AFANYAE HARAKA KATIKA UTAJIRI ATAADHIBIWA-MCHUNGAJI NKANYA.

 


Adeladius Makwega –MWANZA

Mchungaji DanieL Nkanya wa The Free Pentecostal  Church Of Tanzania (FPCT) hapa Malya Kwimba mkoani Mwanza amesema kuwa uaminifu kwa wasomi ni jambo la msingi katika jamii yetu maana wasomi wengi ndiyo wanaokuja kukabidiwa majukumu ya umma na kwa sasa wasomi hao wengi mioyo yao imejaa tamaa na husuda.

Haya yamesemwa Julai 30, 2024 katika viunga vya Chuo Cha Maendeleo ya Mchezo Malya (MCSD) katika mahafali ya jumuiya wanachuo waliokoka wa vyuo vya kati na vyuo vikuu Tanzania (CASFETA) ambao wanamaliza stashahada kadhaa za michezo katika chuo hiki cha umma .

“Nyinyi wote mnaohitimu mmesomea michezo, lakini huko viwanjani tunasikia muamuzi fulani kahongwa. Rushwa yenyewe ya milioni mbili wakati kila mechi unalipwa lakini mbili. Jamani hii ni aibu yako na iabu hata wale waliokusomesha, heri halali kidogo kuliko haramu tele.”

Akizungumzia masuala ya kiroho kwa wahitimu hao, Mchungaji Nkanya alisema kuwa hivi sasa Ukristo unachangamoto kubwa, kumeibuka kuwa na wachungaji, mitume na maaskofu kila kona.

“Mtu akijua kiodogo mistari ya Biblia anaanzisha kanisa laki jiulize wewe umelelewa na nani? Kila mmoja katika imani lazima uwe umelelewa pahala Fulani na huyo mlezi anafahamika.”

Mchungaji Nkanya aliagiza mmojawapo wa wahitimu kusoma Mithali 28,20

“Mtu muaminifu atakuwa na baraka tele, lakini afanye haraka kwa tajiri ataadhibiwa.”

Akizunguza katika mahafali haya Mgeni Rasmi Bi Epifania Bugaga ambaye ndiye Mwadili wa Wanachuo amesema kuwa anawapongeza kwa kuhitimu huku akiwaomba wahitimu hao wasimuache Yesu Kristo maishani mwao.

“Shikeni imani yetu, sisi sote ni Wakristo Yesu ambaye ndiye njia ya kweli na uzima.”

Wakingumza baada ya kuhitimu baadhi ya wahitimu hao walimshukuru Mungu kumaliza salama na pongezi tele kuwapa wakufunzi wao waliwaongoza katika kozi mbalimbali akiwamo Mkuu wa Chuo hiki Richard Mganga.

“Miaka miwili niliiona mingi, kumbe si mingi ratiba ya shule ilikuwa na nafasi kubwa kwangu, leo ninahitimu siamini kama miezi 24 imekamilika.”

Haya alisema mhitmu Endaeli Mtango

 


 

Naye Ezra Lupoli huku akifurahia kuhitimu na akiwaongoza wenzake kwa mapambio kadhaa alisema kuwa Yesu ni mwema, leo anamaliza salama na elimu hii itamfungulia milango zaidi.

“Nimemskiliza vizuri Mchungaji Nkaya kuwa kujifunza michezo kuna hitaji uadilifu nina hakika nitakuwa muamuzi  wa soka na nitachezesha mechi zote kwa haki hata kama mimi ni Yanga au Simba.”

Kwa upande wake Samweli Daudi Almasi ambaye ni miongoni mwa wanachuo wa umoja huo anayeendelea na masomo amewapongeza wahitimu hao kwa kukaa nao vizuri kipindi chote tangu wanawapokea mwaka wa 2023.

 


 

Naye Katibu wa Serikali ya Wanachuo hapa MCSD ndugu Francis Maramonji amesema CASFETA ni umoja ambao unaongozwa na viongozi watulivu, makini, wenye hekima na wakiwa na jambo wanalisema kwa uwazi.

“Nawapongeza wahitimu wote Mungu atawabariki huko waendapo na wanaobaki wajifunze sana kwa wanaohitimu.”

Mgeni Rasmi katika mahafali haya alitoa vitabu 10 vya TENZI ZA ROHONI kwa wanachuo wanaobaki.




 

0/Post a Comment/Comments