Adeladius Makwega-MWANZA
Wakurufunzi kadhaa wa Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya, wadau wa Mchezo wa Soka wa kanda ya ziwa wameshiriki mafunzo maalumu yaliyotolewa katika viunga vya chuo cha michezo huku yakifundishwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Soka la Afrika(CAF) ndugu Kaijage Kaijage hapa mkoani Mwanza.
Mafunzo hayo yalifanyika kwanza kwa nadhalia darasani na baadaye kuhamishiwa viwanjani hatua kwa hatua ili kuonesha kile kilichofanyika katika kuta za darasa kinapaswa kufanyika vipi katika pembe nne mstatiri za kiwanja cha mpira wa miguu.
Kwa hakika hatua zote mbili nadhalia na vitendo zikiwahusisha wakurufunzi wote zaidi ya 50.
“Wakurufunzi wangu wote wamejifunza vizuri na niliweka msisitizo katika masuala mengi, nimewapa mitihani kadhaa ya nadhalia na vitendo, ninasema wazi wamefanya vizuri.”
Haya yalisemwa na Mkufunzi Kaijage huku akiongoza mafunzo yake kiwanjani Malya Mei 15, 2024.
“Kwa hakika nimejifunza mengi, mafunzo haya yamenipa mwongozi mzuri wa kuufundisha mchezo huu, kipo kitu kipya nimekipata, nina hakika hapo mbeleni nitautumia vizuri ujuzi huu.”
Haya yalisemwa na Evodia Komba miongoni wa wakurufunzi hao, mwanachuo wa mwaka wa pili katika chuo hiki cha michezo ambaye pia ni mwalimu katika Halmashauri ya Mbarali mkoani Mbeya.
“Binafsi ni mdau wa ufundishaji wa mchezo wa soka, nilikuwa nakosa fursa kadhaa awali lakini sasa nimepata mafunzo haya yananifungulia milango zaidi ya fursa hizo, ninasema alhamdulilah.”
Haya yalisemwa na Hussein Eliasa ambaye ni mdau wa soka kutoka Kahama ambaye alikuwa miongoni mwa wakurufunzi hao wa mchezo huu walishiriki hatua zote za nadhalia na vitendo vya darasa la Mkufunzi Kaijage, huku mwandishi wa ripoti hii akiona namna mkurufunzi Eliasa alivyokuwa akitekeleza alichojifunza kwa kujiamini kutoka kwa Mkufunzi Kaijage.
Mafunzo hayo yanafikia ukingoni Mei 16, 2024 ambapo Mkufunzi
Kaijenga alifika katika viunga hivyo kutoka Bukoba ambaye anatoa mafunzo haya
maeneo kadhaa, huku idadi ya washiriki wanawake ilikiwa pungufu yaani kati ya 1-5 na ushiriki wa wanaume ukiwa kati
ya 1-40.
Post a Comment