Adeladius Makwega-MWANZA
Mwaka 2009 baadhi ya wakulima wa zao la korosho wa Wilaya ya
Mkuranga walipalilia mikorosho yao vizuri sana na baada ya maua kutoka wakaweka
Salpha. Hawa wakulima Mkuranga wa korosho msomaji wangu tambua ni ndugu zake
Mwanakwetu.
Msimu ulifika wakaokota korosho na kuzikusanya vizuri na
kuziweka katika magunia na kuzibeba katika lori maalumu kuelekea Dar es Salaam
kutafuta wateja.
Dar es Salaam tangu enzi ni soko kubwa la korosho za
kubanguliwa. Huku ndani ya wilaya hii ya mkoa wa Pwani ilikuwa na wanunuzi maalumu
kwa kutumia mtindo Stakabadhi Galani ambapo wakulima walikuwa wakigomea kukopwa,
wakulima walitaka malipo tasilimu na siyo mali kauli.
Wakiwa na mzigo huo kuelekea Dar es Salaam wakakamamatwa na
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga na vijana wa Halmashauri ya Mkuranga.
Baadaye wakakachiwa, huku mzigo wa magunia ya Korosho
ukachukuliwa ikawa mali ya Halmashauri ya Mkuranga.
Ndugu hao wa Mwanakwetu wakaana kuhangaika juu ya kupata mzigo
wao na maisha yalikuwa magumu huku wakikosa hata pesa ya karo na mahitaji ya za
watoto na familia zao.
Katika kutafuta suluhu hiyo hoja hiyo ikamfikia ndugu yao
Mwanakwetu na kufunga safari hadi kwa Mkuu wa Wilaya ya Mkurunga, mzee mmoja wa
Kichaga na baadaye kufika kwa Bi Sipora Liana ambaye alikuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Mkuranga.
Msomaji wangu tambua kuwa Mwanakwetu tangu
awali alikuwa anamfahamu kwa karibu BI Sipora Liana kwa kazi zake nzuri kubwa ni
kuhimiza maendeleo ya watu wa Pwani.
Shajara ya Mwanakwetu inakumbuka haya,
“Bi Liana hapo Mkuranga alihimiza upandaji mkubwa wa miembe
ya muda mfupi, ambapo ulikuwepo mradi wa kila shule ya msingi wanafunzi wake
kuokota kokwa za embe, ambazo zilinunuliwa na watu wenye vitalu na kuotesha,
alafu Halmashauri ya Mkuranga kuisambaza miche hiyo vijijini bure maana
kulikuwa na madai kuwa tajiri mmoja atajenga kiwanda cha juisi eneo hilo.
Mwanakwetu na shangazi yake anayeifahamika kama Christina Makwega walipata
miche 20 ya miembe ya Bi Sipora Liana na sasa miembe hiyo inazaa embe hapo hapo
Mkuranga.”
Kumbuka tu msomaji wangu Mwanakwetu yupo na ndugu zake
ofisini kwa Bi Liana na yeye alimuheshimu mno Mwanakwetu ambaye aliambatana na
Ustadh Kumbirwa wakiwa miongoni mwa ndugu waliokuwa na mzigo wa orosho hizo.
“Hawa ndugu zako walichokifanya ni kutorosha zao letu na
kuinyima Halmashauri yetu ya Mkuranga mapato.Gari hilo lilikutwa linapita njia
za panya. Mapato haya si yangu,si ya Mzee Liana yanatumika kuleta maendeleo ya
wilaya yenu.”
Mazungumzo yalikuwa marefu na
wakulima hao hawakupewa korosho zao na hivyo ndugu hao kwenda mahakamani mwaka huo
huo 2010 .
Yule aliyekuwa Mkuu wa Wilaya
Mkuranga kwa bahati mbaya baada ya uchaguzi wa 2010 hakuteuliwa tena kuwa Mkuu
wa Wilaya hii lakini Sipora Liana-Dada wa Mwanakwetu , Mkurugenzi Hodari aliendelea
na kazi.
Kesi mahakamni inaendelea na ndugu wa
Mwanakwetu wakisaidiwa na wakili wao makini.
Msomaji wangu maisha yanaendelea.
Mwaka 2011 aliyekuwa Mkurugeni Mkuu
wa TAKUKURU Tanzania Dkt. Edward Hoseah akaitisha mkutano wa wadau wa TAKUKURU
kwa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam na mkutano huo ulifanyika UBUNGO PLAZA (Jina la zamani) sasa jengo
hilo linaitwa BLUE PEAR.
Mdau mmojawapo aliyealikwa katika
mkutano huo alikuwa Mwanakwetu kwa mwaliko wa Dkt. Edward Hoseah mwenyewe.
“Wewe ni mdau wetu muhimu katika kuzuia na kupambana na rushwa
hapa nchini, hivyo kwa heshima zote unaombwa kuhudhuria semina hiyo ya siku
mbili hapa Ubungo Plaza.”
Mwanakwetu alifika na kupewa begi la
nyaraka na kitambulisho chenye jina lake akakivaa vizuri na kuingia kikaoni. Katika
Mkutano huo hoja ya wakulima Korosho iliibuka madai yalikuwa ni matumizi mabaya
ya madaraka ya viongozi wetu.
