BAKORA UKUBWANI KUWAFUATILIA KARIBU

 



Adeladius Makwega-MWANZA

Kwa muda wa siku zaidi ya kumi, Mwanakwetu ameeleza kwa kina juu ya Kadhia hii ya Chuo Kikuu cha Dodoma na kwa hakika Mwanakwetu ametoa msimamo wake katika jambo hilo bila ya kuyatafuna maneno na jukumu lao wanaofanya maamuzi ni kuamua kama ilivyoshauriwa au kuamua  vinginevyo maana maamuzi ni yao.

Mwanakwetu katika hili anaomba kusema jambo moja kubwa, katika hao wanaofanya maamuzi kwa niaba yetu wasidhani wanaamua kwa ajili yao , wasidhani wanajiamulia wenyewe hilo abadani, maamuzi ni kwa ajili ya umma wa Watanzania.

Kila mfanya maamuzi popote alipo atambue kuwa,

“Inawezekana mtu akawa anampenda sana, anamuhusudu mno, akimuona mwili wake unasisimka, akiongea mapigo ya moyo wake yanaenda kasi, akitembea anapomtazama macho yake yanamkazia yeye na ayapepesi kando.

Sisi hayo umma si yetu , kumbuka tu kinachotukutanisha pamoja ni maslahi ya wengi, siyo upenzi, siyo husuda , siyo mapigo ya moyo kwenda kasi na siyo macho kutokupepesa kando na siyo nasaba na mtu huyo wa mtu yule.”

Panapokuwa na malalamiko katika taasisi fulani fulani, juu ya mtu fulani fulani, hiyo ni taa inayowaka, viongozi wengi wanayo dhana kuwa usalama wao katika nafasi hizo ni kwa kuwa wanyeyekevu kwa waliowapa nafasi tu, lakini wakiwapa mgongo umma ambao ndiyo mmiliki halali wa nafasi hizo.



Nakuomba msomaji wangu, kama kawaida ya Mwanakwetu nikupe mfano huu,

“Hivi sasa Tanzania suala la umeme kukatikakatika ni kero , ambayo bado haina majibu, kuna wakati taasisi moja ya umma umeme unaokatika ulisababisha kazi zisifanyike. Mara moja moja watumishi wa umma waliamua kuingia mifukoni mwao kununulia lita za mafuta ili kuliwasha jenerata la taasisi hiyo angalau kukamlisha kazi zao kwa wakati kulingana na ratiba ya mwaka.

Mwanakwetu hakuwauliza ndugu hawa kama walikuwa na bajeti ya mafuta ya dharula ofisini, lakini akajijibu hiyo dharula katika siku 31 inakuwa siku 28 maana yake umeme hakuna, hapo ni bajeti ya Jenereta tu.

Kwa bahati nzuri wakaguzi wa utekelezaji wa Ilani wakasema wanatembelea taasisi hiyo, Mwanakwetu siku hiyo Jenereta liliwashwa na mafuta yalipatikana siku nzima likiiunguruma.

Mwanakwetu kwa kuwa alivutiwa na ugeni huo wa CCM akasogea akasikia kusikia CCM wana nini? Muungurumo wa jenereta hilo ulimkaribisha Mwanakwetu na kwa mbali akisikia nyimbo za CCM kadhaa zikiimbwa.

Wimbo mmojawpao ulikuwa ni huu;

Eeee Vijanaaaa...

Vijana Vijana Vijana tayari

Kutumikia Taifa Taifa Taifa.

Kutumikia Taifa Taifa Tanzania.

Mwanakwetu anasubiria ugeni wa CCM waje kukagua utekelezaji wa Ilani, kwa ugeni unaopitia miradi kadhaa ya Wilaya hii, hivyo ulitumia muda mrefu, Mwanakwetu akiwa hapo aliamua kuchukua simu yake na kumpigaa rafiki yake wa utotoni waliokuwa wakicheza naye skauti na chipukizi, ndugu huyu anaitwa Ustadh Abdalah Momboga.

Akamwambia kaka nipo katika shughuli ya chama chetu wimbo wako wa ule Eee Vijana Vijana vijana Tayiri kutumikia Taifa Tanzania.

Wakati Mwanakwetu anayasema maneno hayo kwa mbali zinasikika sauti ya irabu na silabi Kiarabu Alifuuuu Beeee.  Teeee...

Ustadh Momboga ambaye mama yake ni Mzaramo wa Mwanadilatu na baba yake ni Mndamba wa Morogoro, wanafahamiana na Mwanakwetu tangu utoto  miaka 1979 mwishoni akasema maneno haya,

Nyie endeleeni kutumikia taifa, lakini mimi sasa namtumikia Mungu si unasikia darasa linaendelea?

Mwanakwetu akajibu ndiyo, Ustadh Momboga akasema, ‘ Kaka mabati ya madrasa yetu sasa yanavuja, tunaomba bati 20 ili mambo yawe safi.’ Mwanakwetu alijibu hakuna neno , baada ya sekunde kama 30 Wakaguzi wa Ilani, wakiwa na mashati ya kijani walifika na kukagua utekelezaji wa ilani yao na baadaye kwenda zao.”

Katika kisa hicho juu Jenereta linawasha ili kuwaonesha wenye ilani yao kuwa hapo hakuna shida. Mwanakwetu anasema viongozi wa CCM lazima waone hali halisi ilivyo hakuna kuwaficha, lazima waone maisha yenu halisi yalivyo.

