NIVUNJE KIKOMBE NISIVUNJE

 



Adeladius Makwega-MWANZA

Mwanakwetu bado anaedelea na kadhia ya Chuo Kikuu Dodoma, lakini siku ya leo kabla hajaizungumzia kadhia hii kwa kutoa mifano miwili, anaomba ayasema maneno haya kama ilani ya utangulizi ya makala za Mwanakwetu kwa wasomaji wake.

“Mama zetu waliopata bahati ya kuwa viongozi wana wajibu mkubwa wa kuyatazama maslahi ya wanyonge kwa karibu mno maana mama yoyote muda mwingi ndiyo huwa jirani na watoto tangu anatoka tumboni hadi anakuwa mtu mzima.

Akina mama wenye nafasi za utawala lazima watambue kuwa nafasi hizo haina maana kukalia kiti tu na kuyaacha mambo yaende namna yalivyokuwa kama zamani kama awali, hilo hapana. Akina mama hao wanapaswa kuwapambania wanyonge kufa na kupona . Kama watafanya hivyo hao wanyonge watatambua kuwa wanapambaniwa na akina mama hao, uongozi wao utakuwa na tija.

Katika kuwapambania wanawake wenzao, hao hao lazima kutaenda sambamba kuwapambania hata wanaume. Maana mapambano ya maslahi ya wanyonge wanawake, matokeo na faida zake hazina jinsia bali kwa wote wanawake kwa wanaume.”

Nakuomba msomaji wangu irudie hiyo ilani ya Mwanakwetu siku ya leo mara mbili mbli na kama wewe msomaji wangu ni kiongozi mwanamke irudie hiyo ilani mara tatu nakuomba kwa hisani yako fanya hivyo kwanza kabla ya yote.

Baada ya kufanya hivyo, sasa nakuomba nikutoa hapo ulipo msomaji wangu nikupeleke kule Chuo Kikuu Dodoma umbali wa karibu KM 700 kutoka Mwanza alipo muungwana Mwanakwetu.

Tambua kuwa KM 700 ni umbali mrefu sana lakini makala haya yanajaribu kukusafirisha katika viunga vya Chuo Kikuu hiki cha umma na maeneo mengine sawa na mtu anayecheza mchezo wa drafti kilagoni ambapo kuucheza mchezo huo Mwanakwetu mahiri.

Nia ikiwa ni kujenga dhana ya usawa kwa wote katika haki ya kupata elimu nchini Tanzania na wahusika wengine kutimiza wajibu wao ipasavyo katika uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali ya Tanzania.

Msomaji wangu soma kisa hiki,

“Ndugu mmoja aliamua kusoma shahada ya uzamili na chuo alichokichagua kilikuwa Dodoma, akajaza fomu zake na akachaguliwa kujiunga, kabla ya kutoka kazini kwake akalipa karo na pesa ya makazi , pesa ya makazi ikiwa 980,000/- shilingi za Kitanzania.

Baba wa watu akachukua barua ya ruhusa kazini kwake akashika njia kuelekea jijini Dodoma. Akaripoti chuoni hapo na akapangiwa bweni vizuri, akiwa hapo chuoni akayatazama mazingira yalikuwa yanavutia na alipata wasaa wa kuingia katika mifumo ya ya kuona wanachuo wanaoingia chuoni hapo na kuhitimu. Hapo taa nyekundu ikawaka akilini mwake mbona idadi ya wanaohitimu ndogo kuliko idadi ya wanaoingia kwa mwaka uliotangulia?

Ndugu huyu akapata mashaka makubwa, akamtafuta mjukuu wake anayesoma chuoni hapo, hakumpata, akauliza kundi la wanaosali Chuo Kikuu Dodoma kwa dhehebu lake la dini hakumpata.

Mzee huyu akarudi bwenini na wenzake watatu wote wa shahada ya uzamili. Wakajadili hii hali, wakasema jamani tukibakia hapa tunapoteza muda, tutafute Chuo Kikuu kingine.

