MEYA NA MKURUGENZI MTENDAJI

 



Adeladius Makwega-MWANZA

Unajua unapotaka kumfahamu mwalimu mzuri, kazi ya kumfahamu ni nyepesi sana maana kazi ya ualimu ni ulezi, mwalimu ni kiongozi , mwalimu ni mlenga shabaha, mwalimu ni mtoa muelekeo.

Katika ulezi na uongozi mwalimu husimama mbele katika kundi kwa idadi ya wanafunzi wake, liwe na wanafunzi 40, 80, 120 na hata 500 akiwaambia jamani sasa tunakwenda huku na kesho tutakwenda kule ili tufike paleeee...

Ukiondoka katika mandhari ya darasani unaweza kumfahamu mwalimu kupitia wale wanafunzi wake aliwasomesha katika vipindi cha ualimu wake kwa nyakati tofauti.

Kwa Vyuo Vikuu, wewe kama unatamani kujua mwenendo wa tabia ya mhadhiri kazi yake ni ndogo mno.Tafuta majina ya wanachuo wake kwa kipindi fulani aliowasimamia utafiti labda miaka sita nyuma ya 2024 ambayo ni 2023, 2022, 2021, 2020, 2019 na 2018 kila mwaka chukua wanafunzi watatu kwa miaka sita inakuwa kundi la wanafunzi wake 18.

Kwa namna ilivyokaa miaka hiyo unaweza kujipunguzia kazi kwa kuchukua miaka mitatu, hapo katika sita ruka mwaka mmoja mmoja. 2022, 202o na 2018. Katika kuchukua majina hayo na mika hiyo mitatu sasa utakuwa na wnachuo tisa wewe usitilie maanani kama mwanachuo huyo alihitimu au laa wewe chukua zigi zaga.

Kwa hawa wanachuo zungumza nao vizuri bila ya wao kujua nia yako kwa nyakati tafauti alafu omba ushahidi hata mawasiliano ya barua pepe, utastaajabu mengi, mno .

Twende taratibu msomaji wangu , haya ni mambo ya ngazi ngazi.

Mwanakwetu akiwa anasoma shahada ya uzamili, alisimamiwa andiko lake na Profesa Norman Adamson Sigala huyu msomi Mtanzania kutoka huko Njombe eneo leny baridi kali nchini Tanzania.

Mpaka kesho barua pepe ya Mwanakwetu inazo kumbukumbu za mawasiliano baina yao, na barua pepe ya Mwanakwetu ni hii,

“makw_adeladius @ yahoo.co .uk “

Ambao hawafahamu Dkt Norman Adamson Sigala zamani aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la Jmahuri ya Muungano la Tanzania na baadaye Mkuu wa Wilaya kadhaa.

Ukiyatazama mawasiliano baina ya Mwanakwetu na Dkt Norman Sigala wakati huo yaani 2009-2010 utafurahi mno yalikuwa mawasiliano ya kidugu.

“Wewe Bwana Mdogo, ebu maliza marekebisho yako, tuma kazi hiyo haraka , wiki ijayo sikukuu ya Krisimasi nataka kwenda Njombe.”

Prosefa anamwambia Mwanakwetu , naye Mwanakwetu anajibu,

“Dkt Sigala natuma, hapa namalizia marekebisho ya mwisho, kompyuta yangu ilizima gafla, nipo steshanari hadi saa kumi jioni ya leo utakuwa umepata.”

Mwanakwetu alipokuwa akiyasoma haya mawasiliano katika barua pepe hii ambayo siku hizi haitumii sana ameiweka kama kumbukumbu yake kuepusha kufuta baadhi ya mawasiliano aliyoyafanya wakati huo.

Katika hilo Mwanakwetu anaendelea kusisitiza Profesa Lughano Kusiluka aondolewa mara moja Umakamu Ukuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma,

“Watu wanapokulalamikia, hata unapoongea na vyombo vya habari ‘ohh maji ni kero UDOM’ wanachukia zaidi, maana umewakwaza, kwenye vyombo vya habari anapaswa kuonekana mtu ambaye hajawakwaza watu.”

Msomaji wangu tunakwenda ngazi kwa ngazi, nakuomba usichoke katika haya , maana kubwa na linalopigiwa kelele ni utoaji wa elimu ya juu nchini Tanzania kwa haki. Twende sasa katika kisa cha kwanza, kumbuka tu yale mawasiliano ya wakati huo baina ya Mwanakwetu na ya Dkt Norman Sigala ilikuwa ni kuujenga tu utangulizi wa makala haya.

