Adeladius Makwega -MWANZA
Novemba 8, 2021 Mwanakwetu
alikuwepo katika Kijiji cha Ujamaa Ikangao Ulanga Mkoani Morogoro kushiriki
maziko ya babu yake mdogo aliyefahamika kama Otimali Makwega Kazimbaya, Kijiji
cha Ikangao kilikuwa hakina umeme hivyo alitoka zake hapo hadi Tarafani Mwaya
ili aweze kufanya kazi zake kadhaa katika mitandao pesa na simu.
Maana Kitogoji cha Mrundu na
eneo lote la Ikangao hata mtandao wa simu kupatikana ilikuwa tabu.
Akiwa hapo Mwaya ,
Mwanakwetu aliyaandika makala haya,
Wilaya ya Lushoto wakati huo
ilikuwa ikiundwa na Halmashauri mbili nazo ni Lushoto na Bumbuli, huku Lushoto
ikiwa ndiyo wilaya katika mwamvuli wa Halmashauri mbili ndugu , Halmashauri ya
Lushoto ikiwa na majimbo mawili Lushoto na Mlalo.Nalo jimbo la Bumbuli likiwa
na Halmashauri hiyo hiyo ya Bumbuli.
Kwa kukadilia Halmashauri ya
Lushoto ilikuwa na watumishi wa umma wenye ajira za kudumu zaidi ya 3500 kutoka
idara zote.Katika makala hayo Mwanakwetu aliyanukuu maneno haya kutoka kwake
Binafsi,
“Nikiwa na athari ya Uongozi wa Vyama
vya Wafanyakazi kutoka Shirika la Utangazaji la Tanzania maana hapo nilipokuwa
Mwenyekiti wa Wafanyakazi. Unapokuwa mwenyekiti wa wafanyakazi kubwa lilikuwa
nikupigia kelele maslahi na posho za watumishi kila mfanyakazi apate kwa usawa.
Kila safari iliyokuwa hapa TBC wakati huo zilikuwa ni kwenda Bungeni Dodoma
kutayarisha Vipindi vya Leo Katika Bunge,
Maswali a Majibu Bungeni, Mijadala Bungeni na Matangazo ya Moja kwa Moja ya Bunge kabla ya huyu huyu Nape Nnauye(Waziri)
kusitisha matangazo ya Bunge Live
kwa madai kuwa yalikuwa ya gharama kubwa kwa TBC kuyarusha moja kwa moja.
Kwa hiiyo nilipofika Halmashuari ya
Lushoto nikiwa bado nina mawazo ya kuhakikisha posho zinatolewa kwa uwiano wa
wote na kwa usawa angalau kuonesha kuwa kilichopo kinatolewa kwa wote.”
Mwanakwetu yu Mwaya Ulanga
mkoani Morogoro hiyo ni Novemba 2021 kama nilivyokujulisha, aliendelea
kusimulia matukio yq kweli kati ya 2016-2019 LUSHOTO-TANGA na MBOZI-SO.NGWE
“Kuna kijana mmoja ambaye ninamkumbuka
kwa jina moja la Japhert, akiwa ni Afisa Utumishi na Rasilimalia Watu wa Halmashauri
hii ya Lushoto akiwa na cheo kidogo sana niliongea naye juu ya namna ya kutoa
angalau bakishishi/posho kwa watumishi kila wakati wa sikukuu.
Jambo hlo aliniambia kuwa ni gumu sana
lakini nilijaribu kushauriana naye tukiwa wawili juu ya namna ya kuweza kutoa
bakishishi hiyo ambayo ingekuwa kama motisha kwa watumishi. Nilizungumza naye
mengi nikimwambia kuwa ‘Haya mapato
tunayosema tumekusanya kumbuka wanaofanya kazi hiyo ni watumishi wa ngazi ya
chini kabisa, kuna wajibu wakuhakikisha angalau hata kila sikukuu wao watumishi
wa ngazi ya chini kuweza kupata chochote kile.
