Adeladius Makwega-MWANZA
Mei 5, 2024 Mwadili wa Wanachuo wa Chuo cha Maendeelo ya Michezo Malya, Bi Epifania Bugaga alifanya usaili wa vijana 10 waliotia nia kugombea nafasi za uongozi wa Serikali ya Wanachuo katika taasisi hiyo inayotoa Astashahada na Stashahada ya Michezo nchini Tanzania.
Kamati hiyo ilikuwa na wajumbe wafuatao;
“Omari Mataka(Katibu wa Kamati) , huku wajumbe wengine ni Salumu Mtumbuka, Mtweve Kayanda, Wilbert Silvery, Rahma Abdi, Faudhia Chamng’anda na Athanas Mweechela.”
Waliojitokeza kutia nia ni ,
“George Mkinga, Mayasa Semtibua, Francis Maramonyi, Philipo Sagware, Hamisi Meleka, Saira Lunda, Jamali Buchwa, Masela Owenya, Costancia Kisege na Abdalla Msabaha.”
Zoezi na kuwasikiliza wagombea wote lilikuwa refu, huku kila mgombea akipewa muda wa zaidi ya dakika 30 kujieleza na kujibu maswali kadhaa kutoka kwa wajumbe wa kamati hiyo, hadi siku ilipomalizika maamuzi yalikuwa kama ifuatavyo,
“Kwa nafasi ya Katibu wa Serikali ya Wanachuo wagombea ni Francis Maramonji na Hamis P Meleke, Kwa nafasi ya Makamu wa Rais wagombea ni Costancia Kisege na Mayasa Semtibua na Kwa nafasi ya Urais wagombea ni Abdalah Msabaha na George Mlinga.”
Mwandishi wa makala haya aliyekuwepo katika ukumbi huo alishudia wagombea hao wakiulizwa maswali kadhaa yaliyoingoza kamati kuchuja wagombea hao.
Mjumbe Salumu Mtumbuka aliliuliza swali hili,
“Kama ukishinda kwa nafasi unayoiomba, Je falsafa ya uongozi wako itakuwa ya Kuku na Viranga vyake au Bata na Vifaraga vyake?”
Kwa hakika swali hilo lilijibiwa na kila aliyeulizwa kwa uwezo wake na Mwanakwetu hana hakika na alama walizopata kila mgombea wa swali hilo, lakini Mwanakwetu aliona kuna haja ya vijana wetu wa Kitanzania kuzifahamu kwa kina hizo falsafa za maleze ya vifaranga kwa kuku na bata.
Kwa uzoefu wa maisha ya utoto wa Mwanakwetu pale Mbagala Kizinga-Temeke Dar es Salaam.
“Mwanakwetu amekulia maisha ya utoto nyumba nambali 7 Mbagala Kizinga Mbuyuni ambapo wakati huo eneo hilo lilikuwa na mzee mmoja mfugaji wa Bata aliyefahamika kama Mzee BORA, mzee huyu aliweza kufuga bata wengi kwa sababu nyumba yake ilikuwa na maji safi na ya bomba ya kutosha na wakaazi wengi walisita kufuga bata wakidai waliogopa uchafu wa kinyesi cha bata.
Nyumba zote kando kando mtaani zilikuwa na zinafuga kuku lakini siyo bata. Nyumba ya Mzee Bora ilikuwa na wapangaji kadhaa akiwamo mwalimu wa Mwanakwetu wa somo la Sayansi Kimu darasa la saba pale Shule ya Msingi Mtoni Kijichi aliyefahamika kama Mwalimu Mandwanga.
Mwanakwetu alipokwenda kwa Mzee Bora kuchota maji alikaribishwa na harakati za bata wa mzee huyu wengi wakiwa wametotoa vifaranga tele, huku kuona bata dume likiyapanda majike hilo lilikuwa jambo la kawaida mno, hapa Bata alionekana yu mbele huku kundi kubwa la vifaranga vyake vikimfuata nyuma yake.
Hilo lilikuwa tofauti kabisa na kuku na vifaranga vyake ambavyo vilikuwa vinaanguliwa kila nyumba katika mtaa huu wa mbuyuni, kuku alikuwa jirani na vifaranga vyake muda mwingi yupo mbele na nyuma vifaranga na mara zote alikuwa akiwafunika na mabawa yake kama akihisi kuna adui, kuku kupiga kelele ilikuwa kawaida kila aliposogelewa na mwewe.”
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Aina hizi zote mbili za falsafa ya uongozi zina faida na kasoro,Uchaguzi wa aina ya ungozii hutegemea una aina gani ya wafuasi(VIFARANGA).Kikubwa kumuongoza binadamu kunahitaji falsafa zote iwe ya Kuku au ya Bata,.unazitumia kulingana na mazingira ..
Mwanakwetu upo?.
“UongozI Bora Una Tele Falsafa.”
Nakutakia Siku Njema.
makwadeladius@gmail.com
0717649257.
Post a Comment