MPOGOLO ANAYEENDELEA KULA ADHABU

 

Adeladius Makwega-MWANZA

Mwanakwetu yu Malya Kwimba kwa muda wa nusu mwaka sasa, kila mara hapa Malya amekuwa akipata changamoto ya viatu vyake vinachomoka visigino, cha kusikitisha tangu kiatu cha kwanza hadi jozi ya nne hakubatahatika kuweza kukipata kisigino kilichomoka.

Ndiyo kusema jozi zake nne za viatu zilichomoka na sasa zilikuwa  hawezi kuvivaa tena. Mwanakwetu akabaki na jozi tatu tu zilizo salama yaani jozi moja ya mvua , jozi moja ya kiofisi na jozi nyingine ya Tumpeleke Bwana Huyu .

Mwanakwetu akaamua azikusanye jozi zake zote zilizopoteza visigino, akazibeba hadi kwa fundi viatu.

Akiwa njiani na mzigo wake wa viatu alipita eneo moja akasikia azana ikipigwa.

“Allahu Akbar (Mara Nne))

Ashhadu alla ilaha illallah (Mara Mbili)

Ashhadu anna Muhammadar Rasulullah (mara mbili)

Hayya ‘alas-Salah (mara mbili)

Hayya ‘alal-Falah (Mara Mbili)

Allahu Akbar (Mara Mbili)”

Eneo hilo ambalo azana hiyo inapigwa lilimshangaza Mwanakwetu, akajiuliza hapa pana msikiti ? Mbona nipo Malya zaidi ya miezi sita na huo msikiti siufahamu?

Mwanakwetu aliendelea na safari yake, huku kabeba mfuko wa viatu vyake vilivyochomoka visigino na alipofika pahala pa fundi vaitu, hakuwepo na alipouliza fundi yua wapi alipigiwa simu na kufika.

Akamkabidhi viatu hivyo,



Fundi akaviangalia viatu hiivyo akacheka sana, alafu akasema,

“Ndugu mbona viatu vyako vimechomoka visigino tu?”

Mwanakwreu akajibu ndiyo maana nipo kwako nimekuja uniwekee visigino vingine. Jamaa kando ya  fundi anacheka mno.

Jamaa huyu akauliza,

“Wewe kabila gani ?”

Mwanakwteu akajibu kuwa yeye Mpogolo . Jamaa akaendelea kucheka tu, hapo Mwanakwetu katulia tuli.

Jamaa kando ya fundi akasema Wapogolo kwenu mnalima sana mpunga ?

Mwankawtu akajibu naam.

Jamaa akauliuza mpunga wenu ukoje?

“Mpunga wetu ukipikwa wali unanukia sana kuliko mpunga wa Wasukuma.”

Jamaa mmoja kando ya fundi  ambaye alikuwa kimya akacheka sana,

“Wewe ndiyo maana visigino vyako vinapotea kila siku, na vitaendelea kupotea hata hivi vivayotengeneza leo vitachomoka tu. Wewe haushangai vimechomoka vya mguu wa kulia tu.”

Mwanakwetu akajibu visigino vya viatu vyangu vimechomoka kwa kuwa pengine kutokan na kubadili mazingira tu si kitu kingine.Pingine  vilizoea sakafu,maru maru na lami sasa nyini Wasukuma hamna hata kimoja.

Jamaa wa kwanza kuongea akasema

“Daa wewe Mpogolo wewe, Mpunga wa Wapogoro unukie zaidi ya mpunga Wasukuma. Wewe umechelewa kabisa .”

Jamaa huyu akaongeza kuwa wewe hapa nyumbani kwako wali wetu wa hapa Mwanza anakupigia nani?Mwanakwetu akajibu kuwa  mara nyingi anakula mkahawani na mara nyingine anapika mwenyewe.

Jamaa mmoja kando ya fundi akasema,

“Wewe unataka wali unukie alafu unakula kwa mama ntilie? Unakula Mkahawani?Ukitaka wali unukie tafuta binti wa Kisukuma akupikie utauelewa wali wa  Wasukuma kuliko wali wa Wapogolo.”

Fundi viatu anaendelea na kazi yake, viatu hivyo vlitengenezwa vizuri na visogino hivyo kurudishiwa.

Mwanakwetu akallpa pesa ya kazi hiyo alafu akawauliza hawa jamaa ili visigino vyake vya viatu viisichomoke tena afanye nini?

Jamaa kando ya fundi akauliza kaka bado haujapata jibu?


(Mama wa Kipogolo akiwa katika shamba lake la mpunga)

Jamaa wanacheka kweli kweli,

“Siku utakapo pikiwa wali na binti wa Kisukuma na ukasikia wali wetu unanukia ndipo visigino vyako vya viatu vinakapoacha kuchomoka, sasa hivi tunakupa adhabu kwanza hadi somo hilo ulielewe.”

Mwanakwetu aliwaaga na kuelekea kwake , alipita njia ile ya msikiti na alipofika ulipo msikiti ule aliyosikia azana alikutana jamaa wanatoka msikiti akawasalimu vizuri na aliwauliza juu ya msikiti wao.

“Ule wa bondeni ni msikiti wa Suni na wa BAKWATA na huu wetu hapa ni wa Shia hapa Malya.”

Mwanakwetu alifika nyumbani kwake salama salimini na alikaa majuma mawili  bila ya visigino vya viatu vyake  kuchomoka, Novemba 7, 2023 alivaa viatu vyake vyeusi miongoni mwa jozi zile nne  zilivyotengenezwa na majira ya saa sita mchana ya siku hiyo alishangazwa kisigoni kimechomoka na hata alipokitafuta hakukiona , alishuka kwa fundi viatu kukitengeza kisigino hicho.

Fundi huyu alimpokea Mwanakwetu alafu akasema,

Ahaa Mpogolo Anayeendelea Kula Adhabu.”

Fundi huyu siku hii alikuwa peke yake, maneno yalikuwa machache, kisigino kipya kiliwekwa na hapo Mwanakwetu kulipishwa shilingi 2000/- na kwenda zake.

Mwanakwetu Upo?

Kumbuka tu Mpogolo Anayeendelea Kula Adhabu

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257




0/Post a Comment/Comments