KIJANA MZURI SHIDA HAJAOKOKA II

 



Adeladius Makwega-MWANZA

Msomaji wangu kumbuka yule chotara wa Kinyakyua na Kihaya alibakia na imani yake naye Mwanakwetu alibakia na imani yake pia baada ya mizengwe ya Josephine Chipungahelo. Sasa Mwanakwetu alienda masomoni Chuo Kikuu Tumaini Iringa. Huko Isimani ilitangazwa ndoa kuwa chotara anaolewa na jamaa mwingine wa mkoa mwingine mbali na Iringa, Mwanakwetu akitoa mchango pamoja na walimu wenzake kadhaa, maandalizi ya harusi yalifanyika vizuri lakini kwa bahati mbaya juma moja kabla ya harusi mchumba wa binti chotara alifariki dunia gafla bini vuu. Walimu waliwasiliana na Mwanakwetu kumjulisha kilichotekea na baadaye chotara akahamia Iringa Mjini.

Mwanakwetu akiwa Chuo Kikuu awali mlipaji ada alikuwa baba yake mzazi ambaye hakupenda mwanaye alowee Iringa Vijijini hivyo kumtoa huko aliambiwa aende masomoni haraka, huko kijijini alipigwa marufuku asitafute mchumba na wala asiyazoee maisha ya huko.

Mwanakwetu alipotoka kwenda masomoni ruhusa alinyimwa kwa hoja mbili; muda mchache kazini na kozi aliyokuwa anasoma haikuwa ualimu. Akiwa chuoni mishahara yake ikazuiliwa japokuwa ilikuwa inafika kituo cha kupokea mishahara cha Shule ya Wasichana ya Iringa, mhasibu aliyekuwa anasimamia kutoa mishahara ndugu Albart Kwazala jamaa mmoja Mkatoliki Mungwana akampga simu Mwanakwetu.

“Bwana mdogo, mishahara yako inakuja kila mwezi fuatilia wizarani waeleze ukweli watakuelewa tu, wewe Mtanzania kama wengine, hii nchi huru kaka, mshahara wa 108,600/- ni pesa ndogo lakini inasaidia kuzisukuma siku, Nenda Wizarani nako kuna binadamu.”

Mwanakwetu akamjibu analifanyia kazi suala hilo na atakwenda Wzarani Magogoni Dar es Salaam, huku sasa anaendelea na masomo ya Shahada ya Sanaa ya Habari, huku baba yake akimtumia pesa ya karo na pesa kidogo za matumizi. EMS Posta Iringa wakawa wanamtania Mwanakwetu kuwa mkubwa mzima, anatumiwa pesa na baba yake.

Huyu mhasibu wa Iringa Girl Albart Kwazala akamwambia Mwanakwetu,

“Bwana mdogo, wewe kijana upo vizuri, usiwe muoga nenda wizarani, kazi yangu siku hizi ni kubwa kila baada ya tarehe tano ya mwezi nakwenda benki naandikia taarifa mshahara inayorudi hazina ukiwamo wako.

Bwana dogo fuatilia, kama hauna nauli wakati unafuatilia hilo mimi nitakuwa nakupa shilingi 30,000 hadi utakapopata malimbikizo yako , ukipata unirudishie.”

Mwanakwetu kila mwisho wa mwezi anakenda kuchukua 30,000 kwa mhasibu Albart Kwazala huku ndugu Kwazala akimwambia Wewe si upo chuoni fuatilia utaona walimu wenzako wanasoma kozi zingine wengi kikubwa ni mazungumzo na wakubwa kazini. Elfu thelathini japokuwa ilikuwa ndogo lakini ilisaidia mno maisha yakasonga.


 

Siku moja tarehe kama ya 15 ya mwezi wa sita jino gego la Mwanakwetu likauma mno usiku kucha , pesa ya hospitali hana je anafanyaje? Usiku huo akampigiwa  simu chotara wa Kinyakyusa na Kihaya

“Mwenzako ninaumwa sana jino , nataka kuling’oa lakini sina pesa hata kidogo, chotara naomba unisaidie.”

Kulipokucha tu chotara mapema sana alifika nyumbani kwa Mwanakwetu akamuamsha na kumpeleka hospitai ya IMECC Iringa Mjini jirani na yale maghala ya NHC zamani, hapo Mwanakwetu akang’olewa jino vizuri kwa gharama ya shilingi 12,000 akapewa dawa za shilingi 3000 na kuanza kurudishwa nyumbani na huku chotara akimuongeza Mwanakwetu 15,000 na jumla kuu kuwa 30,000.

Njiani Mwanakwetu na chotara kuelekea Mwang’ingo walikutana na ndugu Rashidi Baraza ambaye alikuwa mchumi wa Manispaa ya Iringa wakati huo akiwa amehitimu Chuo Kikuu Mzumbe.

Rashidi Baraza, ambaye sasa ni marehemu ana udugu Ramadhani Baraza ambaye ni mwalimu kitaaluma na Katibu Itikadi Uenezi CCM mkoa wa Iringa sasa. Rashidi Baraza alisoma Tambaza na kuhitimu kidato cha nne mwaka 1995 naye Mwanakwetu alitakiwa kuhitimu 1994.Hawa walikuwa ni watu wanaofahamiana sana.”

Rashidi Baraza akamuuliza Mwanakwetu vipi upo na shemeji ? Mwanakwetu akajibu  hapana. Swali lingine likaje sasa huyu ni nani?Mwanakwetu kimya , Baraza akaendeleza mazungumzo,

“Huyu sista ninakaa naye jirani, ninasalimiana naye lakini kwa tabu kumbe Makwega anapelekwa hospitalini? Mungu anajua kuzitesa nafsi za wengine, basi Mungu mwema kwako maana kama si mimi basi kaka yangu Makwega.”

