Na Eliasa
Ally Iringa
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), *Salim Abri Asas* amesema Serikali imefanya mambo mengi na kazi iliyobaki ni kuendelea kumshukuru Rais, *Dkt Samia Suluhu Hassan*.
Mnec amesema hayo wakati wa Sherehe za ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa kwa CCM, ambayo kwa Mkoa wa Iringa yamefanyika kijiji cha Ilambilole, Kata ya Kising'a, Wilayani Iringa.
"Rais anafanya kila kitu kwa nchi hii lakini wapo wakosoaji ambao hawaoni, mioyo yao haioni kabisa yaani kila CCM itakacho fanya wao ni kukosoa tu," amesema Mnec Asas na kuongeza;
"Hatuoni barabara zinajengwa? hatuoni majengo ya madarasa? hatuoni mbolea ya ruzuku? haya yote yanaoneka,"
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa, Comred Constantine KIHWELE amemtoa hofu MNEC kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu.
Kilele Cha miaka 46 ya kuzaliwa CCM kinatarajia kufanyika Februari, 2024 Manispaa ya Iringa.
Na Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kimetoa wito kwa watanzania kutumia fursa za uwekezaji zilizopo nchini na kusajili miradi yao.
Wito huo
umetolewa Leo na Meneja wa TIC kanda ya nyanda za juu kusini, Deusdedith
Hokororo alipotembelea kiwanda cha maziwa cha Shafa Agro kilichopo kijiji cha
Kidamali, kata ya Nzihi wilayani Iringa.
Akizungumza
baada ya kutembelea na kuona ufugaji wa ngombe na uzalishaji wa maziwa
unaofanywa na kampuni ya Shafa Agro inayomilikiwa na mwekezaji mzawa, Hokororo
amesema kuwa serikali ya awamu ya sita imeweka mkazo katika kuunga mkono
uwekezaji wa ndani.
"Hiki
tulichokiona hapa ndio mwelekeo wa serikali yetu katika kukuza uwekezaji hasa
wa wazawa ambapo tunawahimiza kusajili miradi yao TIC ili waweze kunufaika na
urahisi wa ufanyaji biashara kwa kutambulika na kituo cha uwekezaji
Tanzania", Amesema
Ameongeza
kuwa kutokana na umuhimu wa uwekezaji wa wazawa katika mnyoyoro wa uchumi wa
nchi, TIC imeweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wazawa ambapo inawasaidia
kuwaunganisha na taasisi nyingine za serikali kwa muda mfupi ili kurahisisha
mazingira ya ufanyaji biashara.
Hokororo
amesisitiza kuwa kituo cha uwekezaji Tanzania kinaendelea kuunga mkono maono ya
serikali ya awamu ya sita katika kukuza uwekezaji ambapo kimelenga hadi kufikia
mwishoni mwa mwaka huu kiwe kimesajili miradi 1000 kutoka 504 iliyokuwepo hadi
kufikia mwaka jana 2023.
Kwa upande
wake Meneja Uzalishaji na ubora wa Shafa Agro, Tumaini Fredrick amesema sera na
sheria rafiki za serikali zimesaidia kiwanda hicho cha maziwa kuanza uzalishaji
ndani ya muda mfupi ambapo sasa bidhaa zao zinauzwa nchi nzima.
Amesema
uwekezaji wa kiwanda hicho umetoa ajira 417 mpaka sasa pamoja na ajira za muda
zaidi ya 1000 katika kuzalisha maziwa na vyakula vya mifugo.
Kituo cha
uwekezaji Tanzania TIC kimefanya ziara katika kiwanda hicho ikiwa ni mwendelezo
wa kampeni yake ya kitaifa inayohamasisha uwekezaji wa ndani ambapo tayari
kimewafikia wawekezaji wazawa katika mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Geita,
Tabora, Dodoma,Singida, Arusha, Kilimanjaro, Shinyanga na Tanga.
Post a Comment