Adeladius Makwega-MWANZA
Mwanakwetu alikuwa safarini , basi hilo halikuwa la safari
ndefu sana, baada ya mwendo kiasi wakafika pahala ambapo kulikuwa mkahawa,
abiria kushuka kuchimba dawa na kula chakula.
Kwa hakika abiria wengi walishuka tu kuchimba dawa na wachache
mno waliingia mkahawani humo kula chakula. Siku hiyo Mwanakwetu alikuwa lodi--
Lodi Makwega maana mpangaji wake mmoja alimlipa kodi ya mwaka.
Mwanakwetu aliingia kifua mbele katika mkahawa huo na alibaini bei ya vyakula
na vinywaji ilikuwa aghali mno.
Huu ulikuwa mkahawa wa malodi ,naye Mwanakwetu alikuwa Lodi
wa Msimu
Bei ya soda ilikuwa shlingi kati ya 1000/1500.na kuagiza wali
na nyama na kulipa shilingi 7000/- na kuanza kula chakula hicho
Ndani ya mkahawa huu kulikuwa na watu wachache kama nilivyokwambia
msomaji wangu,, kama abiria wote 70 wa basi hilo wangeingia basi viti na meza
vya mkahawa huu visingetosha.
Mkono wa kulia kwa Mwanakwetu walikuwapo vijana wawili ambao
walikuwa wakiongea huku mikono yao imeshika vitu kama funguo nyingi .
“Unajua hizi safari za dharura siyo nzuri, mimi nimetoka
nyumbani kwangu najua naenda kazini, kufika hapo nimejulishwa kuwa kuna safari
ya kwenda Dodoma, mfukoni kwangu sina pesa ,sina chochote. Mwanaume nina kengele tu.”
Jamaa pembeni yake akawa anacheka alafu
akasema chukua hizo kengele zifanye pesa. Sasa huko Dodoma utakwenda kuishije?
Na usawa wenywe ndiyo huu?
“Bosi kaniwezesha na kasema kama tukifika
Dodoma salama, jamaa wa uhasibu atayaweka mambo sawa. Kwa hiyo kwa siku hizi
mbili za mwanzo bosi wangu atanilinda.”
Jamaa kando akasema
hongera kwa kupata kiongozi muungwana, Ole Wako Upate Kiongozi Mbinafsi .
“Yaani mimi katika kazi yangu hii ya
udereva serikalini mara zote ninaomba Mungu aniepushe kufanya kazi na kiongozi
mbinafsi. Kuna jamaa yangu mmoja alikuwa Halmashauri, alipata kiongozi wake
mbinafsi, maisha yake yalikuwa magumu mno, yaani safari za kushitukiza tele,
mnafika mkahawani bosi anaingia kula chakula yeye mwenyewe na huku wewe kakuacha
katika usukani, anakula vizuri na akirudi anasema, ‘Nimeliza kula sasa tuondoke.’ Hafikilii kabisa kuwa na wewe una njaa
kama yeye na wewe hauna pesa, vipi kuhus familia yako nyumbani. Je utaweza
kufanya kazi kwa njaa? Wakati yeye amekaa pembeni yako na ametoka kula?”
Kumbuka msomaji wangu
Mwanakwetu anakula mkahawani na jamaa kando yake wanaongea.
Gafla basi alilopanda
Mwanakwetu likapiga honi,
Piiiiiiiiiiiiiiii. Piiiiiiiiiiiiiiiii,
Piiiiiiiiiiiiiii, Piiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Kuwajulisha abiria wote
waingie ndani waendelee na safari. Mwanakweu alibeba chakula chake na kutoka
mkahawani, wakati anatoka tu alikutana na magari madogo mawili aina Land Cruzer
yamepaki pembeni yakiwa na namba za serikali, akasema pengine haya ni magari ya
hawa vijana.
Aliingia ndani ya basi hilo na kukaa katika kiti chake,
kuendelea na safari huku akilini mwake akiwakumbuka wale vijana madereva
mkahawani, hasa neno lao hili,
“Mara Zote Namuomba Mungu, Nisipate
Bosi Mbinafsi.”
Wakati safari hiyo inaendelea
Mwanakwetu akafungua simu yake na kukutana na habari katika mitandao ya kijamii
Kuwa Waziri wa TAMISEMI mh. Mohammed Mchengerwa amewasimamisha kazi Wakurugenzi
Watendaji wawili Butamo Nuru na Halmashauri ya Kibaha mkoani Pwani na Lena
Nkaya wa Halmashauri ya Ifakara.
“Waziri Mchengerwa amefanya uamuzi
huo baada ya kupokea taarifa ya awali kutoka Kamati iliyoundwa na Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo, Wakurugenzi hao wakidaiwa kushindwa kusimamia miradi ya
maendeleo katika halmashauri hizo hizo kwa nyakati tofauti.”
Mwanakwetu anaendelea na
safari na hapo hapo akapitiwa na usingizi na kulala kwa muda kigogo kutokana na
ubovu wa barabara hii hakuweza kulala sana alishituka na alipoamka aliichukua
simu yake na hapo hapo alikutana na taarifa aliyoisoma ya Wakurugenzi wale
wawili ipo katika ukuta wa simu yake.