Hapo katika Hiace abiria wanyalukolo wanacheka kikubwa ni maneno ya mchumi wa Manispaa ya Iringa aliyekulia Dar es Salaam mwenye asili ya Morogoro. Mwanakwetu akawa anamwambia mchumi wa manispaa kuwa aongee na huyu chotara vizuri wakielewana tumpeleke kwetu Morogoro akale wali unaonukia mwaka mzima. Chotara anafahamiana na Baraza na chotara hataki usumbufu wa Baraza. Hapa ndani ya hiace chotara akiwa kimya tu na hiace ilipofika kwa Chang’aa Mwanakwetu na chotara wakashuka, nia ya chotara ni kumkwepa Baraza , kwa hiyo Mwanakwetu akasindikizwa hadi kwake , kikapikwa chakula na kuliwa ambapo bahati hiyo Rashidi Baraza hakuipata, baadaye chotara kuondoka zake kwenda kwake na siku hiyo ilikuwa wakati wa likizo.


 

Mwanakwetu aliendelea na masomo huku akimtembelea chotara kwake na hivyo hivyo Mwanakwetu alitembelewa kwake na kila Mwanakwetu alipokutana na Baraza alikuwa haamini anachoambiwa na Mwanakwetu kuwa chotara ni rafiki yangu na urafiki wao hauvuki mipaka.

Mwanakwetu aliendelaa na masomo na akiwa chuoni alibaini kuwa yale yaliyosemwa na Albart Kwazala yalikuwa ya kweli walikuwepo wanachuo wengi walimu waliyokuwa wakisoma kozi zingine na huku wakiwa na ruhusa, kwanini Mwanakwetu anyimwe ruhusa?

Mwanakwetu alikwenda wizarani na kumuona Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi mwalimu Margreth Sitta na kumueleza shida kwa ushahidi . Waziri akaimbia Kurugenzi sekondari ijibu hoja na ifanye maamuzi mara moja, Kwa hekima kurugezi sekondari ilitolea ruhusa na kuagiza Mwanakweu alipwe mishahara yake yote.

“Kwani akimaliza masomo atakwenda kuitumikia Jamhuri ya Kenya? Kama atabaki hapa hapa Tanzania mrudishieni mishahara yake mara moja.”

Mwalimu Margareth Sitta alipigilia msumari wa moto katika maamuzi hayo.

Kurugenzi ilifanya hivyo na kurejesha mishahara ya Mwanakwetu yote, chotara alilipwa 30,000 yake naye mkubwa Albart Kwazala alilipwa 240,000 ya zile 30,000 za miezi nane na baada ya muda mhasibu Albart Kwazara alihamishiwa Chuo cha Ualimu Songea na nadhani atakuwa amestaafu kwa sasa .

“Kwa heshima ya Albart Kwazara jina Albart amepewa kijana wa Mwanakwetu ambaye sasa yu kidato cha kwanza akifahamika kama Albart Makwega kutokaa na kisa hiki.”

Popote ulipo mhasibu Albart Kwazala shikamoo na nakutakia heri na fanaka.


 Aliyeshika tamaa ni Ramadani Baraza, huyu ndiye  baraza mdogoMuenezi  CCM iringa.

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Shabaha ya kwanza ya makala haya, kila binadamu anapitia changamoto za maisha ambazo majibu yake ya utatuzi yapo kwa jamii hiyo hiyo rejea msaada mkubwa aliyopewa Mwanakwetu kutoka kwa chotara wa Kinyakyusa na Kihaya pale alipoumwa jino , rejea ushauri wa mawazo msaada wa fedha kutoka kwa Albart Kwazala.

Pia msomaji wagu rejea uwezo wa mwalimu Margreth Sitta wa kutatua changamoto za wizara yake akiwa waziri ambapo ulitokana nayeye kuwa mwalimu wa muda mrefu , kuwa afisa elimu kwa mua mrefu, kuwa kiongozi wa Chama Cha walimu Tanzania (CWT) .Waziri yoyote ili afanye kaz vizuri na ili serikali isipate aibu lazima awe na uzoefu na wizara anayoingoza wa muda mrefu.

Je wewe waziri wa leo unawahudumia Watanzania kwa kiwango hicho? Je kama ukisimuliwa zitakuwepo simulizi  chanya?


 Huyo jamaa mwneye kaba shingo nyekund nidiye aliyechukua jina la Albart Kwazala

Katika makala haya kuna maelezo haya,

“Mwanakwetu aliendelaa na masomo na akiwa chuoni alibaini kuwa yale yaliyosemwa na Albart Kwazala yalikuwa ya kweli walikuwepo wanachuo wengi walimu waliyokuwa wakisoma kozi zingine.”

Shabaha ya maelezo haya ni kuwa ikiwekwa kanuni katika masuala ya umma itende haki kw wote bila kubagua  ikibagua tu hapo ni tatizo na kanuni hiyo inakuwa batili.

Shabaha ya mwisho ya makala haya ni kujibu maswali ya wasomaji yaliyoulizwa baada ya makala ya kwanza kutoka. Naendelea kuyapokea maswali yale ambayo yanaweza kujibika huku nikiendelea kuheshimu haki za kadhaa za wahusika kadhaa katika makala haya mathalani matumizi ya jina chotara badala ya jina halisi la mhusika na nimebaini chotara mwenyee ameyasoma makala haya.


 

Mwanakwetu upo?

Kumbuka,

“Kijana Mzuri Shida hajaokoka.”

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257


 

 

0/Post a Comment/Comments