Kwa
utaratibu wa utumishi wa umma namna ulivyo, mkubwa hata kama atalipwa kiasi
gani lazima mtumishi wa ngazi ya chini atashiriki iwe kuweka saini, kulibeba
faili, kuchapa barua, kufanya uhakiki wa malipo hayo, kuhifadhi hiyo nyaraka au
kutuma hizo fedha za kwenye mfumo wa malipo . Kwa hiyo kutoshirikisha watumishi
wa ngazi ya chini kupata posho/ bakishishi na stahiki zote za kisheria kunaleta
malalamiko mengi na huko si kutenda haki na mtake mistake nyaraka za serikali
zitakuwa mitaani.’
Mwisho wa siku tulikubaliana kuwa zoezi
hilo linaweza kufanyika kwa kutoa angalau posho/bakishishi kwa kila mtumishi
lakini si kwa kutoa pesa bali kwa kutoa kitoweo wakati wa sikukuu za kidini.
Jambo hili lilipokamilika nilimuagiza Mkuu wa Idara ya Mifugo wakati huo ambaye
alikuwa akifahamika kama Eliezeer Moses
ndugu huyu alisema kuwa suala hilo linawezekana kwa kuwa wilaya hiyo ilikuwa na
wafugaji wengi basi wangeweza kuwasiliana na kupata wanyama hao ili wachinjwe
kwenye machinjio ya Halmashauri.
Kweli tulipozungumza na Bwana Fedha wa
Halmashauri zoezi hilo lilikamilika na fedha kutolewa kwa kila sikukuu za dini
huku tukishirikiana na wale wanaofanya biashara ya kuchinja mjini hapo na zoezi
lilikuwa jepesi ”
Kumbuka msomaji wangu
Mwanakwetu yu Mwaya Ulanga Morogoro na hiyo ni Novemba 2021.Mwanakwetu
aliendela kuyatayarisha makala yake,
“Kwa hiyo ikiwa kama motisha ya
watumishi wote kwa kila Pasaka, Maulidi, Noeli, Idd al Haji na Idd el Fitri. Kila
kulipokuwa na sherehe hizo ikawa kama destruri ya kununuliwa ng’ombe kadhaa
wakichinjwa na kugawiwa watumishi wa halmashauri hii huku nilibainia kuwa nyama
hiyo ilipotolewa watumishi wote wa wilaya hii kutoka taasisi zingine za umma
walikuwa wakipewa bila ubaguzi ambalo kwa hakikia lilikuwa jambo zuri na la
kujenga umoja na udugu.
Nilibainia kuwa hata watumishi waliokuwa
na kipato kikubwa waliweza kuchukua kilo mbili hizo za nyama kila sikukuu kwani
ilikuwa ni haki yao. ‘Ngoja tukachukue
nyama tuliyopewa na mwajiri wetu’.Hayo yalikuwa maneno ya kawaida
wakiwalingishia wale ambao siyo watumishi wa umma.Kwa hilo lliwavutia baadhi ya
wasio watumishi wa umma kuwa watumishi wa umma.
Kwa hakika Lushoto zoezi hili
lilifanyika vizuri na halikuwa na mashaka yoyote huku sikukuu ikifika hata kama
mkubwa amesafiri bali alikumbushwa juu ya hilo.
Nyuma ya pazia katika kutoa kitoweo cha
kilo mbili za nyama ilikuwa ni kitu muhimu sana kuna wakati wa sikukuu inafika
mtumishi hata kama sikukuu si ya dini yake anawajibu wa kupika chakula kizuri
ili familia yake iweze kuwa na amani. Kwani nyumba ya jirani pana nukia pilau
watoto wa mtumishi wa umma kweli wanakosa chochote?
Wapo wengine ambapo siku za sikukuu
uenda kula sikukuu miji mingine makubaliano na vyama vya wafanyakazi yalikuwa
wale wasiokuwepo wasichukuliane kwa hoja moja kuwa wao sikukuu hawapo “
Mwanakwetu aliendelea
kuyaandika makala yake siku hiyo hapo Mwaya Tarafani.
