Adeladius
Makwega-MWANZA
Ijumaa ya Novemba 24,2023 Mwanakwetu alipita katika kundi
lenye jina MwAnAKwEtU la mitandao ya kijamii saa 5 na dakika 13 ya usiku aliona
nakala ya jarida la Nchi Yetu ambalo
linatolewa na Idara ya Habari Maelezo.
Kwa wale ambao ni hawalifahamu jarida hilo ni jarida la
serikali la miaka mingi, linatolewa na idara hiyo tangu enzi za SHIHATA na
wakati huo likitolewa likiwa na rangi nyeusi na nyeupe tu lakini maendeleo ya
tekinolojia sasa linaotolewa likiwa la rangi.
Jarida hilo ni namba 801 ambalo limetolewa huku Idara hii
ikiongozwa na ndugu Mobhare Matinyi ambaye sasa ndiye mkurugenzi wa Idara hiyo
ya serikali. Jarida hilo lina kurasa 12 zenye maandishi ikiwamo matini kadhaa
zenye habari na matangazo.
Mwanakwetu alilitazama jarida hilo na kutamani kuona mchango
wa umahiri wa mkurugenzi mpya wa Idara hii, akipitia habari moja baada nyingine
na hata uteuzi wa picha katika jarida hilo.
Kwanza aliisoma habari hii Dkt. Biteko Akutana na Balozi wa China Nchini Tanzania. Mwanakwetu
alipoisoma habari hyo alijiuliza je kukutana kwa Biteko na Balozi wa China kuna
maana gani kwa msomaji wa
Ifahamike wazi kuwa jarida hili halitoki kila siku, lilipaswa
kuwaachia wengine juu ya huko kukutana yaani vyombo vingine vya habari; kama
vile redio, runinga na magazeti ya kila siku. Hivyo Idara ya Habari Maelezo
ingejikita katika mazungumzo hayo ya China na Tanzania.
Pia kichwa cha habari kinatakiwa kuwa kifupi , chenye maneno
machache na cha kuvutia , mathalani
“China Kuboresha Umeme Tanzania.”
Mobhare Matinyi afahamu kuwa habari
ni sayansi ya sanaa na uumbaji wa maneno katika sentensi zenye kuvutia kwa
msomaji, msikiliza na hata mtazamaji, hapa hatuandiki kama mtu anaomba kazi. Hapa
ni sanaa ya maneno.
Jambo la pili ambalo Mwanakwetu alijiuliza, hivi kulikuwa na
haja gani ya jarida hilo kuficha jina la mwandishi wa habari hizo na kuandika MWANDISHI WETU?
Mwanakwetu anasema kuwa yeye anahisi kuwa habari hizo zimeandikwa
na Mobhare Matinyi mwenyewe na jina hilo limefichwa makusudi na kwa faida
binafsi.Ifahamike wazi kuwa jina la mwandishi mara nying linafichwa katika habari
za uchunguzi ili kumlinda na shida yoyote baadaye. Kwa hakika tangu jarida hilo
lianze halijawahi kufanya habari za uchunguzi na hata habari zote mbili
zilizoandikwa kwa kuficha jina la mwandishi hazina shida yoyote kwa mwandishi na
habari , jina lake likifahamika labda woga kukosolewa.
Hata tukihoji ilikuwaje ukaficha jina la mwandishi ,majibu
hayapo.
Habari ya ya pili ambaye jina la mwandishi limefichwa ni Dkt. Biteko Akutana na Menejiment ya NMB, ukiisoma
habari hiyo ni pongezi tu kwa Naibu Waziri Mkuu, kwa hakika huo mwezi Novemba
2023 pongezi kwa kiongozi huyo hazina maana yoyote kwa msomaji wa jarida la umma
,hapo kama kungekuwa na hoja ya mazungumzo ya maboresho ya NMB, kweli hoja hiyo
ingekuwa habari kwa umma wa Watanzania kwa jarida linalotoka kwa muda fulani, kidogo
pongezi zilikuwa na tija katika redio, runinga na magazeti yanarusha habari na matangazo
ya kila siku na siyo Nchi Yetu.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo atambue kuwa jarida hilo
ni la umma na hauwezi kuweka habari mbili za kiongozi mmoja , nchi hii ina
viongozi wengi, basi agejitahidi mtu mmoja habari moja na hata habari zenyewe zingekuwa
na uzito, huku siku hiyo hiyo na siku zilizotangulia kukiwa na habari tele
zenye uzito kutoka taasisi mbalimbali za umma.
Shida nyingine kubwa ipo katika matumizi ya picha, unapoyatazama
matumizi ya picha ya jarida hili, Rais hakuwa na habari yoyote zaidi yakutajwa tu
katika habari hizo na tena kidogo, kwa hiyo haikupaswa picha yake kutumika
kabisa kulitambulisha jarida hilo.
Picha za viongozi zimetumiwa sana, jarida hilo linapaswa
kusomwa na wananchi na kila kinachoonekana hapo kijenga dhana ya kueneza mazuri
ya serikali . Picha zote 12 ni picha mbili tu zenye nafuu na hata zenyewe
hazielezi sana mazuri ya serikali.
Katika matumizi hayo ya picha kunaonekana udhaifu mwingine wa
Mkurugenzi wa Idara hii kwa kuingiza picha yake katika jarida hilo.
“Jitahidi kuweka picha za kazi za umma na kupunguza picha za viongozi
ili kusaidia serikali iweze kusemewa kwa kina .”
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ajitahidi mno kwa kuwekeza
nguvu ya umahiri katika kufanya kazi katika idara hiyo. Umahiri huo utasaidia
sana kufanya kazi kwa ufanisi ili serikali yetu iweze kusemewa vizuri na kufikia
shabaha zake.
Mobhare Matingi atambue.
“Hatuwezi Kulenga Shabaha Namna Hiyo.”
Kinyume chake watu watasema,
“Idara ya habari ya Maelezo ivunjwe, alafu watumishi wa idara
hiyo, nusu waende TSN wale wenye ujuzi wa habari za magazeti kidogo na nusu
waende TBC wale wenye ujuzi wa utangazaji na ufundi mitambo. Alafu msemaji wa
serikali abaki Waziri wa Habari, atafutwe bingwa mmoja awe Waziri wa Habari na
Msemaji Mkuu wa Serikali, Hapo Mchezo Kwisha.”
Mwanakwetu anasema,
“Bado anautafuta umahiri wa Mobhare Matinyi katika tasnia
hii.”
Mwanakwetu Upo?
Hatuwezi Kulenga Shabaha Namna Hiyo
Waziri Habari Awe Msemaji Serikali
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
Post a Comment