HATUJUI KUNANINI KESHO

 



Adeladius Makwega-MWANZA

Msomaji wangu kumbuka bado Mwanakweu amekita kambi Chuo KIkuu Dodoma, japokuwa yeye yu KM 700 na kilipo Chuo Kikuu cha Dodoma.

Kwa bahati nzuri kadhia ya Chuo KiKuu cha Dodoma, sasa inabua malalamiko ya wanachuo wanaosoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) juu ya wao kucheleweshwa sana kuhitimu kutokana na sababu zisizo na msingi wowote kama yalivyo malalakimo haya ya Udom.

“Huu ni ugonjwa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hata UDOM imeambukizwa na wahadhiri waliotoka UDSM, baada ya kuhamishiwa hapo.”

Katika uchambuzi wa Mwanakwetu amebaini kuwa ugonjwa huu wa urasimu na katika kazi za tafiti za wanachuo kuwacheleweshea wanachuo unahamishiwa katika baadhi ya idara za serikali ambapo wapo wahadhiri wanaochukuliwa kutoka katika taasisi hizo za elimu ya juu na kuhamishiwa kusimamia idara za umma serikalini, sasa balaa linahamia huko lakini hili siyo mada ya leo.

Mwanachuo anayetoka familia masikini atapata wapi pesa za kumuhonga mhadhri? Wenye fedha, wenye nafasi wa umma serikalini kama vile ubunge na hata mawaziri wao wanasoma kwa wakati na kuhitimu.

“Kama wakimuona mwanachuo anakuja na V 8 wanamgombania kumsimamia utafiti, hata hao wenye vyeo wanagombaniwa sana kusimamiwa tafiti zao, ukifuatilia wao wanahitimu baada ya miezi 18 tu, baada ya muda uliyopangwa, hawakai muda mrefu, chuo hiki ni mali yao, hawa wakiwa na majukumu mengi makazini kwao. Mwanachuo aliyeomba ruhusa kazini, anakaa miaka mitano kisa anasoma shahada ya uzamili, mwenye nafasi anakaa muda mchache, hapo ndipo mwenye kutoa pesa haya, mwenye kutoa utu wake twende kazini ili kupata cheti.”

Mwanakwetu akasema sasa ndugu zetu wanaosoma UDOM itabidi tuwachukue V8 za serika au V8 zetuli tuzibadike namba za kawaida alafu waende nazo hapo Chuoni, tuweke mtego alafu kuwashikishe adabu.

Katika makala haya leo hii nakuomba msomaji wangu nikusimulie kisa cha kweli namna familia masikini zinavyoweza kupenya katika familia zenye mamlaka, familia tajiri , familia za kisomi na hata familia zenye mamlaka ya kisiasa.Koo masikini zinapenya bila ya kutarajiwa na zinaweza kubadilisha muelekeo wa mambo bila ya kutaka.

“Kuna wakati taifa la Liberia liliingia katika misukusuko mikubwa ambapo aliyekuwa Rais wa taifa hilo Charles Taylor alifikishwa katika mahakama ya kimataifa,huu ni ule wakati Fatou Bensoida ndiye alikuwa Mwendesha Mashtaka Mkuu.

Shauri hilo Mwanakwetu alilifuatilia mno tangu shauri linaanza hadi hukumu ,mwenendo wa shauri hilo ulirushwa na vyombo vya habari vya kimataifa. Mawakili wa Charaes Taylor walijenga dhana moja nzuri ambayo ilieleza namna Charles Nelson Taylor alivyozaliwa na namna maisha ya familia yake pande zote kwa baba na mama yalivyokuwa na mtazamo wake na maamuzi yake kama mtawala wa Liberia, namna ulivyokulia ina athari hasi na chanya katika maamuzi yako kama kiongozi.

Mahakama iliambiwa kuwa Baba wa Charles Taylor aliyefahamika kama Nelson Taylor alikuwa anazaliwa na jamii ya Waliberia waliohamia kutoka Marekani wakipata nafasi kubwa kubwa serikalini.

Mama yake Charles Taylor aliyefahamika kama Bernice Taylor alikuwa ni Mliberia wa asili ya taifa hilo kutoka kabila ya Gola.

Nelson na Bernice walikutana wapi hadi kuzaliwa kwa Charles Taylor?

Wazazi wa Nelson Taylor; babu zake walikuwa Wamarekani weusi, walikuwa ni familia bora, zenye fedha , zenye kipato, zenye nafasi hivyo walichukua binti wa kazi kutoka kabila la Gola ambalo ni asilimia kubwa (95% )ya Waliberia wote.

Binti akaja kufanya kazi kwa Baba wa Nelson Taylor(babu wa Charles Taylor). Wakiwa hapo Kijana mmoja ndani ya familia hiyo akampenda binti huyu kutoka kabila la Gola, akawa anatembea naye kwa siri. Mapenzi ya siri yakazaa matunda binti akapata ujauzito.

Ujauzito hauna siri, familia ikajua kuwa kuna uharibifu umefanyika ndani ya nyumba yao yaani Bernice ana ujauzito wa Nelson Taylor. Ndani ya koo hiyo yenye uwezo kukawa na mjadala mzito.

Jamani kweli mtoto wetu anazaa na binti wa machakani/binti wa madongo poromoka?