“Haiwezekani wewe ni kiongozi wa taasi una
furaha kubwa wenzako unaowangoza wana shida, dhiki na tabu. Kwa hiyo kila mmoja
alipata kitoweo chake, yeye alikuwa na jukumu la kutafuta mchele tu na bei ya
mchele ilikuwa kati 1200-2000/= Nyama ilikuwa 6000-7000/- ”
Msomaji wangu tambua hili;
“Katika Bibilia kuna simulizi tele za
umuhimu wa chakula mathalani, kumbuka Yesu katika Karamu ya Mwisho aliketi na
kula na wanafunzi wake, kumbuka nadhani mtoto wa kwanza Yakobo kupoteza Ufalme
hoja ilikuwa ni chakula,kumbuka kisa cha Malkia Sheba na Chakula katika Ufalme
wa Wayahudi.
Kuna umuhimu mkubwa katika maisha ya
mwanadamu pawepo na upatikanaji wa chakula. Unaweza Kusema Kazi Iendelee/ Hapa
Kazi Tu.Je hawa watu wanachakula je wanakula wanashiba?
Watu
Wenye Njaa na KiuuWanahamisha Ufalme”
Kumbuka msomaji wangu
Mwanakwetu yu Mwaya akiandka makala haya.Baadaye ya miaka mitatu Mwanakwetu
alihamishiwa Halmashauri ya Mbozi , alifika hapo Agosti 15, 2018.
Anakumbuka alipofika tu
baada ya juma moja kulikuwa na sherehe ya Maulidi ya kuzaliwa Mtume Mohammed S.A.W.
Kumbuka zile habari za Lushoto uzoefu wake wa kutoa posho hapa alitoa agizo
hilo la kununuliwa ng’ombe na kuchinjwa na kugawawiwa kwa watumishi zaidi ya
4000.
Mbozi walienda mbali zaidi
kwani angalau kila mtumishi walishauri apatiwe na kilo 2 za mchele na kilo
mbili za nyama, hapa posho ilikuwa kubwa.
Msomaji wangu kilo mbili za
nyama na kilo mbili za mchele ni karibu shiling 20,000/= hiyo siyo kitu kwa mtu
mwenye ukwasi na ni kama upuuzi tu LAKINI KWA AMBAYE FUKARA/MASIKINI / HOEHAE/
PANGU PAKAVU TIA MCHUZI / AKINA YAKHE ambaye fedha hana na tena siku ya
sikukuu, hata kama ana mshahara, pengine kaukopea, au anawalipia karo za shule
watoto wake kadhaa, Posho ya Nyama na
Mchele ni mkombozi wa familia.
Nyuma
ya pazia yakizungumzwa haya maneno,
“Duu jamaa kwanini ametoa nyama na
mchele kwa watumishi ? Huyu atakuwa anafanya kafara za kwao.
Huyu jamaa ametoa nyama katika sherehe
ya dini yake, yeye ni Muislamu ndiyo maana amefanya hivyo kwa Waisilamu wenzake.
Hawa waswahili wana shida sana!”
Haya yalisemwa bila hata ya
kutambua dini ya wanayemlalamikia. Posho ya nyama na mchele iliendelea kutolewa
kila sikukuu za dini na hilo liliongeza motisha kwa watumishi japokuwa ilikuwa
vigumu kuweza kuwagusa watumishi wote haswa wale wa vijiji vya mbali na wilaya
ya Mbozi lakini ilibainika kuwa wengine walikuwa wakifunga safari kuchukua
posho yao Mjini wale wa maeneo yaliyokuwa yakifikika na hapo wilayani.
Hapa ni watumishi ambao
walikuwa kata ambazo gharama za kufika Vwawa zilikuwa kwenda na kurudi haifiki
2000-3000/= walikwenda kwa wingi maana
kigezo kilikuwa ni kitambulisho cha kuwa mtumishi wa Halmashauri ya Mbozi tu.