Haya kudanganya na kuficha hali halisi ndiyo yale yale ya Profesa Lughano Kusiluka na Dkt Stergomena Tax katika kadhia ya Chuo KIkuu Dodoma.

Ukiwauliza hapo UDOM Vipi?

“Hapa mambo safi, kumbe siyo kweli , kumbe jahazi linazama.”

Naomba msomaji wangu nikupe mfano wa pili, mara baada ya makala yetu ya kwanza juu kadhia ya Chuo Kikuu Dodoma kutoka , Mwanakwetu alipokea simu na ujumbe kadhaa.

Mmojawapo ulikuwa huu,

“Unaandikaje makala ya uchunguzi, kwa kutumia picha tulizopiga wenzako, unatoa picha kwenya mtandao wetu bila kibali unazitumia unaita huo ni uandishi kweli?”

Ukisoma huo ujumbe unatoa picha kuwa umeandikwa na mtumishi wa Chuo Kikuu Dodoma mwenye taaluma ya habari, ambaye bado siyo mahiri katika taaluma hii, taaluma hii imemzidi kimo, anajaribu kuvaa viatu vya mchuchumio kujaribu kuifikia lakini hawezi. Haya mambo mama yetu ni ya nchani kabisa hauwezi kuyafikia hata kidogo hata ukijaribu kupande na kigoda utandondoka bure, pole sana namba yako ya simu ni 0713412871



Watumshi wote wa Chuo Kikuu Dodoma tangu Mkuu wa Chuo hicho hadi mtumishi wa kawaida wafahamu wao ni makarani wetu na wanafanya kazi kwa niaba ya Watanzania wote chuoni hapo, wanafanya kazi wote wa UDOM hamiliki kitu zaidi ya kuwekewa vitendea kazi ili muifanye vizuri kazi yetu na kazi ya Watanzania .

“Hilo kama hamlifahamu mljjue na ndiyo maana tunawasonta vidole hadharani na siyo upenuni .”

Kwa kifupi Mwanakwetu anasema hivi, wakati ujenzi wa Chuo Kikuu hapo Dodoma , kukiwa vichaka vichaka Chama cha Mapinduzi (CCM) kilifika hapo kufuatilia utekelezaji wa Ilani, wengi hamkuwepo, Waziri Mkuu wa wakati huo alikuwa ndugu Edward Lowassa, siku hiyo Mwanakwetu na yeye alipata  ngekewa ya kuwepo hapo.Ndugu Lowassa akasikiliza stori za kupindapinda juu ya barabara ya kufika hapo UDOM ohh kuna mlima, oooh lile.

Edward Lowassa akasema pasueni mlima huu na njia ipite hapa hapa, hiyo  ni njia hiyo mnayopita sasa na magari yenu,hiyo haikuwa njia ya kufika hapo. Mlima ukapasuliwa na njia ikawepo na njia ikawa fupi, siyo ile ya mzunguko sijui kutokea Nanenane na mizunguko kadhaa.

Kama Mwanakwetu anajua hata njia hiyo ilijengwaje, hivi kweli wahadhiri wanaweza kuwafelisha watoto wetu alafu wakabaki salama?

Nachotaka kusema nyinyi wasomi ili mfanye kazi vizuri lazima mfuatiliwe kwa karibu , wengi wasome wakubwa wa Tanzania hivi sasa walisoma zama zile za shule za kuchapwa viboko, kwa hiyo Viboko vya Ukubwani Kuwafuatiliwa Kwa Karibu tu.

Msomaji wangu usiogope na  sasa niutilie maanani mfano wa mwisho,

“Chuo Kikuu Dodoma kinatamani wanafunzi wote wa shahada ya juu wamalize masomo yao kwa wakati na muda stahiki. Wakuu wa Idara, Wasimamizi wa Utafiti waaswa kuwasaidia wanafunzi ili watimize ndoto zao.”

Profesa Razaki Lokina Mkuu wa Chuo UDOM Taaluma.

Huo ujumbe ni kutoka chuo Kikuu UDOM na ukiusoma huo ujumbe hauwezi kuwaelewa kama kweli hiki chuo chetu wako makini katika mambo yake. Hauwezi kusema unatamani,  kuhitimisha ni wajibu, kama hauitimishi maana yake wanachuo wasijiunge na chuo hicho! Kuhitimisha ni faladhi na siyo hisani na hilo halina mjadala.



Akina Edward Lowassa na nduguye Jakaya Kikwete wasingepoteza muda wao, rasilimali za umma kuhangaika kujenga majengo hayo kama hamuhitimishi wanachuo wenu.

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Wako ndugu zetu ambao ni hodari sana wa kuyapambani maslahi ya wachache, hawa ni ndugu zetu tunawapenda, tunazaliwa nao, tunakua nao, tunasali  nao hatupaswi kuwachukia ,tunaweza kuwapa majukumu mengine ambayo hayawagusi watu wengi.

Mwanakwetu anaiweka chini kalamu yake akisisitiza Profesa Lughano Kusiluka andolewa kwa manufaa ya umma na yeye Dkt Stergomena Tax afungashe virago vyake UDOM atuachie chuo chetu mapema.

Mwanakwetu Upo ?

Bakora Ukubwani Kuwafuatilia Karibu.

Nakutakia Siku Njema

makwadeladius@gmail.com

0717649257






0/Post a Comment/Comments