Mkuu wa Mkoa Ametangaza kuwaondoa Wafanyabiashara Holela katika mjin wa iringa



Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh.Halima Dendego ametangaza oparesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara holela katika mji wa Iringa kuanzia Nov 19 na itakuwa oparesheni endelevu huku akiitangaza kuwa oparesheni ya mwisho ya kuwaondoa wafanyabiashara holela na kuwataka wale wanaofanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi kuondoka katika maeneo hayo.



Dendego ametoa tamko hilo  Leo wakati wa mkutano wake na viongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara Mkoa wa Iringa,Umoja wa wafanyabiashara wa masoko na Shirikisho la umoja wa Machinga Mkoa wa Iringa na kusisitiza wafanyabiashara hao kufanya shughuli zao katika maeneo waliyopangiwa ili kufanya biashara kwa utulivu na kuondoa mivutano isiyokuwa na lazima.


Eliasa Ally

0/Post a Comment/Comments