Ikaja noeli tukatoa vizuri
posho hiyo na hakukuwa na hoja yoyote, kukawa kimya huku sasa wakibaini kuwa
huyu jamaa huwa anatoa posho hiyo posho kila sikukuu na kigezo cha dini
kilipotea na wengine walifahamu kuwa huyu ni Mkristo.
Kumbuka unapoona kuwa kimya
tambua kuna jambo linaendelea, usindanganyike jambo limekwisha, ilipofika Pasaka
ya 2019 maandalizi ya kuwanunulia watumishi ng’ombe na mchele yalifanyika
vizuri huku watumishi wakiekezwa pahala pa kuchukua nyama na mchele hapo hapo
Halmshauri VWAWA.
Mwanakwetu alikuwa yupo
nyumbani kwake huku na yeye akiletewa kiasi ya nyama na mchele na watumishi wa
Idara ya Mifugo waliyokuwa wanasimamia zoezi.
Ilipofika saa 12,30 ya
asubuhi huku nyama hiyo ikikaribia kugawiwa alijulishwa kuwa kuna sehemu ya
nyama ambayo ipo katika machinjo hayo ilikuwa imechinjwa na watu ambao siyo
wahusika wa kuchinja. Jambo hilo lilileta taharuki kubwa huku Mwanakwetu akiwasiliana
na Shekhe wa Kata ya Vwawa na Shekhe Mkuu wa Wilaya hiyo aliyekuwa akifahamika
kama Shekhe Mbwana.
“Nilijulishwa kuwa vijana watatu
waliingia katika machinjio hayo na kuanza kuwachinja ng’ombe wa watumishi lakini
kwa bahati nzuri Shekhe wa Kata ya Vwawa aliwabaini baadaye suala hilo
lilijulishwa kwa viongozi na nyama hiyo
kutengwa na baadaye kugawiwa wahitaji wengine ambao wao wenyewe walihitaji.
Swali lilikuwa nani aliwaruhusu vijana
hao kufanya tukio hilo? Waliingiaje katika machinjio hayo wakati kuna walinzi?Nani
aliwaagiza kufanya hivyo? Walifanya hivyo kwa manufaa ya nani? ”
Mara baada ya kufanya
uchunguzi huo ilikuwa ni kweli kuna vijana waliweza kuingia pahala pa kuchinjia
nyama.Walihojiwa na kuchukuliwa hatua kali huku Shekhe Mbwana-Shekh Mkuu wa Wilaya ya Mbozi wakati huo akisisitiza
wale wanaosimamia uchinjanji wa nyama kwa mujibu wa taratibu za BAKWATA kuwa
makini kuwahi pahala pa kuchinjia na kutimiza wajibu wao ipasavyo na
asiyehusika asisogelee eneo la machinjio hayo kabla ya wakati.
Kwa upande wa Halmashauri
hii walinzi, Bwana Afya wa Kata na wasimamizi wote wa zoezi hilo walitakiwa
kuwa makini maana suala hilo linaweza kuharibu amani na nia njema ya kutoa
posho /bakishishi hiyo kwa watumishi.
Mwanakwetu kumbuka alikuwa
Mwaya alipomaliza kuyandka makala haya aliyatuma katika vyombo vya habari na
kuchapishwa siku zilizofuata.
Mwanakwetu
anasema nini siku ya leo?
Mwanakwetu anakumbuka kuwa
Mei Mosi ya Kila Mwaka ni siku ya Wafanyakazi Duniani swali ni je kila mwajiri
anatimiza wajib wake kuwapa motisha wafanyakazi wake? Shabaha ya makala haya ni
kumkumusha kila mwajiri kutoa motisha kwa wafanyakazi wake hasa watumishi wa ngazi
ya chini, Waajiri wasijitazame wao wenyewe tu, hilo ni kosa na udhaifu mkubwa.
Mwajiri yoyote anapaswa atambue
kuwa katika kujali maslahi ya wengi kuna
vikwazo vingi, maana watu ni wabinafsi,ukiwa mkubwa upe kisogo ubinafsi.
