POLISI WAFANYA OPARESHENI KAMATA WATOTO WA MITAANI

 



 Eliasa Ally Iringa


Jeshi la polisi mkoani Iringa limefanya oparesheni ya kukamata watoto wanao zulula mitaani katika eneo la kihesa kuanzia mida ya saa 12 jioni bila sababu za msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari mbele ya wazazi na watoto waliokamatwa mkuu wa upelelezi na makosa ya ya jinai ACP Issa Suleiman amesema "kuhusu oparesheni hii tulishasema na si mara moja na tumefanya mikutano ya polisi jamii,na katika watoto hawa wapo wazazi waliojitokeza kuwafata watoto wao na wapo ambao hawajaja mpaka sasa" alisema

Aidha Kamanda amewaonya wazazi na walezi kutowatuma watoto usiku kwani ni hatari akiwa peke ake huko huwezi jua atakutana na vitu gani, na kwa hi Leo tutawasamehe lakini kwa mara nyingine hatutowaacha tutawapeleka mahakamani.

Kwa upande wa Afisa ustawi wa jamii manispaa ya Iringa Tinaeli Mbaga, amesema jukumu la kumlinda kwa kumjibu wa sheria ya mtoto Namba 29 inaweka jukumu la Kwanza la kumlea mtoto ni mzazi hata hii oparesheni imefanyika ya kuwakamata wazazi na watoto.

"Na tunaamini kuwa kama mzazi atatimiza wajibu wake kwa mtoto basi tutapunguza matendo mengi ya ukatili wa kijinsia kwa watoto"

Na huko Manispaa ya Iringa
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa Ibrahim Ngwada amesema manispaa imepokea pesa nyingi kutoka Serikali kuu za kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 16 ya shule za Sekondari katika Manispaa hiyo. "

Alisema barabara ya muhimu kabisa ambayo watu wengi tulikuwa tunaililia barabara inayozunguka uwanja wetu wa Samora, kama ambavyo tunajua uwanja wa Samora ni moja kati ya kielelezo cha mji wetu wa Iringa kwasababu mikutano 

mikubwa, mchezo wa mpira wa Miguu timu zote kubwa zikija hapa Iringa zinacheza pale Samora lakini uwanja ule ule ulikuwa umezungukwa na vumbi" - Amesema Ibrahim Ngwada Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa. Mwisho 

0/Post a Comment/Comments