Adeladius Makwega-MWANZA
Mwanzoni mwa mwaka 2023 Kanisa unaloliona hapo juu lilipata
mwanakondo (muumini) mgeni, walimkaribisha vizuri na kukaa naye, kanisa hilo ni
madhehebu ya Kisabato ambayo huwa wanasali siku ya Jumamosi.
Mwanakondoo huyu alikuwa ni mtumishi wa umma, alipokelewa
vizuri na kutambuliswa mbele ya wenzake na maisha ya kituo hicho kipya cha kazi
kuanza; kazini, nyumbani na kanisani.
Ndugu huyu alikaa na wenzake vizuri huku akishirki kutoa
michango ya imani yake kama miongozo ya dini ilivyo.
Mwanakwetu kwa hakika alivutiwa mno na maisha ya ndugu huyu
ya kiroho, akiwa mshika dini wa kweli, katika kufuatilia hilo kama mwanahbari Mwanakwetu
alibaini jambo,
“Kuna wakati baadhi ya
waamini wenzake walimuomba mchango na yeye kuwapatia mchango huo wa kiroho.
Ilikuweza kuupa nguvu mchango huo ndugu huyu aliomba eneo la kilimo kazini
kwake na kukubaliwa yeye na watumishi wenzake kadhaa wakapewa eneo kubwa karibu
ekari 20 na kulima mazao mbalimbali kama vile mahindi, karanga, maharagwe na choroko.
Ndugu huyu aliamua kulima shamba kama ekeri tatu na kupanda mazao kadhaa na
akajiuluiza yeye hapo hana familia, mazao hayo hata akivuna yatakuwa mengi ,
hivyo akaamua shamba hilo baada ya kupanda kuwakabidhi baadhi ya waamini
wenzake , wayapalilie vizuri alafu wakivuna wauze na watunishe mapato ya
kanisa.”
Mwanakwetu kila alipopita eneo hili alikutana na waamini wengi
wakilima kwa umoja kuyapalilia na palizo ya kwanza kwa shirika kila mmoja akiwa
na kipande chake, kazi hii ilifanyika vizuri na mahindi hayo kupendeza mno,
hadi Mwanakwetu akayaonea gere.
Wakati zoezi la kuyafyeka mahindi likiendelea
Mwanakwetu aliwauliza na majibu yao yalikuwa, yule tunasali
naye, mahindi haya tukivuna ni yetu, ametupatia. Mahindi hayo yakawa yanaendelea
vizuri .
Kumbuka hili eneo lililolimwa shamba ni eneo la taasisi ya
umma, Disemba 24, 2023 limetolewa agizo kuwa kuna kampuni ya Wachina inajenga
mradi , hivyo mahindi hayo karibu ekari 20 yakatwe mara moja, ili mradi huo uanze
mara moja.
Vijawa wakataji walipewa kazi, wakayafyeka yale mahindi yaliyokuwa
katika hatua tatu tofauti; baadhi yalihitaji majuma mawili kukomaa, baadhi yakiwa
yatafuta mbelewele na baadhi yakiwa yanahitaji palizi moja tu yatoe mbelewele,
hapo bila ya kutaja hali ya choroko, karanga , maharagwe , alizeti na mazao
mengine.
Mwanakwetu aliposogea eneo la tukio alikutana na zoezi
ufyekaji wa mahindi, hapo alikutana na taswira ya masikitiko makubwa.
“Jamani ulimwengu huu mnayafyeka mahindi ya watu! Mmeshindwa
kuzungumza nao?”
Mwanakwetu alijiuliza,
Kando ya eneo hilo palikuwa na kijana wa kiume kijana na mdogo
wake eneo lenye mazo yao lilikuwa ndilo
linafyekwa.
“Hawa jamaa wanakata
mahindi yetu, mama aliomba ruhusa kulima chuoni, akaruhusiwa , haya mahindi yangekutana
na siku 20 yangekomaa lakini wamekata, mama kapigiwa simu anakuja alikuwa
gulioni, mimi nimetangulia na mdogo wangu huyu mdogo. Wachina wanasema
tukiendelea kukaa hapa watatukamata.”
Hilo ni tukio la kusikitisha sana ambalo
Mwanakwetu ameliona kwa macho yake jumapili ya Disemba 24, 2023.
Umefyeka mahindi ya watu alafu unaruhusu trekta la mtu kubeba mahindi yaliyokatwa
Mwanakwetu anashauri yafutayo kwa
serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mosi, baadhi ya viongozi wamepewa
dhamana na Rais Samia Suluhu Hassan lakini dhamana
rais inaichezewa shere, mtu makini, muugwana, mstaarabu hawezi kuto ruhusa
ya kufyeka mahindi ya watu bila ya kuongea nao kwanza.
Huo mradi unaojengwa siyo mali yako
au mali ya familia yako bali ni mali ya hao hao waliopanda mahindi, zungumza
nao vizuri , malizana nao alafu endelea na mradi.
Aliyetoa agizo la kuyakata mahindi
hayo anaweza kuyapanda mahindi au mazao hayo yakaota ndani ya siku tatu na
yakafike hatua yalivyokuwa?
Iwe taasisi ya umma, iwe taasisi
binafsi inawajibu kwa kuwaheshimu wananchi na hata wafanyakazi wa ngazi za
chini.
Hali ya mahindi kabla ya kufyekwa
Swali ambalo Mwanakwetu anajiuliza
yupo kiongozi , awe mkuu wa taasisi, mkuu wa wilaya , katibu mkuu wa wizara yoyote
anaweza kuthubuti kuyakata mahindi ya wanakijiji ambapo rais anatoka/ anazaliwa?Yupo
kiongozi wa taasisi, wilaya au wizara anaweza kuyakata mahindi ya wazazi wake
kijijini bila kuzungumza nao?
“Tuheshimu wakubwa na
wadogo.”
Mwanakwetu anashauri suala hilo lichunguzwe
mara moja, viongozi waliohusika na tukio hilo wachukuliwe hatua mara moja,
kampuni ilivofanya hivyo na hata vijana walifanya uharibifu huo kwa maagizo ya
wakubwa wachukuliwe hatua na wakulima hao walipwe fidia ya uharibifu huo ikiwamo
waumini wa kanisa la Wasabato hapa Malya.
Mambo ya watu yajadliwe katika vikao
pawe na muhtasari mwisho wafikie uamuzi, inawezekana jambo hilo linafanywa
makusudi kwa sababu maalumu, lichunguzwe mara moja.Tanzania ni nchi ya watu wa
aina zote na hata miradi ni mali ya watu, ukiwa kiongozi wewe ni karani na
unafanya kazi hiyo kwa niaba ya watu, ndiyo maana likitokea lolote kwako
binafsi kazi inaendelea.
Nakukumbusha kuwaheshimu wakubwa na
wadogo.
Nakutakia siku njema.
0717649257
Shamba wazi baada yamahindi kufyekwa
Post a Comment