Babu wa Charles Taylor alikuwa Wakristo wenye misimamo mikali ya dini akasema maneno haya,

‘Kama umeweza kumgusa binti kutoka machakani, huyu binti wa madongo poromoka anafaa kuolewa, binti amefuvu kuwa mke wako hivyo bingi huyu amepata kibali cha Mungu kuolewa, hivyo naagiza mfungishwe ndoa mara moja.’

Bernice na Nelson wakafungishwa ndoa na hapo ndipo akazaliwa Charles Nelson Taylor ambaye alikuwa Rais Liberia.Hapo kule kuchanganya damu ya kabila la Gola( 95%) na damu hiyo ya Wamarekani weusi kulimsaidia kusoma shule nzuri, kupata elimu bora hadi kusoma Marekani na kushika nyadhifa kubwa.

Huyu Nelson Taylor yaani baba wa Charles Taylor aliwahi kuwa mwalimu na baadaye akawa Jaji nchini Liberia huku akihukumu kesi kadhaa.”

Nakuomba msomaji wangu twende taratibu na sasa turudi katika viunga vya Chuo Kikuu cha Dodoma.

Hapa kuna kijana mmoja, yeye anafanya utafiti wa shahada ya uzamili juu ya kabila ya Kikinga ile lugha yake namna ilivyo. Kijana huyu ni mkufunzi kutoka vyuo vya kati, aliamua aende hapo asome shahada hiyo ili angalau aweze kuongeza mshahara.

Udom alikutana na danadana za hapa na pale , alihangaika hadi TCU hakuna alichojibiwa mwendo ni danadana tu , maamuzi yake ya mwisho ilikuwa aende mahakamani.



Mwanakwetu alipolipata hilo ilibidi afuatilie kwa kina mambo mengi na maoajwapo ni elimu ya mhadhiri husika,

“Je anajua lolote juu ya Kikinga? “

Mhadhiri huyo alikuwa hajui lolote juu ya Kikinga na wala hajui lugha yoyote ya kabila la kibantu zaidi ya Kiswahili, lakini mwanachuo alikuwa anazungumza Kikinga vizuri, huyu mhadhri angetumia nafasi hiyo ya utafiti na yeye kujifunza kitu na kama angekuja mwanachuo mwingine kufanya utafiti wa lugha yaKikinga mhadhri huyo angekuwa mahiri maana njia anaijua.

Katika kesi nyingine ya binti mmoja yeye alieleza bayana kuwa amekaa Udom miaka mitano, kisa kuitafauta shahada ya uzamili amekusanya ushahidi kuwa hatendewi haki anakwenda mahakamani. Huyu binti mwanawake mwenzake Dkt Tax.

“Dkt Tax umekalia kiti, umefumbata mikono na umekunja na nne, hongera sana mama, lakini akinamama wenzako wanalia, wanashindwa hata kufumbata mikono, wala hawana hata wazo ya kukunja nne, wala hamu/tamaa ya kuwa jirani na wenza wao, wakiitafuta elimu kwa vita, sasa suluhu ikiwa mahakamani. Hongera sana Dkt Tax.”

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Yule kijana wa utafiti wa Kikinga, huyu binti anayekwenda mahakamani na wale wanaopata discontinue wengi wa shahada za kwanza hao wote ni kutoka familia maskini. Hawa ndugu wanarudi nyumbani wakiwa hawana vyeti.


Hawa wa shahada ya kwanza wakirudi majumbani wanafanya kazi kazi za kawaida na wachache mno wanasoma VETA na vyuo vya kati na wengine wanafanya kazi za ndani. Hao wanaofanya kazi za ndani, wanatambua lugha Kiingereza, wana akili ile iliyowasaidia kufaulu kidato cha nne na cha sita na hizi kazi za ndani wanazifanya kwa ufanisi mkubwa, hapo wanapiga hodi katika familia bora kama ile ya Babu wa Charles Taylor.

Natambua wasomaji wa Mwanakwetu ni watu makini sana na hadi hapo wamuuelewa,

Utasikia Watanzania wanasema,

“Mimi nataka kijana/binti wa kazi anayejitambua na anayetambua majukumu yake.”

Ndani ya kazi kazi za ndani yanatokea yale yale ya Nelson na Bernice na jawabu lake ni Charles Taylor .

Hizi familia bora zinakuwa hazina budi kutunza ujauzito ulitokea ambayo hiyo ni damu yao, inayounganishwa kwa nguvu, kwa lazima na hapo hta urithi unampa. Sasa huyu Bernice mlikaaje naye? Atamwambia nini mtoto wake huyu Charles Taylor? Mmefelisha chuoni , hana pesa ya chakula, maisha magumu na hana mtetezi.

Kikubwa ambacho kinasitizwa, wenye nafasi vyuo vikuu vyetu vya umma iwe UDSM au iwe UDOM sikilizeni watu, tendeni haki kwa wote bila kufanya ubaguzi wa chochote kile, toeni alama kwa haki.

“Hatujui Kunanini Kesho.”

Ndiyo maana Mwanakwetu anaendekea kusisitiza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Lughano Kusiluka aondolewa kwa manufaa ya umma na Dkt Stegemena Tax abakiziwe tu majukumu yake ya kisiasa .

Mwanakwetu upo?

Hatujui Kunanini Kesho.

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257





0/Post a Comment/Comments