SHEIKH MKUU MWANZA AONGOZA DUA KUMUOMBEA RAIS SAMIA MAHAFALINI.



Adeladius Makwega-MWANZA

Jumuiya ya vijana wa Dini ya Kiisilamu wa Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu Tanzania tawi la Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya(MCSD) Juni 29, 2024 imefanya mahafali ya wahitmu wake wanaomaliza masomo yao katika michezo huku mahafali hayo yakiambatana na dua maalumu kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mahafali hayo awali yalitanguliwa na kisomo maalumu kutoka aya mbalimbali za Korani Tukufu huku vijana hao waliyosoma wakitunzwa kwa zawadi na fedha.


 

Baada ya kisomo hicho ndipo maikrofoni allikabidhiwa Kaimu Shekh Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ustadh Fadhili Salimu Lugiwe akisema kuwa mjumbe hauwawi , Sheikh wa Mkoa wa Mwanza amemtuma yeye yote wayasikilize aliyoagizwa.

“Awali kabisa nawaombeni tumumbee Rais Samia Suluhu Hassan ili awe na afya njema na aweze kufanya kazi yake vizuri na abaki katika njia sahiihi ambayo yupo mpaka sasa.”

Dua hilo lilisomwa kwa dakika kadhaa huku waamini na waalikwa wote wakiwa wamesimama, awali Sheikh Lugiwe alisema kuwa katika maisha binadamu unatakiwa kusema jambo unalolijua na kufanya jambo unalolifahamu na hiyo ndiyo elimu na ndiyo maana mkitoka hapa mmehitimu mtaweza kusema na mtaweza kufanya kwa uhakika.

“Mungu anasema elimu ninayowapeni ni kidogo tu, mwanadamu hawezi kujua yote, mkimaliza msipandishe mabega, heshimuni watu wote wakubwa kwa wadogo.”

Kaimu Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mwanzo aliongeza kuwa ,

“Maisha ya sasa hayana ujanja ujanja, elimu inahitajika ilikuyakabili maisha haya vilivyo.”

Akizungumza baada ya mahafali haya ustadh Yahaya Said ambaye ni miongoni mwa wahitimu hao alimshukuru Mungu kumaliza salama naye Ustadhat Modesta Lupenza alisema kuwa amefurahi kwa Shekh Mkuu Mkoa wa Mwanza kuyapamba mahafali hayo kwa dua maalumu la kumuombea mema Rais Samia Suluhu Hassan.

“Binafsi tu namuombea Rais Samia afya njema.”

Kwa upande wake katibu Serikali ya Wanachuo hapa MCSD Francis Maramonji amewapongeza wahitimu hao kwa kufanikisha mahafali yao

“Jumuiya hii inashirikiana vizuri na serikali ya wanachuo, wenzetu wanahitimu na zamu yetu inafuata, nawatakia maisha mema huko waendapo.”

Wanachuo hao wanakaribia kufanya mitihani yao ya kuhitimu hivi punde.







 







 


0/Post a Comment/Comments