“Katika Halmashauri moja walimu wawili walihangaika kuwekwa katika mpango wa masomo, kwa shahada ya uzamili. Baada ya miaka kadhaa waliwekwa katika mpango huo. Wakaomba Vyuo Vikuu na walimu hao wawili walipata Chuo Kikuu cha Dodoma. Wakapewa fomu za kujiunga na kuziweka katika mafaili yao ili kupata mikataba ya kwenda masomoni .

Mikataba ikajazwa vizuri kupitia kwa Afisa Elimu Sekondarii, ikatoka hapo na kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji ili iende kwa Meya/Mwenyekiti Halmashauri mkataba ukamilike.

Mikataba hiyo ilipofika kwa Mkurugenzi Mtendaji, akapitisha mikataba ya vyuo vikuu vingine vyote lakini ile ya UDOM alishituka , akiwa na rejea ya maombi ya walimu kadhaa wanasoma UDOM awali kutoka halimshauri hii kuomba kuongezewa muda. hakuipitisha akaiweka kando, akaibeba hadi kwa Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri.

‘Shikamoo mhe. Meya! Leo nina shida, hapa nina mikataba miwili ya walimu wanaojiunga na Chuo Kikuu cha Dodoma. Chuo hiki kina shida waliokwenda huko wanakaa muda mrefu, kwa hiyo walimu wetu hawa wawili tutawapoteza , watakwenda kupoteza muda wao bure, hivyo mimi sijapitisha kwa hoja hiyo , wanaweza wakaja kwako , nimekuja kwako  kukutaarifu mapema ili sisi sote/ mimi na wewe tuwe na uelewa wa pamoja. Naandika hapa katika stamp sticker kumjulisha Afisa Elimu Sekondari hawa walimu watafute Vyuo Vingine.’

Meya/Mwenyekiti wa Halmasahuri akaelewa vizuri , kwa bahati alikuwa msomi, Mkurugenzi Mtendaji akachukua stamp sticker mbili akaandika na kuzibandika kuelekeza hayo juu kwa Afisa Elimu Sekondari.

Walimu wote wanaokwenda masomo wakafika kuchukua mikataba yao waondoke masomoni, wamejiandaa na walipofika masijala wenzao wakapata mikataba yao, lakini hawa wawili, hawakuipata wakielekezwa kumuona Afisa Elimu Sekondari.

Walipofika huko mwanzoni hawakuelewa, hodi hadi kwa Meya/ Mwenyekiti wa Halimashauri hapo walipewa mifano ya walimu na majina yao waliokuwapo UDOM ambao walikuwa hawajahitimu, ndugu hawa wakawa wapole. Wakakubaliana hali hiyo  na wakati huo dirisha la usajiri vyuo vingine lilikuwa limefungwa, hivyo walikubaliana na Meya/ Mwenyekiti wa Halmashauri kuomba vyuo vingine mwaka uliofuata.

Msomaji wangu tazama kisa hicho, kumbuka tu unapompiga mtu, anaporudi kulia huwa anawaeleza nduguze , anapofanya hivyo nduguze wanatambua tabia yako, hivyo hawawezi kumleta ndugu mwingine apigwe kama yule ndugu wa mwanzo.



Mwanakwetu ndiyo maana anasisitiza lazima yafanyike mabadilko makubwa katika Chuo Kikuu Dodoma na Watanzania wajue yamefanyika ili kulinda uwekezaji mkubwa uliofanya na serikali lakini hilo liwe fundisho kwa vyuo vikuu vyote vya umma hasa hasa UDSM.

Nakuomba sasa tuhamie katika kisa cha pili.

“Kuna taasisi moja ya umma yenye idara kadhaa,i dara tatu za utambulisho, hapa idara mbili zilipata madaktari wa falsafa kutoka vyuo vikuu, kwa bahati mbaya wasomi watano hao wote walitoka Chuo Kikuu cha Dodoma.

Watu wakawa wanajiuliza, hivi wale wanaopanga hivyo hawezi kuona madhara ya kuchukua wakuu wa idara kutoka taasisi moja? Kama hao ndugu wakiwa wazuri Mungu bahati wanaweza kuivusha taasisi lakini vipi hawa ndugu wakiwa siyo, wanaweza kuivusha taasisi? Hapo wataizamisha kabisa,mjadala ukawa mkubwa.

Desturi ya Watanzania wengi wanayajadili mambo kama furaisha baraza tu, katika vikao vile rasmi hawasemi, wanakaa kimya, wanafanya hivyo kuogopa kukosa baadhi ya bakishishi kama vile safari , warsha, vikao na hata kuepuka kuhamishiwa machakani, maeneo magumu , madongo promoka.

Akija kiongozi mkubwa akalisemea hilo watalipigia makofi na kushangilia, eti sasa umepatikana mwarubani. Hiyo siyo tabia nzuri, na inaweze kutuzamisha siku tusiyoifahamu.”