Ndugu hao wakatafuta wakapata Chuo Kikuu cha Jordani na wkati huo dirisha la usajili lilikuwa bado halijafungwa, lakini lilikuwa ukingoni.

Wakaomba , wakakubaliwa, wakakusanya vitu vyao hapoa Udom- bwenini je wanafikaje huko wakiwa na mizigo? Mungu bahati miongoni mwao mmoja alikuwa na garik ubwa ikapakia mizigo hadi Morogoro. Wakafika huko wakapokelewa, hawa Jamaa wa Chuo Kikuu kingine walibaini kuwa ndugu hao awali waliisajiliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma, inakuwaje wanajiunga na chuo hiki?

Jamaa hawa wakahoji sana, lakini hawakuambiwa kisa ni nini? Miongoni mwa waulizaji aliyekuwa mjanja alijenga ujirani nao, baadaye alipata majibu ya kilichowaondoa Udom ilikuwa nini, huku wakisamehe na karo na pesa ya malazi kila mmoja, kumbuka -‘Kilichokwenda Kwa Mganga Hakirudi.’

Huyu mzee aliendelea kumtafuta mjukuu wake anayesoma Udom, baadaye alimpata na kumueleza kilichotokea.

Huyu mzee akamwambia mjukuu wake haya;

’Nilipokuwa nawasomesheni nyinyi sekondari, tulikuwa tunatafuta shule nzuri , baada ya Baraza la Mitihani la Taifa kutoa matokeo, shule yenye ufaulu mzuri, tuliwapeleka wanetu bila woga,nikiwa hapo Udom niipotazama mwenendo wa matokeo na wahitimu ya kila mwaka nilikwazika sana, nikaamua kuondoka zangu.’

Mzee huyu aliagana na mjukuu wake na kila mmoja kuendelea na masomo katika chuo chake.”

Msomaji wangu nikueleza juu ya babu na mjukuu wake hapo juu, sasa babu akaribia kuhitimu shahada yake ya uzamili lakini mjukuu wake aliyepo udom sasa ana miezi zaidi 36 katika kozi ya miezi 18.



Nyuma ya pazia baadhi ya watu wanasema Vyuo Vikuu binafsi ni money oriented, Mwanakwetu anakwambia Chuo Kikuu kama taasisi lazima kikusanye pesa ili kijiendeshe lakini lazima kitoe huduma yake kwa ufanisi. Hata kama Udom serikali inalipa mishahara , italipa mishahara pale Udom kama itaendelea kuwa wanachuo, yakibaki majengo matupo na kukakosekana wanaosoma  hapo, serikali haiwezi kulipa mishahara hiyo, na hilo halitakubalika kwa Watanzania hata kidogo, kwa hiyo chuo chochote kiwe cha umma ama binafsi lazima kitoe huduma bora na kwa wakati sahihi. Hao hao wahadhiri ndiyo wanasomesha Udom wanawasha magari yao kwenda Jordani na vyuo vingine binafsi kusomesha.

Hii nidhamu ya Vyu Vikuu binafsi tunaitaka iwepo katika Vyuo Vikuu vya umma.

Msomaji wangu nakuomba nikusimulie kisa kingine,

“Familia moja ilisomesha watoto wao vizuri wakifuata misimamo thabiti ya dini yao, binti mmoja akafanya vizuri kidato cha sita , akachaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dodoma, binti akafika hapo kuanza masomo.Akiwa masomoni, mhadhiri mmoja akanza kumsumbua binti wa watu kwa hili na lile ,huku na kule.

Mhadhiri huyu akawa anasema maneno mengi machafu-ashakumu si matusi– ‘Kwani ukinipa mimi mara moja kitaoza?’ Binti mdogo hayo mambo hayajui masikini wa Mungu, binti akachanganyikiwa , maji yakafika shingoni.

Binti akarudi nyumbani kwao akamwambia baba yake, ‘mzee mimi sitaki kuendelea na masomo.’ Ee mwangu umepata mume amekwambia hayo?. Binti akasema hapana, mazingira ya Chuo Kikuu cha Dodoma siyaelewi.

