Adeladius Makwega-MWANZA
Wakristo wameambiwa kuwa masomo ya dominika ya leo yanasisitiza kila mwanadamu kumthamini mwanadamu mwenzake na ndiyo maana visa viwili vinavyoonekana katika Injili ya leo vinaonesha Yesu alivyo msaada kwa jamii mbili.
“Kwa Jina la Baba na La Mwana na la Roho Mtakatifu-AMINA. Bwana Awe Nanyi- Awe Rohoni Mwako. Ndugu zangu karibuni katika Adhimisho la Ekaristi Takatifu ndani ya dominika ya 13 ya Mwaka B wa Liturujia ya Kanisa, wakati tunakatafakari masomo ya misa hii kila mmoja atilie maana namna Yesu Kristo alivyomfufua mtoto wa Jailo na namna alivyomponya mama aliyekuwa akitokwa damu miaka kumi na miwili, mama huyu alipokea uponyaji kutokana na imani yake nasi tukumbuke tutapokea uponyaji wetu kadili ya imaini yetu, kubwa sisi sote tumfanye Yesu Kristo kuwa kila kitu katika maisha yetu.”
Haya yamesemwa na Padri Samson Masanja Paroko wa Parokia ya Malya-Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza katika misa ya kwanza iliyoanza saa 12.07 ya asubuhi katika Kanisa la Bikira Maria Malkia wa Wamisionari.
Padri Masanja alianua jamvi la mahubiri yake akisema kuwa injili inaonesha Yesu Kristo anakimbilia na watu wote na kwake changamoto zote zinatatuliwa, je wewe na mimi tunamkimbilia nani? Sote tukumbuke kimbilio letu ni Yesu Kristo.
Katika misa hiyo hiyo ya kwanza ya jumapili umeme ulikatika saa 7. 11 ya asubuhi na baadaye kurejea saa 7.13 wakati huo misa hii ilikuwa katika kipindi cha MAGEUZO Padri Masanja aliweza kuendelea na MAGEUZO vizuri maana mwanga wa jua ulisaidia yeye kuweza kuongoza misa hii japokuwa ulikuwa mwanga hafifu.
Kwa sasa katika eneo la Malya na viunga vyake kumekuwa na desturi ya umeme kukatikakatika na kurudi hata mara nne kwa siku moja ambapo zoezi hilo ni hatari kwa vifaa va umeme, makazi ya watu na hata watoto wanaozaliwa NJITI na kuhifadhiwa katika Ikubeta ndani ya Hospitali zetu.
Post a Comment