Mwanakwetu akasema
moyoni,
“Ebo sisi tuntaaka miradi ikamilike ,
hiyo kamati iliyoundwa na huyu Katibu
Mkuu TAMISEMI wangeenda kusimamia miradi hiyo ikamilike , siyo kwneda kukusanya
maneno. Maneno hayakamilishii miradi.”
Hapo yakamjia maswali
mengi, Kweli jamani watu wazima lukuki wanaungana kuwapotezea maisha wakurugenzi
hawa wawili?.
Tafakari ilikuwa kubwa
sana kwa Mwanakwetu siku hii.
“Waziri wa TAMISEMI unapomsimisha
Mkurugenzi Mtendaji kwa madai ya kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo katika
Halmashauri hiyo ni hoja dhaifu. Hapo inaibuka hoja ya uonevu kwa watoto wa
watu. Katika eneo alipo Mkurugenzi Mtendaji yupo Mkuu wa Wilaya yeye mbona hajachukuliwa
hatua? Katika eneo hilo wapo madiwani katika baraza lao karibu watu 50 mbona
hawajachukuliwa hatua? Yuko Mwenyekiti wa Halmashauri mbona hajachukuliwa
hatua? Yupo Mbunge wa jimbo mbona hajachukuliwa hatua?Yupo Mbunge wa viti
Maalumu mbona hawajachukuliwa hatua? Ipo Kamati ya Siasa ya Wilaya ya CCM
ambayo huwa inakagua miradi hiyo mbona haijachukuliwa hatua? Wapo Wajumbe wa
Kamati za Ulinzi Wilaya yenye Katibu Tawala
wa Wilaya na wajumbe wengine wa kamati hiyo mbona hawajachukuliwa hatua. Katika
eneo hilo yupo Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani na Mkuu wake wa Mkoa na hivyo
hivyo kwa mkoa wa Morogoro mbona wao wanaendelea kupuyanga tu.? Waziri wa
TAMISEMI utoke Dodoma na kuwaadhibu watoto wa watu? Huo kama siyo uonevu ni
nini? Kundi kubwa la wanasiasa ambalo ndiyo linawajibu mkubwa wa kuihamasisha
jamii katika miradi ya maendeleo linabaki na kuwabebebesha mzigo watumishi wa
umma hilo halikubaliki.”
Mwanakwetu anaendelea na
safari yake, hapo hapo akakumbuka maneno ya wale vijana pale mkahawani kuwa
unapokuwa na viongozi wabinafsi ni hatari sana.
Mwanakwetu alishuka na
kuendelea na safari hadi kwake.
Mwanakwetu anasema nini siku
ya leo?
Mhe Mchengerwa anatakiwa
kutambua kuwa yeye kama waziri anawajibu wa kulinda maslahi ya wanasiasa na
maslahi ya watumishi wa umma. Yeye kama waziri wa TAMISEMI atambue TAMISEMI ina
watumishi wengi wanaowahudumia Watanzania . Yeye kama waziri asipoonesha upendo
kwa watumishi wa TAMISEMI hakuna wa kufanya hivyo. Kuendelea kufukuza hakuna
tija kwake wale kwa serikali , wala kwa chama chake na wala kwa Watanzania,
kuwafukuza kazi ni kuwachukia watumishi na jamii ya Watanzania hilo linawakera
Mwanakwetu anatambua
kuwa Waziri wa TAMISEMI ni Rais mwenyewe, Rais mwenyewe atoe muelekeo wa
TAMISEMI na hizi tabia za kufukuzana na kuwasimisha kazi watoto wa watu katika uchunguzi
wa awali hazifahi, waiache mahakama ifanye kazi hapo ndipo maamuzi mengine yafanyike.
Timu inapopoteza mchezo kosa siyo ya golikipa pekee kwa kuwa yupo golini , makosa ni ya timu nzima, mathalani Kamati za Ulinzi za Wilaya na Mikoa zipo wapi kusimamia miradi hiyo inayokwama? Kamati za Ulinzi na usalama siyo jukumu lao kutekeleza majukumu ya kazi zao la msingi tu na kutambulishwa wakati wa ugeni bali na kazi yao nyingine ni kusimamia miradi hii inayokwama , hata Mbunge wa jimbo ambalo Mkurugenzi amesimamishwa jina lake 2025 CCM lisilirusdishe kugombea ubunge na hata diwani ambaye kata yake miradi hiyo haikusimamiwa vizuri jina lake lisirudishwe.Hapo kazi itafanyika siyoi kuwabebesha mizigo hiyo wakurugenzi peke yao.
Kubwa wale wanaofanya
maamuzi hayo watambue kuwa na wao siyo safi hata kama wanajinasibu wao ni safi.Waziri
Mchengerwa atambue kuwa jamii inafahamu namna anavyoshinda kura za maoni za CCM
kupata tikeyi ya ubunge jimboni kwake ,zipo simulizi nyingi katika hilo.
kila mmoja anayo madhaifu yake mengi kikubwa
tuheshimiane, turekebishane kwa staha na kama kuwajibisha tusibaguane .
Mwanakwetu Upo?
Nakutakia siku Njema.
0717649257
Post a Comment