BURIANI JELLAH MTAGWA.

 


Adeladius Makwega.-MWANZA.

“Wewe ni Waziri wa kwanza toka tumepata uhuru, mimi nimecheza mpira siku nyingi sana, toka ezi za Julius (Julius Nyerere); mpaka leo hakuna hata kiongozi mmoja aliyewahi kuja kuniona au waziri anayeweza kutembelea watu kama sis, (watu kama sisi), mwenye moyo kama wewe sijamuona.”

Hiyo ni MAELEZO ya marehemu Jellah Mtagwa ambaye alikuwa mchezaji wa zamani ya Timu ya Pan African ya Kariakoo na Young African ya Jangwani zote za Dare es Salaam na timu ya taifa –Taifa Stars ya Tanzania ambaye amefariki Mei 16, 2024 katika Hosptali ya Mloganzila.

Kwa ambao hawafahamu Jellah Mtagwa ni miongoni mwa Watanzania wenye asili ya mkoa wa Morogoro ambapo mara baada Uhuru mkoa huo ulitoa vijana wengi wenye vipaji katika Sanaa, Michezo na hata Utamaduni wa taifa hili la Afrika Mashariki.

Jellah Mtagwa mpaka leo hii Mei 17, 2024 ndiye Mtanzania pekee aliyeiongoza Taifa Starts kwa kipindi kirefu kama nahodha kwa miaka 10 na kuifikisha timu hiyo katika mafanikio makubwa ya soka.

Akiwa hai marehemu Jellah Mtagwa aliwahi kusema maneno haya,

“Viongozi wengi wanatoa kauli zuri lakini hakuna ufuatiliaji hata kidogo, ndiyo maana Mzee Ali Hassani Mwinyi(Rais wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) alisema Tanzania ni Kichwa cha Mwedawazimu hawakumuelewa anamaanisha nini, hilo halikufanyiwa kazi hadi kesho. Kiongozi upo madarakani haujui hata kiongozi aliyekutangulia alisema nini au alikosea wapi? Hatuwezi kushinda namna hiyo; kero yangu nyingine hawa POSTA TANZANIA wametumia picha yangu hawajanilipa hata senti tano.”

Hayo pia ni malalamiko ya nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania kwa miaka 10 ambayo ameibeba bendera ya taifa letu kwa niaba yetu sote, kilio hicho kinatutaka mimi na wewe kutimiza wajibu wetu na ndiyo maana tunapewa majukumu.

Jellah Mtangwa alilalamika na hata familia yake ililalamika.

“Tatizo kubwa ni stroke, mifupa yake ilikataa kabisa , baada ya kupata madawa mengi pressure ilipungua, ikawa afadhali , sukari pia ikawa afadhali lakini mifupa iligoma na hii inatokana na kazi yake aliyoifanya katika mchezo wa soka.”

Haya ni maelezo ni ya mke wa Jellah Mtagwa aliyejitambulisha kwa jina la Mboni Binti Ramadhani.



 

Mwaka 2019 aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe akiambatana na aliyekuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Nchini ndugu Yusuf Singo walimtembelea Marehemu Jellah Mtagwa nyumbani kwake ,miaka mitano baadaye yaani Mei 16, 2024 Jellah Mtagwa amefariki dunia.

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Suala la malalamiko ya Jellah Mtagwa yalisikika lakini, lakini shida ya Tanzania kila mmoja anaona hausiki, tunaweza kusema Shida ni POSTA Tanzania lakini tujiulize ile furaha ya ushindi wa Timu ya Taifa ni ys POSTA Tanzania peke yake, ilikuwa ni ya Waziri Mwakyembe peke yake? Je hakukuwa na mtu hata mmoja  wa kuwaambia POSTA mpeni Jellah Mtagwa pesa yake? Jamani mpeni haki yake, achani dhuluma.?

“Katika Furaha tuwe pamoja na katika dhiki tuwe Pamoja”

Buriani Jellah Mtangwa

makwadeladius@gmail.com

0717649257




 

0/Post a Comment/Comments