Sasa nakuomba msomaji wangu kwa hisani yako usichoke na twende kwenye kisa cha mwisho kwa siku ya leo maana leo Mwanakwetu anakupa visa vitatu maana pengine Profesa Lughano Kusiluka na Dkt Stegomena Tax wakaelewa zaidi.

“Hapo hapo katika taasisi hii kulikuwa na kikao kinafanyika, wakaomba mwandishi wa habari aingie kikaoni, kikao kikafanyika vizuri huku kukihusisha idara kadhaa za umma.

Wasomi wale wale wa falasafa kutoka chuo hiki ni viongozi, na taasisi kikao kinaendelea huko hoja moja baada ya nyingine zikijadiliwa na kufungwa kwa kuwekewa maazimio.

Mwandishi wa habari wa taasisi kaalikwa yupo kazini , maagizo nyuma ya pazia habari za serikali ziandikwe msichelewa kuzisambaza. Kikaoni ikafika saa saba watu kwenda kula alafu wakarudi kikao kikaenda kama nusu saa, mwandishi akandika yale yaliyoazimiwa vizuri.

Habari ikasambaa vizuri, huku waziri mwenye dhamana, akapiga simu kuuliza mbona hiyo taarifa siifahamu? Waliopigiwa ni wale wakuu, badala ya kusema tumelijadili, tutakupa taarifa rasmi, wao wanasema mwandishi katoa mapema? Mmelijadili? Huyo kaandika mambo yake.

Waziri akaomba maelezo ya pande zote mbili, wakuu taasisi na mwandishi . Wakuu wanaruka kimanga, mwandishi kuukata mzima fitina akatoa nukuu zote za kikao akisema hata kama unataka sauti za mjadala wote nitakupa, mhe Waziri suala hilo nitakupa sauti la mjadala wote, hilo lilifunga pazia la mjadala hadi kesho waziri akaelewa.”

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

“Kwanza tusichukue wakuu wa taasisi moja au idara moja wengi kutoka taasisi moja ya elimu , hilo ni kosa kubwa , wanahama na yale madhaifu yao , wapo wenye uwezo lakini wachache.Hapo kunatengenezwa genge la kulinda madhaifu hayo na kulinda maslahi yao kufa na kupona. Kweli nirudi kufundisha tena? Kule Chuo Kikuu sina V8? Kule nitakosa posho hii na ile.

Hapa tujaribu kuchanganya watu kutoka kada tofauti wasiofahamiana ili kazi ziende na siyo kulinda maslahi binafsi.

Kwa mfano unatafuta viongozi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Tekinolojia , Naibu Katibu Mkuu unaweza kumchukua kapteni wa JWTZ akashika nafasi hiyo,

Katibu Mkuu unampa DCI Ramadhani Kingai, analo jina la utani zamani RPC Mnoko. Naibu Waziri ukamchukua mbunge ambaye ni Daktari wa Mifugo tu na Waziri wa Elimu akawa Mbunge ambaye amewahi kuwa mwalimu kafundisha kama Weruweru au Kilakala , Wizara  hii itasonga, haya mamboya UDOM na UDSM hayatokuwepo.”

Ukiutazama huo muungano hapo juu Kapteni a JWTZ, RPC Mnoko (DCI wa Sasa), Daktari wa Mifugo na Mwalimu wa Weruweru hao ni Watanzania ambao hawajawahi kukutana hata mara moja. Kitakachowakutanisha ni kazi na maslahi ya Watanzania wanyonge yatafikiwa.

“Mathalani mwanachuo alamlalamikia Profesa wa UDOM, akienda TCU anakutana na Profesa ambaye amemsimawa utafiti na Profesa huyu huyu wa UDOM, hapa mwanachuo anaenda Wizara ya Elimu anakutana Profesa Adolf Mkenda ambaye labda anafanya kazi ya miradi ya tafiti binafsi pamoja na huyu huyu Profesa wa UDOM hapo hatuwezi kujenga tutabomoa tu.”

Hawa wasomi wetu wanalindana sana kama kisa kile taasisi ya umma na ndiyo maana malalamiko mengi vyuo vikuu hayana majibu, matokeo yake ndiyo kile kisa cha Meya na Mkurugenzi Mtendaji.

Mwanakwetu anaendelea kusisitiza Profesa Lughano Kusiluka aondolewa kwa manufaa ya umma naye Dkt Stegemena Tax afungashe virago vyake UDOM na kwa huruma abakiziwe majukumu yake ya kisiasa hadi utakapofanyika uchaguzi wa 2025.

Mwanakwetu Upo?

Haya ni Meya na Mkurugenzi Mtendaji

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257




.

 

0/Post a Comment/Comments