Adeladius Makwega-MWANZA
Novemba 13, 2023 Mwnakwetu alipigiwa simu na mdau mmoja, akimpongeza kwa kuandika makala iliyopewa jina Hongera CWT Wilaya ya Magu.
Ndugu huyu alisema kuwa anamshukuru kwa makala hayo kuandikwa ili jamii iweze kujifunza,
“Taasisi zinaweza kununua magari yake, kama mabasi na malori kwa kutumia njia mbalimbali ikiwamo, mosi kupanga manunuzi katika bajeti zao za kila mwaka, pili kujibana kwa baadhi ya matumizi yasiyo ya lazima na kuachana na matumizi ya kimazoea mathalani ununuzi wa vinywaji katika vikao na hata malipo ya posho kwa wajumbe. Hapo mnaweza kujinyima kwa kipindi maalumu alafu mnanunua lori/basi lenu.
Hawa CWT walikubaliana kuwa ndani ya miezi mitatu zile pesa ambazo zinarejeshwa matawini wakiweka kadilio la kila mwalimu shilingi 5000/- zihifadhiwa na wakanunua basi hilo kwa karibu shilingi milioni 85 mwishoni mwa mwaka 2022, sasa basi hilo lina mwaka mmoja na lilinunuliwa likiwa KM 0.
Kwa sasa linamsaada mkubwa katika mambo kadhaa ya kijamii katika eneo hilo. Lakini ukifuatilia muhtasari wa vikao vyao hawa CWT unaweza kuona kuwa pengine wapo waliweza kupinga hilo ambalo kimawazo lilikuwa ni haki yao lakini wengi walikubaliana nalo. Ndiyo maana CWT ipo nchini nzima wilaya nyingi hazina basi kama hilo.
Hiki ni kisa cha kujifunza kwa kila mmoja aliyekisoma na ndiyo maana nimekupigia simu.”
Mazungumzo haya yalikuwa marefu kidogo, ndugu huyu akasema kuwa kama vyama vya wafayakazi, vyama vya siasa na vikundi vya mijumuiko mikubwa kama Makanisa na Misikiti kwa hakika wakijipanga vizuri, kuyafanya mambo kama haya ni jambo dogo tu.
Ndugu huyu alisema Kwa vyama vya siasa mathalani CCM ni chama cha miaka mingi, hakina mabasi yake katika ngazi za wilaya,mikoa na hata taifa kinategemea hisani tu, ikifika wakati wa uchaguzi baadhi ya watu wajanja wenye minufahiko katika siasa wanatoa mabasi na malori yao kuwabeba wanachama kwenda katika mikutano na vikoa hivyo na hata vile vya maamuzi .
Wanafanya hivyo wakiwa na malengo yao ya kisiasa au kiuchumi
“Kama CCM ingekuwa kila wilaya, mkoa ina mabasi yake wakati wa kura za maoni ingewabebeawajumbe wake wenyewe, inafunga mlango wanaanza safari hadi wilayani/mkoani wanafanya uchaguzi alafu wanarudishwa makwao kwa amani.
Kinachofanyika ni aibu, kila mwaka utasikia huyu kasaidia mabasi kadhaa, anapotoa basi hilo yeye anaonekana bora kuliko mwanachama fukara .
Mwenye mabasiau mchangia chama akitaka ubunge au akitaka rafiki yake a we kiongozi wa CCM anaweza kufanya hivyo kwa urahisi . Kinachofanyika kinaonekana sawa na mtoto anayejifunika macho yake kwa mikono yake huku akiona kupitia sehemu zilizo wazi katika vidole vyake lakini akisem amejificha
Mwanakwetu Kujutegemea Kiuchumu ni Kujitegeea Kimaamuzi”
Mwanakwetu alikubaliana na ndugu huyo kuwa Kujitegenea Kiuchumi Ni Kujitegemea KImaamuzi. Mwanakwetu alimwambia ndugu huyu kuwa baadhi ya wenye mabasi wanatoa vyombo vyao kuwasaidia wajumbe kwenda kwenye uchaguzi na ndani ya mabasi hayo yapo madai kuwa inakuwa kijiwe cha kutoa hongo kwa wajumbe hao.
Wajumbe wasimpomchagua mwenye mabasi au malori, siku hiyo kurudi kijijini inakuwa tabu .
