JAMANI TUTHAMINIANE-KATEKISTA ANTONY

 



Adeladius Makwega-MWANZA

Wakristo wameambiwa kuwa wasijiangalie tu wao ni watu wa namna gani, bali wawe tayari kujuta makosa yao maana mwenyezi Mungu atasamehe maovu hayo.

Haya yamesemwa na Katekista Antony Ibrahimu Doto kutoka Parokia Malya-Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza katika ibada maalumu , mtaa wa Bikira Maria -Malkia wa Wamisionari, Januari 31,2024 wakati wa ibada maalumu iliyohudhuriwa na walei wa mitaa huo hapa Malya –Kwimba Mwanza.

“Mimi na wewe tunajikwaa, mimi na wewe funaangaika katika maovu, jamani Daudi anatufundisha tusiangalie tu sisi ni watu wa namna gani, tuwe tayari kutambua na kujutia maovu yetu.”

Akiendelea kuzungumza katika ibada hiyo Katekista huyu kijana alisema kuwa Wayahudi walishindwa kutambua mchango wa Kristo kwa kuwa walimzoea, hawakumthamini, nasi tusiwe kama wao, tunapaswa kuthaminiana.

“Unaweza kusema huyu si mwalimu tu , huyu selemala tu, Kristo anasisitiza tuthaminiane jamani.”

Katekista Antony alisema kuwa Wayahudi walitambua kuwa Yesu ni Selemala, hawezi kufanya miujiza yoyote, hakuwa kitu, ni fukara, walifikiri hivyo kwa kuwa miujiza kulihitaji ujuzi wa kusomea mazingaombwe huko Misri.

Wakijiuliza huyu selemala kapata wapi pesa za kujifunza na kununua mazingaombwe?

“Sote tunaalikwa leo hii kuthaminiana, kazi ya Mungu inatendeka katika kila nafsi, Mungu katupa talanta na kila mmoja na kipaji chake, wako walimu na wako walezi, tuthaminiane kwa kila mmoja kadili na kipawa chake.”

Ibada hii iliyohudhuliwa na viongozi kadhaa wa juu wa Parokia ya Malya, ilifanyika katika hali ya utulivu mkubwa na hali ya hewa ya Malya ilikuwa ya jua la kadili, huku siku hii hadi ibada inakamilika  saa moja ya usiku mvua hakuinyesha kabisa, japokuwa madimbi ya maji ya mvua zilizonyesa siku zilizotangulia yalipamba barabara nyingi za mitaa ya Malya na viunga vyake.

Madimbwi hayo yalipamba njia hizo na kuwa kama kioo, yakionesha taswira ya anga katika maji ya madimbi. Taswira hiyo ilionesha kana kwamba anga limehamishiwa katika madimbwi hayo kabla maji hayajatibuliwa, huku anga likiwa palepale na ardhi ikiwa palepale.

0/Post a Comment/Comments