KATIKA KRISTO SOTE NI SAWA -PADRI MSIGALA

 



Adeladius Makwega-DODOMA

Wakristo wameambiwa kuwa Pasaka ndiyo sikukuu kubwa kwa dini hii na watambue kuwa hata adhimisho la misa takatifu ya kila domnika ni adhimisho la Kipasaka na kwa Kristo hakuna aliye mkubwa wala mdogo, sote ni sawa.

“Hapa Kristo Mwanakondooo anapokea kifo kama sadaka kwa ajili ya dhambi zetu.”

Haya yamesemwa katika mahubiri ya Misa ya Alhamisi Kuu, Machi 28, 2024 na Padri Gidioni Msigala katika Kanisa la Bikira Maria-Imakulata, Parokia ya Chamwino Ikulu, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.

Padri Msigala alirejea na kuzitaja changamoto kadhaa ambazo taifa la lsrael walipitia huku Musa na Farao wakitunishiana misuli hadi Mungu alipoingilia kati.

“Musa anamuomba Mungu watu watoke, Mungu alimwambia Musa nenda kwa Farao lakini Farao hakutaka. Musa alipotoa nyoka naye Farao alikuja na nyoka wake.

Mungu akaamua watu hao watoke Misri na huko kutoka ndiyo Pasaka na ndiyo kutoka katika giza kwenda kwenye nuru.

Watu walipoambiwa watoke walikataa huku wakipewa masharti ya kula na kuchinja kondoo asiye na hila na jambo hilo ndiyo maana Ukristo unasisitizwa mara zote mtu asiwe na hila.

Adhimisho la Pasaka likaendelea hadi wakati wa Yesu pale alipoumega mkate.

“Yohane alieleza juu ya Ekarist Takatifu, Marko alifanya hivyo lakini Paulo amelisimulia hilo kwa msisitizo zaidi, maana adhimisho la Pasaka liliendelea hata kwa Wakristo wa Kwanza.

Kumbuka wakati huo hakukuwa na makanisa, walisali hekaluni na kuumega mkate majumbani mwao, jambo hilo likaibua mgawanyiko kwa familia zenye uwezo kuumega mkate pamoja na hilo likaleta shida na mgawanyiko na ndiyo maana Paulo anasisitiza kile kikombe tukinywewacho ni ushirika wa Kristo.”

Padri Msigala alisisitiza kuwa kwa Kristo hakuna aliye masikini wala tajiri, hakuna aliye mdogo waka mkubwa, kwake yeye wote ni sawa .


 

Hata taifa teule wakati wanakombolewa wote walikuwa sawa, mwenye kondo moja na mwenye kondoo 10,  wote walivuka pamoja na hivyo ndivyo ilivyo katika Kristo.

Katika misa hiyo Padri Msigala mara baada ya kusoma Injili aliwaosha miguu waamini kadhaa.

Misa hiyo pia iliambatana na nia na maombi kadhaa,

“Uwaite vijana wetu wawe na moyo wa Upadri ili tupate wahudumu wa Ekaristi -Eee Bwana-Twakuomba Utusikie.”

Hadi misa hiyo inamalizika majira ya saa moja ya usiku wa Machi 28, 2024 hali ya hewa ya eneo la Chamwino Ikulu ilikuwa na jua la kadili.


 

 

 

0/Post a Comment/Comments