Jambo hili ni
shida ya muda mrefu tangu vyama vya siasa vya Tanganyika huru , kila
mmoja kajiziba sura yake akidhani haoni lakini anaona vizuri.
Kwa hakika unapofika katika matukio ya kitafa, unaweza kuona latika runinga zetu na kusikia haya,
“Mpendwa mtazamaji katika maadhimsho haya ya miaka... ya uhuru wa Tanganyika
hilo basi linaloonekana, lenye bandera ya Tanzania, sasa wanapanada mabalozi wa
mataifa mbalimbali na basi linalofuata lilioandikw Wizara ya Mambo ya Nje watapanda wabunge wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na basi la mwisho watapanaa Makatibu wakuu wa Wizra
mbalimbali, basi lenye maandishi wa Wizara ya Mambo ya Nje watapanda wakuu wa wilaya zote za Tanzania
Bara na mabasi hayo yako matano... ”
Swali linakuja kwa mtazamajii vipi uwepo wa mabasi kama hayo katika ngazi za wilaya na Halmashauri zetu?
Wakati wa Ujamaa Wilaya zote zilikuwa na malori na hata ukienda sasa utayakuta yamechakaa yapo juu yam awe.Je Tanzania ipo likioz ya kununua malori ya Serikali?
Miaka inavyozidi kwenda , uwekezaji katika ngazi ya chini umekuwa ni ununuzi wa magari ya viongozi. Tu magari ya kifahari.
“Vipi uwekezaji wa ununuzi wa mabasi ,malori na matrekta ya ngazi za chini hadi vijijini? Vipi ununuzi wa magari ya wagonjwa katika kila Kituo cha nchini Tanzania?
Nchi hawezi kuendelea kama Waziri / Katibu Mkuu wa Wizara fulani kama anapanda gari la milioni 400 lakini lakini lakini taifa litaendelea kama kila kijiji kina lori ] la kubeba nafaka zao msimu wa mavuno kutoka shambani kwenda sokoni. Kijiji kitaendelea kama kina trekta lake lenyewe la kulimia msimu wa kilimo.
Mwanakweu siku ya leo anasema nini?
Vyama vya kijamii ikiwamo vyama vya siasa, lazima vifahamu kuwa Kujitegenea Kiuchumi ni Kijitegenea Kimaamuzi. Kinyume chake chama cha siasa kinaweza kuwekwa rehani kwa makundi ya watu kutokana na uwezo wao wa fedha.Ni kweli vyama va siasa vinahitaji pesa kufanikisha mambo yake lakini katika kupima utu wa mtu utajiri usitumike kama silaha .
Kwa serikali sasa ni wakati wake wa kuwekeza kwa walio wengi, hasa ngazi za chini, ambapo hilo siyo geni wakati wa Ujamaa vijiji vilikuwa na magari yao na hata zana za kilimo ikiwamo wanyama kazi , majembe ya plau na matrekta na jmabo lilifanya uzalishaji wa chakula kuwa maradufu japokuwa Tanzania ilikuwa na watu wachache.
“Waziri /Katibu Mkuu anaweza kwenda
kazini hata kwa baiskeli na nchi ikaendelea
vizuri kama tu kila kijiji kina trekta/lori lake na wakulima wanalima vizuri kwa
kufuata taratibu za kilimo na wakivuna mazao yao yanafika sokoni kwa wakati.”
Kwa wale ambao taasisi zao zinatoa vibali vya ununuzi wa magari serikalini wawe makini, kuweni wakali. Unapotoa vibali vingi vya ambulance kwa kila kata hilo gari la wagonjwa linaweza kukusaidia wewe mtoa kibali, hata baba yako, hata mama yako, na hata wadogo zako pale kijijini wanapopata dharura yoyote ya ugonjwa kijijini kuwafikisha hospitalini kwa wakati na wewe mwenyewe na kulinda uhai wao. na wako.
“Gari la Waziri au hata gari la Katibu Mkuu linamuhudumia mtu mmoja.”
Mwanakwetu upo?
Kujitegenea Kiuchumi ni Kujitegeea Kimaamuzi.
Nakutakia siku njema.
makwadeladius@gmail.com
0717649257
Post a Comment