Adeladius
Makwega-MWANZA
Siku
ya Januari 26, 2024 ilianza kwa hali ya hewa ya jua, hakukuwa na mawingu, japokuwa
mwezi huo ulikuwa msimu wa mvua za masika hapa mkoani Mwanza.
Mwanakwetu
alitoka nyumbani kwake, begi lake mgongoni akielekea katika majukumu yake
ambayo siku hiyo yalifanyika katika eneo lenye umati mkubwa wa watu.
Mwanakwetu
akiuchapa mwendo, akitumia TZ NYAYO,
hatua kwa hatua, mara alisikia sauti ikiita.
“Baba,
Baba Baba, Mzee Mzee.”
Mwanakwetu alipogeuka tu, alikutana na sura na
kijana mmoja, aliyevaa sare za Shule ya Msingi, shati jeupe na kaptura ya rangi
ya khaki, chini akiwa amevaa yeboyebo za rangi ya uaridi akiwa amepanda
baiskeli.
“Mzee
umeangusha kitabu chako, pale juu, twende ukakichukue, mimi nilikuwa naenda
shule, nimeona wakati unadondosha .”
Kweli Mwanakwetu alirudi nyuma hadi
aliopoingusha kitabu hicho, akiwa na kijana huyu mdogo , kijana akaikota kumbe
ni shajara nyeusi na kumpa Mwanakwetu.
“Shajara hiyo ilikuwa ya mwaka 2024,
ilichomoka katika begi lake, ambalo hakulifunga zipu yake vizuri, ikiwa ndani
yake kuna nyaraka yake muhimu ya thamani.”
Mwanakwetu alimshukuru sana kijana huyu
aliyejitambulisha kama RENATUS EMMANUEL
mwanafunzi wa SHULE YA MSINGI MWANAGELE,
wilayani Maswa, mkoani Simiyu.
Kutokana na kitendo hicho Mwanakwetu
alijifunza Jiografia ya Kijiji cha Mwanegele, inaonesha kuwa kijiji hichi kinapakana
na Kijiji cha Malya Kilichopo Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza., ambapo hapo
awali MWANEGELE na Malya vyote vilikuwa vijiji vya Wilaya ya Kwimba mkoa wa
Mwanza.
Mwanakwetu alibaini kuwa kijiji hiki
kina shule za msingi nne na shule za sekondari mbili zinazohudumia wananchi wa
Kata ya Nyabubinza, huku watu wa Mwanegele na Malya wakishirikiana vizuri tangu
enzi.
“Hapa tuna zahanati yetu nzuri, tunapata
huduma vizuri , japokuwa awali wahudumu hawa wa afya walitusumbua lakini sasa
hali hiyo imebadilika, tunamshukuru Mungu”
Mwanakwetu alibaini kuwa kijiji hiki tangu
enzi ni cha wakulima na wafugaji, awali kulikuwa na wafugaji wengi lakini
ugonjwa SOTOKA ulihatarisha mifugo mingi na wafugaji wengi kuondoa katika eneo
hilo.
Changamoto cha kijiji hiki anachosoma
kijana Renatus Emmanuel ni
kutokuwepo kwa maji safi na salama, kijiji hiki kinacho mtandao wa mabomba na
chanzo cha maji lakini maji yanatoka mara hache haya wekwi dawa yoyote ile
kutoka bwawani yanatoka kama yalivyo.
Mwanakwetu siku ya leo anasema nini?
Kwa hakika kwa umri wa Mwanakwetu
amewahi kufanya kazi katika mazingira magumu sana na ya vijijini sana nchini
Tanzania kwa vipindi tofauti.
“Mathalani mwaka 2003-2009 aliwahi kuishi
Kijiji ch Ujamaa Isimani-Iringa Vijijini Mkoani Iringa, mazingira yake yalikuwa
magumu na upatikanaji wa maji ulikuwa kwa wiki maji ya bomba yalitoka mara
mbili, lakini kizuri maji hayo ambayo yalikuwa yanatoka mara mbili yalikuwa yanawekwa
dawa, haya ni ya mkoani Iringa.
Huu ni mwaka 2024 miaka ishirini baadaye, hali
ya maisha ya wanakijiji Cha Mwanegele ni gumu, japokuwa kuna mfumo wa maji
lakini maji hayawekwi dawa yoyote ile, hilo ni hatari kubwa kwa afya ya binadamu
na uhai wa maisha ya binadamu.
Shida ya Kijiji cha Mwanegele, hiyo hiyo ndiyo
shida ya Kijiji Cha Malya ambacho Mwanakwetu anaishi, Mamlaka husika zinatakiwa
kujitathimini kwa kuyaangalia maeneo ambayo yana miradi ya maji jamani wekeni
dawa.
Hii ni SIMIYU na MWANZA ya 2024 jirani na Ziwa
Victoria, Watanzania wanakunywa maji yasiyowekwa dawa? Ambayo hailingani na
hata IRINGA ya 2004? Vipi kipindupindu na magonjwa mengine ya tumbo kwa
wanavijiji hawa?”
Mwanakwetu
hamfahamu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu angeweza kuwambia neno lakini Mungu Bahati
anamfahamu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ndugu Amos Makalatangu akiwa UVCCM, Waziri Mdogo wa Michezo, wakati Mkuu wa Mkoa enzi ya Rais Magufuli, wakati ukuu wake wa Mkoa unatenguliwa na hata wakati anarudishwa Ukuu wa Mkoa na Rais Samia, namuonba ndugu yetu Amos Makala afuatilie suala la
maji katika kijiji cha Malya yatoke kwa wakati na maji hayo yawekwe dawa na viongozi
wa SIMIYU walitatue hilo la maji ya Kijiji cha Mwanegele.
Mwanakwetu upo?
Kumbuka MWANEGELE 2024 SIYO ISIMANI
2004
Nakutakia Kwaresma Njema.
0717649257
Post a Comment