Adeladius Makwega-MWANZA
“Mwana
wa pakaya! Siku inapita, bila ya kuona makala yako ya miaka 60 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar? Mbona nimesona makala kadhaa zenye maudhui mengine?
Mwanakwetu anaulizwa maswali
hayo mawili yaliyomo katika jozi moja ya maswali pacha inayohitaji majibu yake.
Mwanakwetu alipokea jozi
hiyo ya maswali, kwanza aliyatuliza gambani mithlili Michael Platine, alafu
akaja na kicheko. Ndugu huyu muuliza jozi ya maswali alihoji kicheko hicho cha
Mwanakwetu.
“Kwani ninasema uwongo? Leo ni Aprili
26, 2024, ukihesabu tangu Aprili 26, 1964 hadi leo ni miaka 60, hayo makumi
sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sasa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina
mvi na uwalaza juu yake.”
Mwanakwetu alijibu kwa utani
kuwa sasa Jamhuri imevaa wigi. Jamaa akacheka sana.
Mwanakwetu akaongeza maneno
haya,
“Natambua hizo kumi sita
lakini nilijipa nafasi ya kusoma makala za waandishi wengine, mimi sina la
kusema.”
Ndugu huyu akauliza maoni ya
Mwanakwetu yakoje kwa miaka hiyo 60 ya taifa lake? Kutokosa la kusema kwa Mwanakwetu
ni kukosa uzalendo , Mwanakwetu aliambiwa.
Hapa Mwanakwetu alicheka
sana alafu alimsimulia ndugu huyu visa viwili baina ya Watanganyika na
Wazanzibari.
“Kuna wakati hawa tunaodai ni Watanzania walikuwa wanafanya kazi nje
ya nchi, katika taasisi hiyo waliyokuwa wanahudumu, hawa Wazanzibari walikuwa
wengi huku Watanganyika walikuwa wachache, makadili yalikuwa ni 10 kwa 3.
Hawa Wanzanzibari mwenyezi Mungu aliwajalia
walikuwa ndiyo washika usukani wa taasisi hii huku wakiunyonga vilivyo nao
Watanganyika ndiyo utingo huko huko ughaibuni.Mzungu akawaamini hawa Watanzania
kutoka upande wa visiwani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika taasisi hiyo walikuwepo raia
kadhaa wa mataifa ya Afrika kama vile Kongo, Kenya, Rwanda, Burundi, Komoro,
Madagaska ,Uganda na Somalia Kwa hakika idadi ya Watanzania ilikuwa kubwa
watumishi zaidi ya 13 huku haya mataifa ya Afrika yakidonoa nafasi ya mtumishi
kati ya 1-3.Huku mataifa mengine yakiambulia sufuri. Hawa Watanzania wakaanza
kubaguana huyu anatoka Zanzibar anapewa ajira huyu anayetoka Kilimanjaro
anapigwa mkasi. Ikawa heri ajira apate raia kutoka mataifa mengine kuliko Mtanzania
mwenzao. Jambo hilo lilikuwa linalalamikiwa kwa siri kwa maneno ya hapa na pale
lakini hali ilikuwa hivyo hivyo.Watanzania wanashitakiana ‘Ohh huyu kaukana
uraia lakini bado anamiliki nyumba Pemba na Tanga.Waswahili wanasema, ‘Mwana akiwa na Kidonda Mjukuu huwa na
kovu.’ Mwisho wa siku nafasi zote juu zikajazwa na raia wa mataifa mengine
ya kando ya Tanzania.Hawa raia wa mataifa kando ya Tanzania wanasema waziwazi ‘Watanzania wana mambo yao ya zamani, bado
wameyabeba moyoni, nafasi hizi zilikuwa zao ngoja sasa tuwatawale. Wanatumia
kibali cha kusafiria kimoja lakini hawaelewani, ngoja wagombani na wakiwa huko chini
na waumizane vizuri.’
Hoja siyo tu ya
Mtanganyika na Mzanzibari bali hata ya Muunguja na Mpemba .
‘Wanadai kuwa huyu Mpemba anafungua
barua zao katika pigion Box zao, wamefikia hadi kiapo kwa kuapa kwa kuipiga
chini tasbihi, hawa ni ndugu na tena wa dini moja, Watanzania Pendaneni Jamani.
Mpo
Ugenini.’
”
Jamaa akauliza kwa hiyo mchezo
ukaishaje?Mwanakwetu akajibu kuwa ndivyo hivyo Ufalme Umehamia Kwingine. Huyo Mpemba tena alikuwa ameoa mama wa
Kindengereko, chuki tele,huku Waafrika
wenzao wameshauchukua ufalme, kurudi majaliwa. Jamaa huyu akamuuliza Mwanakwetu
sasa hapa shida ipo wapi? Mwanakwetu akajibu kuwa kosa ni la Mwalimu Nyerere,
“Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
tumeungana, huyo kapoteza vyote huyu kapoteza kidogo, hapo ndipo Nyerere alipobugi(alipotea).Tulitakiwa
kama kupoteza tunapoteza wote alafu tunaungana.Kama wewe tunaungana na mimi
ukibaki na chee na mimi nabaki na chee.
