Adeladius Makwega MWANZA
Mwanakwetu jioni ya Novemba 9, 2023 ametembelea ukurasa wa Instagram wa Mbunge wa Malinyi mhe. Antipas Zeno Mngungusi na kumkakagua mheshimiwa huyu. Safari ya ukaguzi wa kurasa wa kiongozi huyu wa watu katika Jimbo hilo lililopo katika mkoa wa Morogoro ilikuwa ndefu mno.
Huku akikutana na kazi kadhaa za mheshimiwa huyu alizofanya kwa wananchi hao wa Malinyi.
“Wananchi wa kijiji SOFI MAJIJI akiomba kwa
Mbunge, mabasi ya abiria toka Dar na Moro, yaingie ndani Senta ya kijiji,
kinyume na sasa, yanapita nje, ambapo abiria hulazimika kukodi pikipiki .”
Mwanakwetu aliona
majibu ya Mbunge Mngungusi,
“Jambo hili nimelipokea NINAWAAHIDI LITAFANYIKA
KAZI MARA MOJA kama mlivyoomba. Nawasiliana na Viongozi wenzangu wa Serikali.”
Mwanakwetu akawa
anaendelea kupitia ukurasa huo wa kiongozi huyu na kukutana na picha moja ya mheshimiwa
huyu akikagua barabara inayojengwa, huku mafundi hao wakiwa kazini.
Mwanakwetu
aliendelea kuukagua ukurasa huo alafu akakutana na picha moja ya Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa akitetea jambo na mhe.
Mnungusi .
Kwa hakika hapo Mwanakwetu akasema,
“Yapo mambo mengi yenye mfanano baina Lindi na
Morogoro, hasa hasa upande wa Ulanga na Malinyi.”
Mwanakwetu akasema
moyoni kwa kuwa Waziri Mkuu ni mzaliwa wa Lindi anayefahamu mengi juu ya Lindi
na Morogoro, hapo hoja zitapata majibu tu.
Mwanakwetu anaendelea
kuukagua ukurasa wa Instagram wa mhe Antipas Mngungusi, mbele kidogo akakutana
na picha moja ya mheshimiwa huyu akishiriki mashindano ya mbio huko Zanzibar .
Hapo hapo Mwanakweu
akakumbuka kuwa mheshimiwa huyu ni mpenda michezo wa miaka mingi, siyo leo tangu
miaka mingi nyuma.
Mwanakwetu
akasema kumbe mheshimiwa huyu bado ni mwanamichezo.
Mwanakwetu
akaendelea kuupakua ukurasa huu wa Instagram wa mheshimiwa huyu na hapo hapo
akakutana na maneno haya.
“Hongera sana Mwanafunzi wangu wa Kamba Mhe.
Bahati Ndingo...”
Mwanakwetu akawa
anajiuliza, huyu Bahati Ndingo ni nani? Hivyo alianza kumsaka kwa kina na hapo
hapo Instagram.
“Leo nimeapa kuwa mtumishi wa wananchi wa Mbarali,
ee Mwenyezi Mungu nisaidie.”
Mwanakwetu
akafahamu kuwa mheshimiwa huyu kumbe ndiye mbunge mpya wa Mbarali katika
uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.
Mwanakwetu
akasema moyoni kama mhe. Bahati Ndingo anafundishwa kuruka kamba na mbunge wa
kwetu Malinyi Morogoro mhe Antipas Mngungusi basi tunamuomba amualike mhe. Bahati
Ndingo aende kutembelea mkoa huo, hasa hasa Ulanga kule Mbangayao aone namna Vyura
walivyohama na Wapogolo baada ya kuhamishwa alafu mhe. Bahati Ndingo aende
Malinyi kwa mwalimu wake wa kuruka kamba.
Mwanakwetu upo
Mhe Bahati Ndingo
Karibu Msitu wa Mbangayao Uone Vyura Waliohama na Wapogoro.
Nakutakia siku
Njema.
0717649257
Post a Comment