MIMI NITAUPELEKA ZANZIBAR.

 

Adeladius Makwega-MWANZA

Salumu Mtumbuka ni Mkufunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya (MCSD) alionekana amevalia kofia ya Mungu Usinione ya Rangi Nyeusi, fulana ya Rangi ya Kijani na suruali ya michezo Nyeusi Tii na miguuni akivalia raba nadhifu, Mwanakwetu akajiuliza.

“Huyu Mkufunzi leo hii anakwenda UMISETA mkoa gani?”

Mwanakwetu alibaini kuwa UMISETA na UMITASHUNTA bado haijanza, sasa leo hii mkufunzi huyu anakwenda wapi aukua Mwege wa Uhuru, maana nao wanava sare za michezo.
?
Alipouliza alijibiwa kuwa anakwenda kufundisha Mpira wa Kengele(GOAL BALL), hilo likamvutia Mwanakwetu hadi darasani kujionea  mwenyewe juu ya Mpira wa Kengele.

Mkufunzi Mtumbuka aliingia darasani kwake na kuanza kufundisha kwa vitendo baadhi ya mbinu za kuucheza mchezo huu.

“Mchezo huu unawachezaj watatu kila upande na kila timu inawachezaji watatu wanaoweza kuingia uwanjani kwa kubadilishwa kutoka wachezaji wa akiba yaani wale wanaosugua benchi. Hoja zikiwa sababu kadhaa kuumia, timu kubadilisha wachezaji au dharura  yoyote uwanjani.”

Mkufunzi Mtumbuka aliendelea kufundisha somo hilo kwa vitendo naye Mwanakwetu akipandwa na midadi ya Mpira wa Kengele.

“Mchezo huu unachezwa na wanaume na hata wanawake lakini kikubwa wakicheza wanawake wanacheza wenyewe na wakicheza wanaume wanacheza wenyewe, maana maumbile na misuli baina ya wanaume na wanawake yanatafautiana mno namna yalivyojengeka.”

Somo hilo lilifanyika kwa vitendo kwa zaidi ya saa mbili kwa darasa lenye wanafunzi zaidi ya 100 na mmojawapo alikuwa ni Prisca Silivine Ngombo ambaye alisema haya,

“Mpira wa Kengele nimeupenda sana, mimi ninatokea Halmashauri ya Igunga mkoani Tabora, Ninatarajia kwenda kuufundisha shuleni kwangu na kama nikipwa ruhusa ya kuufudisha kwa ngazi ya Kata, Tarafa na Wilaya nitafanya hivyo kwa moyo wangu wote.”

Darasa hili lina mkusanyiko wa wanafunzi kutoka pande zote nne za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwamo 


 

Makame Hamis Salumu akitokea Zanzibar;

“Mimi ninategemea kuufundisha mchezo huu baada ya kuhitimu mafunzo yangu, ninaziona fursa tele katika Mpira wa Kengele, mchezo huu unachezwa na wenye uono hafifu, Mimi Nitakwenda Kuufundisha Zanzibar natambua Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaniunga mkono.”

Wakati somo hili linafundishwa kwa vitendo mwanachuo Fortunatus Frazon Boniface Mpira wa Kengele ulitupwa katika mikono yake na kutupwa katika miguu yake na ulipotupwa tumboni mwake alipiga mayowe na kitendo hicho kilitokea kwa wanachuo wengi lakini hali ilikuwa tofauti kwa mwnachuo Makame Hamisi Salum kutoka Zanzibar na alipoulizwa kwa nini yeye hakupiga kelele mpira ulipotupwa tumboni alijibu haya,

“Namna ya ninavyofanya mazoezi kila mara,ni kweli huu mpira ni mzito, una kilo moja na robo ukitupwa tumboni lazima utapiga yowe ..”

Alipotafutwa Fortunatus Frazon aliyepiga kelele sana mafunzoni alisema haya,

“NI kweli nilipiga kelele sana, kwanza kabisa yule mtupa mpira nilijua unakuja mikononi lakini yeye alitupa tumboni kwangu, nilishituka sana lakini hii ni mara ya kwanza naamini kipindi kijacho nitafaya vizuri.”

Mpira wa Kengele ni mchezo uliochewza mara ya kwanza Ulimwenguni baada ya Vita vya Pili vya Dunia kumalizika, wapo waliopoteza maisha yao, wapo waliopata vilema vya kudumu kwa viungo mbalimbali vitani, ikiwamo miguu, mikono na macho na kuwa vipofu wa milele. Waliopata vilema hivyo walikuwa wakipambana katika vita hivyo kulinda amani ya wengine.Ndugu hao kabla ya vita hivyo walikuwa wakishiriki michezo kadhaa, lakini vilema walivyopata vitani vikakwamisha kushiriki michezo tena. Je walipaswa kutengwa na jamii zao? Majibu yake yalikuwa hapana lazima iandaliwe aina ya michezo watakayoweza kushiriki wakiwa na upofu/au uono hafifu.


 

Ndugu Hanzi Lorenzen wa Australia na Sepp Reindle raia wa Ujerumani, mwaka 1946 walikuja na majibu ya mchezo huo kwa vipofu na wale wenye uono hafifu, mchezo huo ukaitwa Mpira wa Kengele Huku kwa mara ya kwanza nchini Tanzania inaaminika kuwa ulichezwa kwenye mashindano ya 20 ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (Umitashumta) mwaka 2021 yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha, Pwani.Mchezo huu pia ni mchezo mgeni mno kwa Mwanakwetu nayeye hafahamu kama wewe msomaji wake unautambua zaidi yake na ndiyo maana akayaandika makala haya.

Mpira wa Kengele ni Mchezo unaokataa makelele ilikuwapa nafasi wachezaji kusikia milio ya kengele ndani ya mpira na kuufuata ulipo.

Leo hii msomaji wangu mkumbuke sana ndugu Makame Hamisi Salumu anayesema,

“Mimi Nitaupeleka Zanzibar.”

Nakutakia siku njema.

 makwadeladius@gmail.com

0717649257









 

 

0/Post a Comment/Comments