Adeladius Makwega-MWANZA
Mwanakwetu siku ya Disemba 25, 2023 alitulia nyumbani kwake , hakwenda kusali misa ya Noeli ya Disemba 25, 2023 maana alisali mkesha Noeli hivyo alizaliwa pamoja na Bwana, maana Misa hiyo ilikuwa ndefu karibu saa 5 tangu saa 4 ya usiku wa Disemba 24 hadi saa 9 usiku hiyo ikiwa Disemba 25, 2023.
Siku nzima ya Noeli alikaa nyumbani kwake, labda kidogo alitoka kwake na kwenda kuchunga mifugo yake, jua lilipozama aliongea na simu na ndugu zake kadhaa, alafu akauchapa usingizi.
Asubuhi ya Disemba 26, 2023 Mwanakwetu aliwasiliana na mama mmoja ambaye alizungumza naye mambo kadhaa, likiwamo suala la Ukataji wa Mahindi ya Baadhi watu katika mradi mmoja hapa Malya.
Mama huyu akasema, Makwega ngoja nikusimulie kitu,
“Kuna wakati nilikuwa mtumishi wa huko Mbarali, Rais John Pombe Magufuli akatoa pesa za ujenzi wa Vituo vya Afya kadhaa , pesa ilipatikana kuna kata mojawapo ya hapo Mbarali ilinufaika na shilingi milioni 400. Pesa ilipopatikana walipokweda kwenye eneo la mradi, wakakuta walimu wa shule ya msingi kando, inayopakana na eneo hilo wamepanda mahindi, yamependeza vizuri. Viongozi wa Mbarali wa chama na serikali, wakalijadili jambo hilo kwa kina, makubaliano wakasema wafanye mazungumzo na walimu hao waliolima mahindi. Wakafunga safari hadi shuleni, kikaitishwa kikao, viongozi mbele, walimu wengi na baadhi ya wanakijiji wakakaa katika madawati , hapo mjadala ukaanza. Mwisho wakakubaliana kuwa walimu wapewe siku 30 wayavune mahindi yao, japokuwa yalikuwa hayajakauka. Hapo kikaoni mama mmoja ambaye alikuwa mwenyekiti wa UWT wa kata ya mradi huo akasimama akasema maneno haya,
’Walimu wangu poleni sana,(asante) natambua Mahindi yenu hayawezi kukauka vizuri katika siku 30, lakini mnayavuna kwa hoja moja tu ili sisi mradi ufanyike, milioni 400 zisipotelee mbali, nawaombeni yavuneni, yatoeni majani ya nje kadhaa, alafu kila hindi acheni majani manne yanayofunika hindi hilo, majani mawili yafunike hindi na mawili fungeni kamba yaning’inizeni katika kamba kama za kuanikia nguo au miti yatakauka vizuri. Huu ni mradi wa umma kwa ajili wananchi ambao ni sisi na nyinyi , kuliko mradi huu uondoke sehemu nyingine.’
Kweli baada ya siku 30 walimu hao waungwana wa Mbarali walishavuna mahindi wakayaanika kama alivyoelekeza Mwenyekiti wa UWT wa kata Kikaoni.”
Msimuliaji
huyu kwa njia ya simu alimwambia Mwanakwetu kuwa mahindi hayo yalikauka vizuri
na Hata Yeye Alikula Ugali wa Mahindi Hayo.
Kwani kisa hiki kinasimuliwa?
Viongozi wetu wawe makini sana wanapofanya kazi za umma, baadhi ya viongozi wanadhani mtumshi umma siyo mwananchi , hiyo dhana siyo sahihi , mtumishi wa umma ni mwananchi na ana haki na stahiki zote za raia wenzake, bali mtumishi wa umma yeye ni mwajibikaji katika baadhi ya mambo tu, ambapo dhana hilo mwneyekiti wa UWT kata huko Mbarali anaielewa vizuri.
Walioyakata mahindi ya wananchi Malya wamekosea sana, wanatakiwa kuwajibishwa mara moja.
Viongozi wa
Wizara ya Utamaduni tangu Waziri , Naibu Waziri , Katibu Mkuu na hata Naibu
Katibu Mkuu kwa ukweli wa Mungu leo hii Mwanakwetu anamuomba amsumbue Rais
Samia japokuwa pengine yupo katika mapumziko ya mwaka mpya, mama nakuomba wapigie simu kuwawuliza maswali mawili mosi,
“Huko Malya umepeleka mradi wa Bilioni 31 za watu wa Tanzania, ndugu
zetu, Je umeshawahi kufika?”
Majibu yatakayotolewa na kila mmoja , Rais yamuongozwe katika majukumu yake ya kila siku na suala hilo likiambatana na mahindi yaliyokatwa bila hata ya kuongea na wenye mazao hayo.
Ndani ya eneo hilo ambalo kulikuwa mazao yalifyekwa Disemba 24, 2023, kuna kaburi la miaka mingi ambalo wenye kabur hilo wameliwekea alama mbili; maandishi yaliwekwa katika ya kaburi likiwa ni jina la marehemu, pili kaburi hilo limezungushiwa mikonge kadhaa.
Mwanakwetu anamuomba mheshimwa Rais Samia, suala la pili la kuwauliza ndugu hao ni hili,
“Suala la malipo ya kaburi la MALOLE BUHORE
KATWANGA imeshalipa? Hata ndugu zake mnawafahamu? Je mmewatafuta?Je mnafahamu
kuwa kama kuna kaburi ndani ya mradi?”
Haya ni mambo madogo sana, kama mazungumzo yapo, kama kuna ujirani na kama kuna udugu kw hakika hauweze kuyakata mazao ya watu bila kuongea nao, hapo nakuomba msomaji wangu mkumbuke Mwenyekiti wa UWT kata huko Mbarali, hawezi kujenga mradi juu ya kaburi la mtu. Hawa walioharibiwa mazao yao na ndugu wa wenye kaburi wanaweza kwenda mahakamani na kuuwekea zuio mradi, Uongozi maana yake kuongea na watu, uongozi siyo ububu.Msaidieni Rais Samia ili baadaye watu wasimsimange hakufanya hiki na kile.
Nakuomba msomaji wangu niishie hapo.
Kumbuka tu,
Hata yeye Alikula Ugali wa
Mahindi Hayo
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
Post a Comment