Mwanakweu alikuwepo na akachangia
kidogo katik hilo, Ustadh Kumbira nayeye alialikwa na kumbe BI Sipora Liana nayeye
alikuwa miongoni mwa waalikwa japokuwa hakusema neno lolote katika kikao hicho
cha siku mbili.
Kwa bahati nzuri Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU wakati huo Dkt. Edward Hoseah alisimama na kulijibu swali hilo vizuri
katika majumuisho yake ambapo Mwanakwetu sasa anakutana kwa mara ya kwanza na
Dkt Hoseah.
“Hilo suala tuliache kwa kuwa lipo mahakamani, lakini kikubwa
wananchi wanapokuwa na jambo lao wasisite kutoa hisia zao katika jambo hilo,
sisi tunaosimimamia vyombo hivi tunapaswa kutambua utaratibu ukoje na tutoa
majibu sahihi kwao bila kufanya uonevu wowote ule.”
Baada ya kikao hicho waishiriki wote
walikula chakula cha mchana na mkutano huo uliokwisha wajumbe walipewa poshi
zao akiwamo Mwanakwetu na kupiga picha na watumishi wa TAKUKURU wakati huo akiwamo
Dkt Edward Hoseah.
Wakati wa kupiga picha Mwanakwetu
alibaini kuwa Bi Spora Liana alikuwa kando
na Theophili Makunga ambaye alikuwa ana cheo kikubwa katika mojawapo ya
magazeti ya hapa Tanzania wakati huo.
Mkunga na Bi Liana wakamuita
Mwanakwetu na kuzungumza kwa kirefu mno, Mwanakwetu akimpa heshima zote Theopili Makunga maana alikuwa mwanahabari
mwenzake, baada ya mazungumzo hayo kila mmoja kurudi nyumbani kwake.
2011 ukapita, 2012 ukapita, 2013 pia
2014 nao pia , 2015 ukaishi na ukaja 2016.Huku kesi ya wale wakulima wa korosho
inaendelea mahakamani naye Bi Sipora Liana
akizunguka katika Halmashauri kadhaa za Tanzania akichapa kazi .
Wale wakulima wengine wanafariki dunia
huku sasa kampuni ya uwakili inandelea na kesi mahakamani nao warithi ya
korosho hizo wakiendelea kufuatiliwa haki yao mahakamani.
Julai 7, 2016 Rais John Magufuli
alimtuwa Mwanakwetu kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Lushoto Tanga,
naye Bi Sipora Liana akawa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam ambapo uteuzi
huo kwa Bi Liana ulikuwa wa haki maana alikuwa Mkurugenzi mzoefu na mwenye
uwezo mkubwa wa kazi
Julai 12, 2016 Mwanakwetu akakutana Bi
Spora Liana Ikulu ya Magogoni.
BI Sipora Liana akacheka sana akasema,
“Haya mkulima wa korosho wa Mkuranga, njoo uyaone mwenyewe
huku mambo yalivyo ili uje kusimuliandugu zako wa Mkuranga .”
Kweli kikao hicho cha
Rais Magufuli kilifanyika na kila Mkurugenzi aliyeteuliwa kuelekea katika
kituaochake chake cha kazi alichopangiwa.
Mwanakwetu Upo?
Mwanakwetu siku ya
leo anasema nini?
Mwanakwetu amewakumbuka
ndugu zake wanne;
Kwanza wale walkulima
wa korosho ambao walipata haki yao mahakamani mwaka 2018, miaka minane baadaye.
Wengi haki hiyo hawakuiona kwa macho yao bali warithi wao maana wao walishalala
makaburini.
Pili Mwanakwetu
amemkumbuka Theophili Makunga- Mwanahabari Mkongwe wa Tanzania na mazungumzo
yao pale Ubungo Plaza baada ya
kupiga picha na Dkt Edward Hosea.
Tatu amemkumkumbuka
dada yake Bi Sipora Liana ambaye alimwambia Mwanakwetu maneno haya,
“Haya mkulima wa korosho wa Mkuranga, njoo uyaone mwenyewe
huku mambo yalivyo ili uje kusimulia ndugu zako wa Mkuranga .”
Mwisho Mwanakwetu
amemkumbuka Dkt. Edward Hoseah ambaye alikuwa Mkurugenzi wa TAKUKURU alikuwa ni
kiongozi na sifa moja kubwa ya uwanadiplomasia ambapo aliweza kufanya kazi
vizuri ya kuzuia rushwa kwa kutumi uwezo wake mkubwa wa diplomasia na kushaswishi
kutumia semina , mafunzo akiwakusanya wana taalumu mbalimbali katika kuifanya
kazi hiyo. Huku akiwatambua watu weye vipaji mbalimbali vya ushawishi katika
jamii.
Msomaji wangu tambua
kuwa Dkt. Edward Hoseah alitambua kuwa TAKUKURU
ina KU mbili ambazo zinabeba majukumu mawili ya chombo hiki. Kwanza kuzuia hapo
inahitaji elimu na diplomsia ya juu alafu ndipo unakuja Ku ya pili unapambana
na rushwa ambapo hapo sasa unatumia upolisi.
Mwanakwetu upo?
Dkt.Edward Hoseah
alikuwa Mkurugenzi wa TAKUKURU Mwanadiplomasia.
Nakutaki siku njema.
0717649257
Post a Comment