Adeladius Makwega-MWANZA
Wakristo wameambiwa kuwa yako mengi ya kujifunza kwa Mama
Bikira Maria katika dominika ya nne ya majilio kwani japokuwa aliambiwa jambo
la ututanishi mkubwa alilipokea na kulikubali, kama yalivyo mapenzi ya Mungu .
Hayo yamesemwa na Padri Samson Masanja, Katika Kanisa la
Bikira Maria–Malkia wa Wamisionari Parokia ya Malya, Jimbo Kuu Katoliki la
Mwanza, katika misa ya kwanza ya dominika ya nne ya Majilio, Disemba 24, 2023.
“Kukubali kwake mpango wa mwenyezi Mungu ni ishara ya unyenyekevu,
ni ishara ya unyofu wa moyo na ni ishara
ya kujishushwa kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.”
Padri Masanja aliongeza kuwa agizo hilo la Malaika Gabrieli
kutoka kwa Mungu hata kama lingemfikia mtu wa leo lingekuwa jambo gumu na
pengine hali ingekuwa tofauti zaidi.
Padri Masanja alisema kuwa kwake Mungu hakuna
kinachoshindikana, mambo yote yawe magumu namna gani .yanakamilika.
Misa hiyyo pia iliambatana na nia na maombi kadhaa,
“Utasaidie kuzikipokea kazi na wajibu
ambazo umetukabidhi tuzitimize , ee Bwana - Twakuomba utusikie.”
Hadi misa hiyo imalizika
majira ya saa moja ya asubuhi, hali ya hewa ya Malya na viunga vyake ni mvua na
jua, sasa wakulima wakipandikiza mipunga yao kwa mabonde kwa juhudi kubwa
kutoka vitaluni.
Post a Comment