Adeladius Makwega-MWANZA
Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimesema kuwa wanachama wa chama hiki kikongwe barani Afrika wanayo majukumu makubwa matano kuelekea uchaguzi wowote ule, ambayo yanapaswa kutekekezwa na kila mwanachama, popote alipo, iwe mwanachama wa kawaida au kiongozi.
Hayo yamesemwa na Katibu Muenezi CCM mkoa wa Mwanza ndugu Prudence Senipa wakati akizunguza na wanachama kadhaa wa CCM wa Mkoa huo Wilaya Kwimba, katika shughuli ya kuwapokea wanachama wapya 150 wa kata Malya.
“Kila Mwanachama anayo majukumu manne; Mosi , nyinyi na mimi pamoja ni
wapiga kura, CCM inategemeea tuwe wapiga kuwa wake. Pili nyinyi na mimi tuwe watafuta
kura za CCM popote tulipo. Tatu, nyinyi na mimi tunatakiwa kusimamia kura zetu wakati
wa kupiga kura. Nne, nyinyi na mimi tunatakiwa tuwe mstari wa mbele kuwatetea
viongozi wetu wanapotukanywa. Punde tukitimiza haya majukumu manne hakuna chochote
tunachodaiwa linabaki jukumu moja la viongozi , hili ni jukumu la kila kiongozi wetu kutimiza wajibu wake wa
kuleta maendeleo kwetu.”
Baada ya maelezo hayo kiongozi huyu wa CCM Mkoa wa Mwanza alimuagiza Kiongozi wa CCM Seneti Mkoa wa Mwanza ndugu Christian Kimaro kuwaongoza wanachama wapya kula kiapo na kurejea ahadi za mwanaccm, hapo hapo kila mwanachama mpya alinyanyua mkono wa kulia juu na mkono wa kushoto ukishika kadi yake na wengine mkono wa kushoto ukiwekwa kifuani.
Wakati zikisoma ahadi hizo za mwanaccm, ahadi moja ilirudia mara mbili,
“Nitasema Kweli Daina, Fitina Kwangu Mwiko. Nitasema Kweli Daima Fitina
Kwangu Mwiko”
Ahadi hiyo ilisomwa mara nne , mara mbili na mwenyekiti wa seneti na mara mbili na wanachama wapya.
Mwandishi wa ripoti hakufahamu kwanini Mwenyekiti wa CCM Seneti Mkoa wa Mwanza alifanya hivyo.
Mwisho wa kikao hicho alisimama Katibu Mwenezi Kata ya Malya Bi Hawa Salehe akasema amewapokea wanachama hao wapya katika kata yake, sasa wana haki ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa viongozi wa CCM, hivyo yeye ndiye mlezi wa matawi yote ya CCM kata hii na anatoa ahadi ya kutoa ushirikiano mzuri kwao.
Miongoni mwachama wapya waliokula kiapo ni Bi Consolata Mkwawa ambaue ni Kitukuu cha Chifu Mkwawa wa Lilinga, yeye alisema kuwa anatoa ahadi mbele ya Mungu na mbele ya umma huo kuwa atakuwa mwanachama muaminifu wa CCM maishani mwake .
.
Post a Comment