Adeladius Makwega-MWANZA
Mwanakwetu alipigiwa simu na ndugu mmoja ambaye ni Mngoni, akijitambulsha kuwa amesoma makala ya Mwanakwetu juu ya ujio wa Rais wa Ujerumani nchini Tanzania ,akisema kuwa Wao kama Wangoni wameshasamehe katika hilo.
Kitendo cha Rais wa Ujerumani kukanyaga Ardhi ya Wangoni na kuomba radhi kina maana kubwa.
Mwanakwetu alimuuliza ndugu huyu kina maana gani?
“Kwanza hilo halikufanyika bure, Wajerumani kipo lipo walichokipata hadi wakafunga safari kutoka huko hadi kufika Songea, kwa nini hawakwenda kwa Kinjeketile Ngwale?Walikwenda moja kwa moja Songea? ”
Ndugu huyu akisema kuwa wazee wao hawakuondoka bure, walikasirika mno na hasira hiyo ni ya kizazi na kizazi lakini sasa mzigo umetuliwa kwa Wajerumani.
“Vita vya Maji Maji tangu viishe ni miaka zaidi ya 116, hapo vimepita vizazi vingine . Kile kilichohusika. Kwa hesabu zakawaida Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier umri wake wa sasa ni miaka 67, hapo amezaliwa mwaka 1956 huko Detmold . Hilo likimaanisha kuwa kizazi cha babu wa kiongozi huyo kinacholinga nae kilichotuhumiwa kufanya kadhia hiyo hapa Tangayika. Babu, Baba, Mtoto (Frank Walter Steinmeier) Mjukuu, Kitukuu na sasa wapo Kininginila .”
Mazungumzo na ndugu huyu yalibua hoja kuwa vita vya Maji Maji vilishirikisha makabila mengi na pengine tukio la kabila la Wangoni linakumbukwa sana kutokana na kuwepo na kumbukumbu nzuri zilizofanywa na Wamisionari.
“Nina hakika kama makabila mengine yangekuwa yamefanya uhifadhi wa kumbukumbu za vita hivyo kwa hakika kungekuwa na uelewa mkubwa juu madhara ya vita vya MajiMaji katika ardhi ya Tanganyika.”
Katika mazungumzo haya kuliibuka hoja kuwa kama kungekuwa na kumbukumbu za kutosha, je Ujerumani ingeweza kupita kote kuomba msamaha?
“Kikubwa ni kiongozi huyu wa taifa hilo kuomba msamaha makosa yaliyofanywa na ndugu zake na sasa hatuna budi kusamehe.”
Kikubwa ulimwengu umefahamu kuwa yapo mabaya yamefanyika na kuombewa msamaha.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?Kwa hakika kila anayeomba msamaha anapaswa kusamehewa kwa kosa analolijitia.Ni ukweli ulio wazi kuwa safari ya kutoka kwako kwenda kuomba msamaha ina mengi.
“Kwanza kunakuwa na vikao vya
hapa na pale, pili unabaini kuwa kuna ukweli wa kosa lilifanyika, kwa hakika linawahusisha
watu walio jirani na nawe. Je kweli msamaha uombwe , panapokubaliwa hilo, ndipo
msamaha unaombwa.Baada ya maombi hayo kusemwa je waliombwa msamaha wanasema
nini?”
Kwa hakika jambo moja lifahamike kuwa kunyongwa kwa Watawala wa Wangoni kulifanyika wakati Ujerumani ni mtawala wa Tanganyika. Jamabo hilo liliwavunja nguvu kubwa makabila mengi yaliyoshiriki vita hivyo na kujenga uwoga kwa jamii za Tanganyika wakati huo
Mwanakwetu Upo?
Kumbuka Urefu wa Safari ya Msamaha
Nakutakia siku njema.
0717649257
Post a Comment