Mzee huyu muungwana sana, afisa mkubwa wa serikali, mzee wa Kisabato akamuuliza binti yake shida nini? Baba huyu kwa kuwa alikuwa jirani na familia yake binti huyu akasema moyoni ,

‘Je nivunje kikombe nisivunje-vunjaaa.’

Binti akavunja kikombe mbele ya baba nakutaja jina la mhadhiri.

‘Sasa nashindwa kusoma, pia anaweza kunifelisha, mwisho wa siku.’

Mzee huyu rafiki wa Mwanakwetu, mzee wa Kisabato akawambia bintiye baki nyumbani nalifanyia kazi.

Wakati huo huo Rais John Magufuli ndiyo anasisitiza ofisi za serikali zihamie, watumishi wa umma wanakimbizana kuhamia Dodoma. Baba huyu na yeye akahamishiwa Dodoma.

Mzee huyu akawa na mambo matatu ya kufanya awapigie watu wa utawala wa Chuo Kikuu Dodoma, ampigie Profeaa mmoja aliyesoma naye ambaye anafanya kazi Udom au  amtafute huyu mhadhiri uso kwa uso?

Maamuzi ya mzee huyu wa Kisabato aliamua kumtafauta huyu mhadhiri , lakini baadaye roho ya imani ilimjia akasema si vizuri bali ngoja nimpigie simu.

Akampigia simu akijitambulisha vizuri, ‘Hapo chuoni unapofanya kazi yupo binti yangu anasoma anaitwa Fulani bini Fulani, nimepokea malalamiko kuwa unamtaka binti yangu na maneno yako unayosema ya uchafu,ukome, usirudie tena. Nakuonya mara mwisho nikisikia lolote dhidi ya binti yangu nitaongea kwa vitendo, mwanangu hajakuja hapo kutafuta na kufunga ndoa,Udom siyo bomani.

Mhadhiri aliomba msamaha na alimtafuta binti huyu na kumuomba msamaha mara mbili mbili na binti kuendelea na masomo.”

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Kwenye utangulizi wa makala haya Mwanakwetu alizungumzia nafasi za akina mama waliopewa madarakani wana wajibu wa kuisadia jamiii ya Watanzania masikini kwa moyo wote na kujitoa kweli kweli hata kwa muda wao usiku na mchana.

Katika visa hivyo viwili vina wanachuo watatu waliosajiliwa na Chuo KIkuu cha Dodoma; yule aliyehamia Jordani na wenzake , yule anayesoma shahada ya uzamili kwa miezi 36-48 na huyu binti wa kisa cha mwisho cha nivunje kikombe nisivunje



Mkuu wa Chuo KIkuu Dodoma ni mwanamke Dkt. Stegomena Tax, Mwanakwetu anajiuliza huyu Dkt. Tax ameshawahi kuamua kukaa na mabinti wanaosoma hapo Dodoma waliofeli kabisa na kuongea kabla ya kuondoka chuoni nawaseme wanashida gani?

Kila baada ya matokeo Mkuu Wa Chuo unakaa na mabinti waliofeli unaongea nao, Je Dkt Tax ameshawahi kufanya hivyo? Dkt Tax jiulize hilo na Mungu wako alafu fanye maamuzi.

“Kama Dkt Tax angekaa na hao mabinti, kwa hakika angejifunza mengi na wahadhiri wangekuwa waoga, maana siri zao zingejulikana, hapo hapo hata wanachuo wavulana wangepata nafuu Chuo Kikuu Dodoma kingeenda vizuri, mabinti wanafeli wanazunguka mitaani wanapokelewa na mikono hatari ,hapa tunawapoteza akina Dkt Tax wengi wa kesho.”

Mwanakwetu anaendelea kusisitiza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dodoma Profesa Kusiluka aondolewe kwa manufaa ya umma nayeye Dkt Stegomena Tax abaki na majukumu ya kisiasa.

Mwanakwetu Upo

Kilichokwenda Kwa Mganga hakirudi au Nivunje Kikombe Nisivunje ”

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 



0/Post a Comment/Comments