SAFINA NDANI YA SAFINA YA KWELI







 

Lucas Masunzu – MAKOLE

3. Ee Yesu, Mwokozi mpendwa, Wajua nalihifadhi

Tumaini la kukuona. La kukaribishwa nawe.

Ukija kwa watu wengine, Kama mhukumu wao,

Kwangu utakuwa rafiki, Nakesha, nakungojea.

 

WAKRISTO wapolimaliza kuimba kwa furaha ubeti wa wimbo 174 katika nyimbo za Kristo, uliotanguliwa na Fungu kuu 1Petro 3:20 walipokea ombi kutoka kwa Yusuph Andrew ambalo lilimnyanyua mzee wa kanisa Malugu Peter John akahudumu siku hiyo katika ibada takatifu iliyofanyika Jumamosi ya Disemba 23, 2023, katika kanisa la Waadventista Wasabato la Udom West Social, jijini Dodoma.

Katika ibada hiyo Mzee Malugu alisema kitabu cha Mwanzo kinaeleza vizuri maisha ya Nuhu jinsi alivyokuwa mtu mwema, mwenye haki, asiye na hatia mbele za Mungu. Utiifu na uaminifu wa Nuhu kwa Mungu ulifanya atii hata alipoagizwa na Mungu kujenga safina (Mwanzo 6:22; 7:5, 9; 8:18).

 

 

Nuhu alikuwa mwanadamu kama sisi lakini alikuwa mtu wa haki, mkamilifu tena aliyepata neema machoni pa Bwana. Katikati ya watu waovu, Nuhu alikuwa na mahusiano mema na Mungu wake. Nuhu alifanya kama vile Bwana alivyomwamuru. Swali kwetu leo tunafanya kama Bwana anavyotuelekeza kupitia maandiko matakifu?

 Baada ya safina kukamilika mvua ikanyesha juu ya nchi, siku arobaini mchana na usiku, kila chenye uhai juu ya nchi kilikufa isipokuwa juhudi ya Nuhu ilifanikiwa kuokoa watu wanane tu walioingia kwenye Safina (Mwanzo 7:7).

Mzee Malugu alisisitiza kuwa katika maisha yetu leo shule ya sabato ni safina ndani ya safina ya kweli ambalo ni kanisa la Mungu. Shule ya sabato ni kama safina inabeba watu mbalimbali, inakaribisha kila mtu kujifunza hata pale mshiriki anapopewa karipio shule ya sabato humkaribisha na kumkumbatia kwa upendo “karibu tujifunze”. Mtu anapoingia kwenye kikosi cha watu sita ndani ya shule ya sabato ni safina ndogo inayomuandaa kuingia katika safina ya kweli ambayo ni kanisa la Mungu. Kutokana na vikosi vilivyo katika shule ya sabato ni rahisi kujifunza pamoja, kutafutana hata pale uasi unapoibuka ni rahisi kuonekana kabla haujafikia hatua kubwa.

Hadi ibada hiyo inakamilia majira mchana hali ya hewa katika kanisa la Waadventista Wasabato la Udom West Social ilikuwa ni jua kiasi ambapo washiriki wa kanisa na waumini walitawanyika kwenda kupata mlo baadaye walirudi kanisani kuendelea na vipindi vya mchana.

Ubarikiwe, Nakutakia Siku Njema

0762665595

theheroluke23@gmail.com.

 

 


 

 

0/Post a Comment/Comments