Adeladius
Makwega-MWANZA
“Mimi ni mzabibu- nyinyi ni matawi yangu,
akaaye ndani yangu -nami ndani yake, huyo huzaa sana. Ndugu zangu wapendwa tunaadhimisha
jumapili ya Tano ya Pasaka tunaalikwa kukutana na Kristo, tunaalikwa kuonana na
Kristo, maana Pasipo yeye sisi hatuwezi kufanya lolote pasipo yeye sisi
hatuwezi kuzaa matunda bora, pasipo yeye hatuwezi kuwa na faida kwetu wenyewe na
hata kwa watu wengine.”
Hayo
ni maneno ya utangulizi ya mahubiri ya Padri Samson Masanja mara baada ya kuisoma
injili ya Dominika yaTano ya Pasaka, katika Kanisa la Bikira Maria-Malkia wa Wamisionari-Parokia
ya Malya -Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Aprili 28, 2024 .
Padri
Masanja alisema kuwa Kristo ambaye ni Mzabibu wa Kweli wakati sisi ni matawi
yake na kila Mkristo anatakiwa kuishi katika muunganiko huo., alisisitiza kuwa kama
sisi ambao ni matawi yake kama tutaruhusu muungano huo kuvunjwa basi tutatupwa
motoni, alirejea maisha ya Sauli mara baada ya kumpokea Kristo alifanya kazi
yake vizuri huku akiwa tayari kwa mapambano kwa ajili ya Kiristo ambapo awali
Sauli huyo huyo alilihangaisha Kanisa la Kwanza,
“Paulo anabadilika kabisa nakuwa kiumbe
kipya na kufanya kazi ya Kristo na hata mitume wanapomuona wanamtilia shaka
maana wanazijua kazi zake zote alizozifaya.Upya wa Saulo unakuja baada
kuunganika na Kristo.”
Hapa mitume bado wanamashaka
hadi Barnaba anaingilia kati kwa kuwaambia mitume mpokeeni.Hata katika maisha
yetu tunafundishwa kuamini katika mabadiliko ya wenzetu.
Barnaba anasisitiza,
“Huyu
siye Sauli aliyewauwa Wakristo bali huyu ndiye Sauli anayemtangaza Kristo.”
Tukubali mabadilko katika
maisha ya wenzetu na uwezekano wa kubadilika ni wa Bwana.Padri Masanja aliongeza
kuwa ni jambo gumu kuamini katika mabadiliko ya wenzetu kama ilivyokuwa kwa
mitume,
“Unaishi na mtu mwongo kwa miaka kadhaa,
unaishi na mtu mwizi kwa miaka kadhaa alafu unamuona amebadilika, hilo linakuwa
gumu, nawaomba tuamini katika mabadiliko hayo ya wenzetu.”
Padri Masanja aliufunga
ukurasa wa mahubiri yake kwa kusema kuwa hivyo ndivyo Kristo anavyotufundisha kuzifanya
kazi zake ambapo anatutaka sisi kuzaa matunda mema,
“Matendo mema yanatokana na imani yetu
iliyo thabiti, imani yetu iliyo imara kwa hiyo tutazaa matunda bora”
Misa
hiyo pia iliambatana na nia na maombi kadhaa,
“Ulisema kwamba yule asiye kaa ndani
yako, huyo atatupwa nje na kunyauka, utuimarishwe tusinaswe na kishawishi cha kujitenga
nawe –Eee Bwana Twakuomba Utusikie.”
Kwa
hakika hadi misa hiyo ya kwanza iliyoanza saa kumi na mbili inakamilika saa
moja ya unusu ya asubuhi, hali ya hewa ya Malya Wilaya Kwimba umbali wa karibu KM
120 kutoka lilipo Jiji la Mwanza ni jua la kadili, mandhari ya chanikiwiti kila
kona nako huko mabaweni(mabondeni) wakulima wakivuna mipunga yao.
Post a Comment