Adeladius Makwega-MWANZA
Kumekuwa na dhana kuwa Serikali huwa haipati hasara, jambo hulo linasemwa na wengi ambao wengine wapo Serikalini huku wanalipwa mishahara kwa Serikali hizo na dhana hiyo inajaribu kuambukizwa hata wale wasiolipwa mishahara na serikali.
Msemo ukiwa ule ule,
“Serikali Haina Hasara.”
Dhana hiyo kabla ya kukubaliana nayo au kuikataa ni lazima upate majibu juu ya huyo ni mwenye Serikali ni nani?
Wapo baadhi ya watu wanaamni Serikali ni ule mfumo wa kiutendaji na ni wale wanaohudumu katika huo mfumo. Wengi wanaoliamini hilo ni wale wanaohudumu katika mfumo huo katika nafasi hasa za juu na hawa ndiyo wengi na hata baadhi ya wachache wale ngazi za chini.
“Serikali
ni watu wenyewe, wakijiongoza wao wenyewe, kutoka miongoni mwao, hasa wale
wanaowaamini, wenye umahiri wa kuwapitisha katika njia moja yenye madaraja
mengi .
Huku
hawa wachache wakipewa nguvu, iwe ya mawazo, fedha, ujuzi na hata rasilimali
huku wakipokezana miongoni mwao.”
Nakuomba msomaji wangu soma kisa hiki cha kweli cha Serikali za Kiafrika,
“Taasisi moja ya umma ilikuwa inamuhitaji mtumishi wa umma aene awaongeze nguvu kiutendaji taasisi mpya , jamaa hawa waliotangulia kuianzisha taasisi hii wakawa na sifa za mtu wanayemtaka kwa nafasi hiyo. Wakafanya uchunguzi maana ilikuwa tasisi mpya ya Wizara mojawapo, huku hata hawa jamaa walihamishiwa hapo kutoka taasisi zingine za umma kwenda kuongeza nguvu.
Walipofanya utafiti wakabaini mtaalamu mmoja ambaye na yeye alikuwa mtumishi serikalini lakini Wizara nyingine. Mkuu wa taasisi akaandika barua yake vizuri na kumuomba ndugu huyo ahamishiwe hapo, kwenda kuongeza nguvu.Barua zikaandikwa mbili moja kwa mwajiri wake kwa taarifa nay a pili kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ajira ya kumuomba mtumishi huyo.
Barua zikapelekwa vizuri, hawa jamaa wa Wizara ya Ajira wakamfuatilia mtumishi huyo alafu wakajibu barua hiyo.
‘Tumepokea maombi yenu ya kuomba
mtumishi tajwa ahamishiwe hapa kwenu, maombi yenu yamekataliwa na kwa barua
tunamuagiza mwajili wa mtumishi huyu amchukulie hatua za kinidhamu, ili kujenga
nidhamu katika utumishi wa umma.’
Jamaa wakapata barua na kuisoma wakajiuliza
sisi tunahitaji kile kipaji chake kije kuongeza nguvu, hawa wakubwa wao wameona
madhaifu. Kwani huyo bwana ni mwizi? Jamaa wakafuatilia hakuna wizi wala jinai yoyote
bali
majungu ya huyu kenda pale huyu karudi pale.
Hii barua ya majibu ilijibiwa na kusainiwa na Kwa Niaba ya Katibu Mkuu. Mdau mmoja wa taasisi hii akasema labda tumfuate Katibu Mkuu tumuhoji. Mdau mwingine akasema, ‘Hao achaneni nao, jamaa ndiyo wale wale wanaosema Serikali Haina Hasara .Yaani sisi tunamuhitaji mtumishi wa kutuongezea nguvu wao, tunataja kwa jina, jamaa wao wanasema aadhibiwe? Tuachane nao , tusiwatafutie shida watoto wa watu.
Sisi tumeuona umahiri wa mtu wao wanatuonyesha udhaifu na adhabu juu yake.Hata sisi tukiamua kumfuatilia lhuyu aliyeandika barua hii na kusaini hapa chini hapo hapo ofisini kwake tutakutana na madhaifu yake mengi na mengine hayatavumiliki.’
Kibaya hata huyu jamaa mwenyewe hawamtumii kabisa.
Aaah Kweli Serikali Haina Hasara.”
Msomaji wangu upo?Mambo ndiyo yale yale ,
“ Serikali Haina Hasara.”
Swali la kujiuluza huyu aliyeandika barua ya majibu kwa taasisi kwa Niaba ya Katibu Mkuu ambaye jina lake linasomeska chini ya barua hiyo tena majina matatu; lake mwenyewe, la baba yake na babu yake anatambua kuwa barua hiyo inabaki milele?
Anatambua kuwa kazi yake ilikuwa ni kumuhamisha tu mtumishi huyo ? Anatambua kuwa kazi hiyo ilihitaji mtaalamu ambaye taasisi husika ilishambaini ?
Anatambua kuwa maamuzi yake yanahidhoofisha taasisi hii ya umma?
Nakuuma sikio kuwa taasisi hiyo iliyomuomba jamaa huyu haikufanya vizuri ilifeli vibaya sana.
Mwanakwetu anasema nini siku ya Leo?
Kama dhana ya serikali ni lile kundi la watawala wachache na wenye nafasi na huku zinazotumika kodi wanazolipa wao tu, hapo kweli serikali haina hasara.
Kama maana ya serikali ni hawa watu walio wengi na miongoni mwao wamewachaguana ili viongozi wao kuwavusha kutoka daraja moja kwenda lingine, hapo serikala ina hasara na tena kubwa kwa walipa kodi ambao ndiyo walio wengi.
Mwanakwetu Upo?
Wenzako Wanaona Umahiri, Wewe Unaona Madhaifu.
Wenzako wanatafuta mtu mwenye umahiri wa kuuzima moto , wewe unataja madhaifu huku moto unaendelea kuwaka na kuleta madhara.
Umahiri Unaivusha Jamii.
Tuachane na hizi habari za ati Serikali Haina Hasara,
Nakutaki siku Njema.
0717649257
Post a Comment