenda haki kwa jamii yako na Je jamii yako inafahamu kuwa unatenda haki?


Padri huyu alipigia msumari wa mahubiri hayo kwa kusema kuwa jinsi wewe unavyopenda na jinsi wewe unavyofurahi chukua hiyo furaha na huo upendo usambaze, uubebe na uwapelekee wengine.

“Kumpenda Mungu lazima lazima ihusishwe roho , moyo na akili .”

Misa hiyo ilifanyika kwa utulivu kubwa na ilikuwa na nia na maoni kadhaa

“Ee Baba MUngu, Upendo wa Kikristo una sura nyingi sana, utupe moyo wa kuutimiza upendo huu wa Kristo.”

Hadi misa hiyo inamalizika majira ya saa moja ya asuhubi, hali ya hewa ya Malya na viunga vyake ni jua na mvua na shughuli za kilimo zikiendelea.





0/Post a Comment/Comments