KIFUTO CHAKE KIMEWEZA KUFUTA



Lucas Masunzu – MAKOLE

IKAJA siku hiyo, nduguyetu akapelekwa kuyaanza maisha mapya ya shule. Alipowasili darasani siku hiyohiyo ya kwanza aliingia jamaa mmoja akaandika chemsha bongo ubaoni halafu akaagiza kila mwanafunzi afanye ndani ya dakita tano. Chemsha bongoikafanyika, counter book zikakusanywa jamaa akaandoka nazo kumbe huyo jamaahakuwa mwalimu haukuwahi kurudi huo mzigo wa counter book mpaka kesho. Miakamingi ikapita lakini tukio hilo limebaki kama simulizi kwa nduguyetu, ni kadhiamojawapo aliyoipitia akiwa na shangazi yake wakiwa ni wanafunzi wa bweni kidato cha kwanza. Ndiyo maisha ya shule enzi hizo yalivyokwenda kila mtu anasimulizi yake!

Nduguyetu alibahatika kukua akikimbizana umri na shangazi yakcae wa mwisho hukuwakicheza na kuchunga mbuzi na koondoo wa babu yao pamoja. Maisha yalikuwamapya shuleni hapo, vuta nikuvute za hapa na pale zilitokea na kutatulika. Wiki hiyohiyoya kwanza wakiwa hawajazoea maisha ya bweni nduguyetu akapoteza mshipi mweusialiopewa na babu yake pamoja na slipa za kuogea. Akamweleza shangazi yakealiyeishi bweni jingine la wasichana akampa mbinu ya kupachika kufuri kwenyesanduku lake. Maisha yakaendelea nduguyetu na shangazi yake wakapangiwa mkondoE, wakiwa darasani walipanga dawati zao karibu na kwa haraka wakaanza kujifunza kimombo maana mawasiliano shuleni yalifanyika kwa kimombo. Kwa kuwa walikaakaribu darasani walipogonga mwamba kuwasiliana kwa kimombo, kwa sauti za chinichini za kuibiaibia waliwasiliana kwa lugha ya kabila lao maana lugha hiyowaliimudu vizuri lakini hapakuwa na mtu aliyeweza kung’amua jambo hilo.

Muhula wa masomo ukakatika shule ikafungwa wakafurahi kuona wamewafuatwa na usafiri wa ndugu zao tayari kwenda kuanza likizo ndefu wakiwa nyumbani. Wakaianza safari ya kurudi nyumbani siku hiyo waliwahi kufika maana ndugu zao hao walikuwa ni mabingwa katika kuendesha usafiri huo wa baiskeli.


Shule likizo, shule likizo ikawa ndiyo maisha yao. Hatimaye ndugu hawa wakazoea maisha ya shule wakaingia kidato cha tatu mambo yakawa mengi, shangazi akahamia mkondo wa sayansi na nduguyetu akasalia mkondo uleule. Hapo wakawa wanaona kwa nadra tena kwa mbali wakiwa kwenye msururu wakigawiwa uji na kwa siku za mwisho wa wiki walionana kwenye birika la maji wakifua sare zao za shule. Wakati mwingine walionana pale walipoitwa kwa pamoja ofisi ya makamu mkuu wa shule nahapo walifahamu wakiitwa ofisi hiyo babu yao alikuwa amewatembelea kuwaletea kalamu na mche wa sabuni ya kufulia. Wakiwa kidato cha tatu babu yao akafilisika hakuwa tena na nguvu ya kuweza kuwasomesha, mbuzi na kondoo wote waliuzwa ndipo ikabidi shangazi abaki nyumbani upendeleo wa kuendelea masomoukamwangukia nduguyetu.

Nduguyetu alihitimu na maisha yaliendelea, kwa muda mrefu akaishi kwa kuhamahama

akitafuta ugali wake, akawa anawasiliana na shangazi yake kwa simu. Miakaikaongezeka ndipo nduguyetu akamtembela shangazi yake wakiwa ni watu wazima sasa wakacheka na wakataniana sana. Haikuwa kwa kuibiaibia tena kama ilivyokuwa darasani siku hiyo waliongea kwa uhuru lugha ya kabila lao. Wakasimuliana kasheshe zilizotokea wakiwa sekondari wakakumbushana wimbo wa Bwana shamba walivyoimba siku ya kwanza shuleni.


Bwana shamba had a farm ee-eye, ee-eye-oh

And on that farm he had a cow ee- eye, ee-eye-oh

With a moo, moo here and a moo, moo there

Here a moo, there a moo, everywhere a moo, moo…

Walizungumza mambo mengi, wakamkumbuka pia mwalimu wao wa kimomboaliyempachikwa jina la Bwana Shamba baada ya kuwafundisha wimbo huo. Shangazi yake alisimulia maisha yalivyoodea kwa miaka hiyo na wakakumbushana namnaambavyo safari ya masomo ya shangazi ilivyoishia njiani. Shangazi yake alizidi kusimulia kuwa miaka hiyo hali ilikuwa ngumu mno hasa kwa wanafunzi waliotoka familia zilizo kwenye mduara wa umaskini. Kulipa karo ya shule kwa miaka hiyo hiyoilikuwa ni mzigo mzito kwa mzazi, ni ni watotot wa matajiri tu ndio waliotamba na adayao. Wazazi wa leo tushindwe wenyewe, hata kama una wanafunzi sita kwenye familia yako wanasoma bila tabu kabisa. Hakuna cha ada tena kifuto cha mheshimiwa Samia

Suluhu Hassan kimefuta kwa wanafunzi wote wa sekondari, leo hii kila mwanafunzianatamba.

Nakutakia siku njema.


theheroluke23@gmail.com


0/Post a Comment/Comments