Katika jamii zetu walio
wengi wanateseka sana na wanalalamikia mioyoni mwao.
Katika kuwasaidia watu kuna
changamoto moja kubwa anaye fanya hivyo anaweza hata kupoteza hata nafasi yake kwa visa vingi.Mwanakwetu
anakwambia usirudi nyuma wewe leo ni mkubwa kesho siyo wewe na siy mwanao, ni
mtu mwingine kabisa.
Kumbuka kama hawa waliotuwa
kuingia zizini na kuwachinja ng’ombe huku wao wakiwa siyo wahusika na siyo
Waisilamu, hiyo yote ni kumrudisha nyuma mtu mwenye nia njema .
Katika tukio hilo waliofanya
hivyo hawakutambua mambo mengi ;
mahusiano ya Mwanakwetu na
Ustadh Mbwana na pia hawakutambua kuwa
Ustadh Mbwana -Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Mbozi alikuwa anafahamiana na
Mwanakwetu kabla ya kufika hapo, hawakutabua Ustadhi Mbwana alikuwa anazo
taarifa za Mwanakwetu za utoaji wa ruzuku nyakati za sikukuu tangu Lushoto.
Kwa kukuongezea msomaji
wangu wakati Mwanakwetu anatoka Lushoto aliwaaga Viongozi wa BAKWATA Wilaya ya
Lushoto , akiwamo Katibu wao maana mwenyekiti alikuwa amefariki hawa Viongozi
wa BAKWATA walituma ujumbe kwa BAKWATA–MBOZI.
“Huyo
jamaa anakuja , ametoka hapa Lushoto, ni mtu mwema , ni Mkristo nawaombeni mkae
nae vizuri.”
Mwisho kabisa huyu Ustadh
Mbwana Mwenyekiti BAKWATA Mbozi alikuwa alikua mzaliwa wa Korogwe Milimani- Kwa
Profesa Maji Marefu, Tanga
Katika jambo hilo msomaji
wangu tambua kuwa viongozi wa dini wanayafahamu mengi kikubwa kwa viongozi
serikali na waamini waheshimuni sana sana bila kujali wa dini yako au dini ya
mwingine, hawa wana taarifa nyingi za maeneo walipo a hata taarifa za viongozi
.
Mwisho kabisa Mwanakwetu
anasema haya ,
“Anawaomba
viongozi wa CCM wa Mkoa wa Songwe shirikianeni na huyu Mkuu wa Mkoa wa sasa
ndugu Daniel Chongolo, kwa maana spidi ya maendeleo ya mkoa wa Songwe
Mwanakwetu anatilia shaka, shida ni wanasiasa wa kutoka CCM lakini wananchi wa
Songwe ni wanapenda maendeleo sana.
Mfano Mdogo Hamashauri ya Mbozi hadi leo hii bado ni Halmashauri ya Wilaya, ipo mkoani! Je walipo sasa wanakusanya mapato vizuri? Mbozi ikiwa Manispaa Mlowo inakuwa Halmashuri ya Wilaya -bajeti ya miradi ya serikali inaongezeka idadi ya watu mnayo, mapato yapo kama yanasimamiwa vizuri
Msaidieni Daniel Chongolo, mjisaidie
wenyewe, angalieni maendeleo ya upande wa mpaka kule Zambia oneni gere, lazima
Mbozi iwe manispaa ili Mbozi ikutane na Mbalizi.na ikutane na Tunduma.
Viongozi
wakifika hapo wanaondoka vibaya kwanini? Kila Mkuu wa Mkoa mbaya? Chiku Galawa alikuwa mkuu wa mkoa Mzuri ameondolewa W.ananchi wa Songwe wanataka / wanayapenda maendeleo.
Namuomba
Dkt Emmanuel Nchimbi itazameni CCM ya huu mkoa na wale waliyopigiwa kura iwekeni
vizuri. ”
Kumbuka tu hii,
“Wenye
Njaa na Kiu Wanahamisha Ufalme”
Nakutakia
Siku Njema.
makwadeladius@gmail.com
0717649257
Post a Comment