Mwanakwetu akamuongozea
ndugu huyu kisa cha pili;
“Kuna
jamaa alikuwa anasafiri kutoka Mwanza kuelekea Tanga, hivyo alipanda basi hadi
Arusha Mjini, siku hiyo basi hilo lilikuwa bovu lakini saa tano ya usiku
walifika Arusha Mjini. Walipofika Arusha tu akapanda coaster hadi Moshi usiku huo huo
maana alikuwa anawahi shughuli ya Komuniyo ya mtoto wake, hivyo usiku huo saa
saba na ushehe alikuwa Stendi Kuu Moshi Mjini, jamaa alikaa saa kadhaa
akashauriwa kama anakweda Tanga apande boda boda hadi Njiapanda ya Himo hapo hapo
akakata shauri na kupanda bodaboda kwa shilingi 10,000/=akabebwa hadi Njiapanda
ya Himo,
kama
saa tisa kasoro ya Alfajiri alipofika hapo Njiapanda ya Himo tu akapanda lori
ambalo lilikuwa limetoka kushusha saruji na kuomba alipe shilingi 12,000/= hadi
Mombo akakubaliwa akaingia mbele ya kichwa cha lori hilo kubwa na kukaa nyuma
ya kiti cha dereva huku akiambia vua viatu ili asiachafue kiti hicho maana ni
kitanda cha dereva safarini, pale dereva akichoka huwa anapumzika.
Ndani
ya lori hilo kubwa la mizigo kulikuwa na watu watano dereva mmoja, utingo mmoja
na abiria watatu wanawake wawili na mwanaume mmoja.
Dereva
wa Lori hilo ambalo ni mali ya kampuni ya saruji akawa anaongea na utingo wake,
‘Hii
Safari tumebahatisha, tunarudi kiwandani, unajua sina hakika kama tutapata tena
safari ndefu kama hii ya kuleta saruji huku maana safari zilizopo ni kubeba
saruji kutoka kiwandani kwenda bandarini- hizo ni safari fupi, kwa muda mrefu kazi
ni hiyo kwani ile saruji inayokwenda Zanzibar, huko wanajenga nini? Saruji ni
nyingi wana mradi gani mkubwa?
Safari
hizi ndefu ndiyo zina pesa bwana, tuombe Mungu tupate safari ndefu.”
Mjadala
ukawa mrefu na safari inaendelea, sasa hawa akina mama, mmoja alishuka kati ya
Himo na Mwanga na pili kati ya Same na Makanya–Hedaru. Kumbuka msomaji wangu
anayesimulia hilo yeye ni miongoni mwa abiria anayeshuka Mombo. Awali huyu
anayesimulia aliwauliza wale waliokuwamo katika lori ni wenyeji wa mikoa gani?
“Dereva alijibu kuwa yeye anatokea
Mtwara, Utingo Kilimanjaro hawa akina mama wawili ni wenyeji wa Tanga na huyu abiria
mshuka Mombo ni wa Morogoro.”
Wa Mombo alipofika tu alishuka
huku hawa jamaa wakaendelea na safari yao na kilichoendelea kwa dereva na
utingo wa lori hilo la saruji huko kiwandani kama walipata safari ndefu au
waliendelea na safari za Kiwandani Forodhani, huyu aliyesimulia hafahamu hilo
bali anakumbuka hiyo ilikuwa mwanzoni mwa Augosti ya 2023.
Mwanakwetu anasema nini siku
ya leo?
Hivi, inakuwaje hawa watumishi
lori la kiwanda cha saruji wanauliza kunajenga nini huko Zanzibar? Na kwanini
hawahoji hii saruji iliyobebwa na wao wenyewe na kuipeleka mkoani Kilimanjaro
ambao ni umbali mrefu kutoka kiwanda kikubwa cha saruji? Msomaji wangu majibu
yake ni mengi;
“Kwanza wanapenda safari ndefu zinaposho
tele na pili kwa sasa mtawala wa hii nchi anatokea Zanzibar (Wanasema huko
kunajengwa nini?)
Ndugu hawa bila ya kujua huko Zanzibar
pengine hata Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar pengine ina miradi yake
inayohitaji saruji tele kutoka bara na pengine wananunua huko kiwandani au kuna
kampuni ia mrdai mkubwa inaujenga huko Zanzibar.”
Kwa hakika visa vyote viwili
vinatoa taswira ya huo muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulivyo na jamii
haziaminiani.Wananchi kwa wananchi na hata wananchi kwa viongozi. Je nani anapaswa
kuutetea muungano huu? Je ni maziara ya Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume? Je ni maziara
ya wale walioshuhudia muungano huu?Je Viongozi walipo madarakani peke yao?Je ni
hiyo katiba na sheria za nchi hii? Je mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Je ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Je ni vyombo vya ulinzi na usalama?
Mwanakwetu mtetezi halisi na
wakweli wa muungano huu ni kila Mtanzania ambao ni mimi wewe, kubwa viongozi wetu
watoe muelekeo wa kurekebisa makosa ya Julius Nyerere na majibu yake ni Katiba
Mpya na maamuzi ni mawili tu kama wakurudishiwa arudishiwe na kama wa kupoteza
apoteze .
Mwanakwetu Upo?
Kumbuka tu msomaji wangu,
“Muungano
huu ni wa walio hai, hauwezi Kutetewa na waliolala maziarana Mimi na wewe Watetezi Muungano.”
Nakutakia
siku njema.
0717649257
NB Maana ya neno Ziara ni Kaburi
Post a Comment